Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yaani wanatuhumu wazungu kwann hawajaleta chanjo. Mpaka hapo wanaonyesha jinsi gani mzungu anategemewa hapa ddun
Hawakubali kivipi? Lini alihitaji kwenda kwao akakataliwa?Sio kigezo cha kusem kuwa ndio hajatawaliwa kifikra kam sio kwann toka aend ulaya akidai kurud kwao ethiopia hawakubal mkuuu angalia
Big No.Wala siyo kwamba hatuwezi kutengeneza chanjo zetu na wala si kwamba hatuna akili. Tatizo kubwa ni ukoloni, na miaka ile ilikuwa ni ukoloni wa kutawala kimabavu moja kwa moja ila kwa zama hizi ni ukoloni wa kutumia mifumo. Njia za ukoloni ni tofauti ila matokeo ni yale yale. Kazi kubwa ya mkoloni ni kuhakikisha kwamba anaondoa ile hali ya kujiamini na kujithamini kwa yule anayemtawala. Kwa ukoloni wa sasa hivi mifumo kama WHO, IMF n.k inahakikisha inatengeneza mazingira uone kile unachokifanya nje ya mifumo yake hakina uhalali wala hakina matunda. Na ndicho tunachojaribu kupandikiziwa ili tuwasubiri wao, tufanye yao na tuwasikilize wao tu.
Mtu yeyote huru au nchi yoyote huru haiwezi kusubiri WHO anasema nini. Wanafanya mambo yao. Kuna mtu mmoja hapo juu kauliza eti WHO ni akina nani kama si nchi zote? Mi nimebaki kumshangaa maana wakati mifumo hii inaanzishwa baadhi ya nchi zilikuwa hata hazipo ikiwemo na nchi yetu. Sasa mifumo wajitengenezee wao, wewe upachikwe tu na kulazimishiwa halafu useme huo mfumo upo kwa interests zako? Unaweza usijitoe lakini unaweza pia kukubali uhalisia kuwa ile mifumo ilitengenezwa kulinda maslahi ya wenye nguvu. Kama kuna kifaida tunakipata kwa kuwemo WHO au IMF au whatever, kuna faida kubwa wanaipata wale wenye hisa kubwa katika mifumo hiyo.
Mbaya zaidi aliye andika utakuta ni mtu wa HKL tena mwenye four alafu anakaa anajifanya amekua dokta.WHO hawasemi njia za kupambana na corona afrika(tropical) au nchi zenye joto. Wanasemea tu ulaya na marekani nchi baridi, kweli wanamuambia mtu dar ajifungie na joto za dar kweli,barakoa zenyewe sehemu za joto unyevu na joto hewa inapungua. Kujifungia kwenye joto na unyevu joto barakoa ,tuko salama?
Hebu chek profile pic yangu uyo ndyo professor baridi unayezungumzia?Ukiona Dr. Anaongelea jambo fulani tafakari kwa kina ...Usichukulie kawaida Sanaa maana Dr. Ni profesa baridi.
Kuna unafiki sana kwenye hii pandenic ya corona na namna inavyoshughulikiwa na hizi taasisi za kimataifa. Mtu mwenye fikra huru atakwambia "to hell with corona na politics zake" maana ukichunguza kwa kina kuna ubinafsi na uongo uongo mwingi uliojificha nyuma ya mwamvuli wa "sayansi".
Ok, vaccine za kwanza kuhusiana na corona ni zile za China na Urusi. Ila dunia pamoja na WHO imetuaminisha kwamba zile hazipaswi kupewa air time mpaka tusubiri za Ulaya na Marekani. Magu akitilia mashaka hizi motives anakuwa amekosea?
Haya, wakati wa maelekezo ya kupambana na corona - social distancing, kuvaa mask, bla bla... - WHO walikuwa wanasifia nchi flani flani za kiafrika zilizokuwa zinatekekeza maagizo hayo kama marobot. Sasa hivi kuna vaccines za corona ila tunaambiwa kwamba nchi za kiafrika zitaanza kupata dose zake kuanzia labda mwishoni mwa mwaka 2021.
Nchi inayojitambua na kama unajitambua huwezi kuweka tumaini lako kwenye vaccine za corona ili kupambana na corona. Magu kashasoma hilo gemu lote na yupo sahihi kusema kwamba maisha ya watanzania kwenye corona version 1 hayakusubiri vaccine, na pia hayatasubiri vaccine kwenye corona version 2. Ni upuuzi kutegemea corona vaccine unayoweza kuipata mwaka 2022. Ina maana basi maisha hayataendelea hadi tusubiri vaccine ya 2022 tena wanayotuchagulia wao? Umaskini wa fikra ni umaskini mbaya sana.
Kama kawaida yao walikaa wakajifungia wakaangalia projections ya ukuaji wa uchumi wao wakaona mchina anawatimulia vumbi kila walichokuwa wanamtishia anacho na vingine anavyo vya ziada yaani ana mtaji wa rasilimali watu,
Iko hivi walipoona viashiria vyote vya Ufalme wa China kwenye uchumi wa Dunia walijipanga kumdhibiti mchina kwa kumharibia taswira yake kiuchumi ndio maana wanajeshi wa Marekani wakishirikiana kwa karibu na Taasisi za kijasusi za Marekani walifanikiwa kuisambaza Corona iliyorutubishwa China
Mapema sana baada ya kuusambaza WHO ilishinikizwa itoe maelekezo ya kuiblock China na kuitangaza kwa mitazamo hasi
China kupitia kampuni yake ya HUAWEI ilisaidia majasusi wa kichina kuujua mpango kamili, China wakamuita Mkurugenzi mkuu WHO wakampanga mapema kabla ya Trump hajailazimisha WHO kuiblock China
.
Mkurugenzi WHO walikuwa na kiburi cha kutofuata maagizo ya marekani kwa sababu aliahidiwa murungura maradufu
.
Haya mambo sisi Waafrika tuko kwenye mkumbo tu lkn wababe wanaogombania Ufalme wa Dunia ndio wanaopigana kuhakisha kwamba wanzimana waendelee kutawala
..
Na wewe kificho una comment gani katika hili ?Daaaaah!!
Ninachosikitika aliandika uzi huu ni kipenyo alielewa kvant..
Kipenyo hawezi kuwa wa quality hiiDaaaaah!!
Ninachosikitika aliandika uzi huu ni kipenyo alielewa kvant..