- Unajua mkuu Bubu, maneno yako ni sawa sawa, lakini ni lazima sasa Tanzania tukubali kwamba ya kubadili cabinet na kujizulu viongozi wa chini hayajatusadia sana so far as a nation, wakati umefika sasa kwenda mbele zaidi na uwajibikaji, majuzi kwenye kikao chake cha siri na baadhi ya mawaziri, Muungwana ameambiwa wazi kwamba wamejiuzulu wengi na wengi kuondolewa lakini bado kivuli kipo pale pale, hapa kinacho-miss ni kimoja tu nacho ni huenda ni wakati muafaka wa yeye mwenyewe mkulu wa kaya kujiuzulu au viongozi mafisadi waende mahakamani na wafungwe wakipatikana na makosa.
-- Lakini huwezi kuwa na utawala wa kuheshimu sheria, kwamba mawaziri wa zamani wako rumande huku nyuma wanatokea mawaziri wako wewe mwenyewe rais kuwatafutia mawakili, sasa tutabadili cabinet mpaka lini na mauza uza kama haya? unaaanza kufikia mahali sasa tuanze kufikiria mbele zaidi ya mawaziri na uwajibikaji!
Mama Siti Mwinyi alikamatwa na Mrema pale Dar Airport akitokea Z'bar na madini . Kama tujuavyo Z'bar hakuna madini yoyote ana likuwa anayasafirisha nje ya nchi ili akachangamke na kuyauza. Hiyo si siri, pia kulikuwa na ufisadi mwingi tu wakati wa awamu ya pili hiyo si siri. Sasa kudai wakati wa enzi za Nyerere kulikuwa na kunguni wengi na kusahau kunguni waliokuwamo ndani ya awamu ya pili, ya tatu na ya nne ni unafiki wa hali ya juu.
Anamsifia Kikwete kafanya mazuri, sijui mazuri gani aliyoyafanya, maana katika ahadi zake wakati wa kampeni hakuna hata moja aliyoitimiza.
Wako watu wanalima mchicha, kufunga ng'ombe wa maziwa n.k. hawa wanaishi kwa kipato halali siyo kama wanaotaka uongozi ili wakaitumie Ikulu kufanya uharamia wao na kuwafisadi Watanzania na kukidhi uroho wao wa utajiri wa haraka haraka.
Sasa kwanini ulishindwa kusema yote hayo wakati una-introduce mada na badala yake ume-copy na ku-paste.
Kwani kufanya hivyo ni dhambi!? Tangu lini? Unaweza ukatuma habari toka popote pale na ikawa ni kichocheo cha mjadala kama huu unauona hapa. Halijaharibika neno pamoja na kucopy na kupaste.
Hiyo ni dhambi kwa sababu unavunja haki miliki za watu. Mtu anaye-poach habari kutoka website zingine ana tofauti gani na fisadi. Mwandishi ametumia siku nzima kuandaa kazi yake. Na akisha-publish haichukui dakika tano wewe kuivuta. That's not so cool.
Hiyo ni dhambi kwa sababu unavunja haki miliki za watu. Mtu anaye-poach habari kutoka website zingine ana tofauti gani na fisadi. Mwandishi ametumia siku nzima kuandaa kazi yake. Na akisha-publish haichukui dakika tano wewe kuivuta. That's not so cool.
Hivi unafikiri hao wenye magazeti yao Tanzania hawazioni articles zao mbali mbali zikitumwa hapa jamvini!? Wengine wanaona ufahari mkubwa kuona articles zao zimeanzisha mjadala mkubwa hapa jamvini na huthubutu hata kuchungulia kuona kama articles zao zimeshatundikwa hapa jamvini.
Provided situmii hizo articles zao kuziuza ili kujinufaisha basi hakuna lalam na kama kungekuwa na malamiko basi tungeshayasikia miaka mingi iliyopita maana wanajua lengo la kuweka articles zao hapa ni kujenga na siyo kubomoa. Na sikun zote huwa nahakikisha articles zote nazoziweka hapa naonyesha zimetoka katika magazeti gani ya Tanzania.
Zakumi unaweza kuipa nguvu hoja yako kwa kuweka vifungu vya hakimiliki kutoka magazeti haya?
Bubu un aweza kuweka links za habari hizi? Waandishi wengi ukiweka link inakuwa unawaongezea traffic kwenye sites zao, that's the least you can do while opy pasting.
Traffic zinaongeza hits ambazo zinaongeza matangazo ya biashara katika site hizo na mapato.
Hivyo kutoka katika business na innovation point of views bubu anawarudisha watu nyuma.
Traffic zinaongeza hits ambazo zinaongeza matangazo ya biashara katika site hizo na mapato.
Hivyo kutoka katika business na innovation point of views bubu anawarudisha watu nyuma.
Mzee Mwinyi ni kunguni mwingine tu aliyetafuna taifa. Yeye na mkewe ndio walikuwa wa kwanza kuanzisha biashara Ikulu, wakituuzia Stella Artois na majenereta ya umeme. Sasa anasema nini kuhusu kunguni? It takes one to know one.
Hivi DDT au Expel. or Doom haziu kunguni? si mzee Ruksa angewapulizia hiyo dawa kunguni wangekufa. ( kwanini hakuchukua hatua za kuwa maliza kunguni?)
Kwanza amekosea kusema Watanzania wenyewe walikubali mfumo wa vyama vingi.. sii kweli ukisoma maelezo baada ya maneno hayo..amesema asilimia 80 walikuwa against vyama vingi huwezi kusema Watanzania wenyewe walikubali..Alisema wapinzani sio maadui, na kwamba Watanzania walikubali wenyewe mfumo wa vyama vingi, yeye akiwa mwasisi wa mfumo huo, licha ya kwamba asilimia 80 walikuwa wameukataa maoni ya asilimia 20 ya watu waliohojiwa yalikubaliwa.
Lakini rais huyo mstaafu tangu mwaka 1995, aliwatupia wapinzani dongo la kushindwa kwao kukua: "tangu wakati huo wamebaki na asilimia 20 zao na CCM imebaki na ushindi wake wa asilimia 80," alisema.
Wewe unataka kutetea mazoea yako ya kifisadi. Nenda kwenye therapy.
Hata wananchi wa Tanzania wanaona ufahari kwa kuwachagua viongozi wanaowapa pilau zinazotokana na ufisadi.
Hivi DDT au Expel. or Doom haziu kunguni? si mzee Ruksa angewapulizia hiyo dawa kunguni wangekufa. ( kwanini hakuchukua hatua za kuwa maliza kunguni?)
Mkuu hebu tutajie biashara alizomiliki Mwinyi akiwa ikulu na anazomiliki sasa baada ya kuondoka ikulu.Repoti ya Warioba ilishindwa kutaja zaidi ya kuorodhesha kuwa Mwinyi aligawa viwanja bure kwa jamaa zake au hiyo ndio biashara ?