Mzee Mwinyi ni kunguni mwingine tu aliyetafuna taifa. Yeye na mkewe ndio walikuwa wa kwanza kuanzisha biashara Ikulu, wakituuzia Stella Artois na majenereta ya umeme. Sasa anasema nini kuhusu kunguni? It takes one to know one.
...dah,
...nikikumbukia miaka ile, bora Mzee Ruksa aliyeanzisha biashara ikulu. kwa hali ilivyokuwa, ilibidi huyu mzee anywe nao chai ikulu kuwarudishia imani wafanyabiashara badala ya zile enzi tulivyokuwa tuna tafuna mpaka dola moja ya mmarekani tusijekamatwa ulanguzi uchumi!
...maisha gani yale ya kujivunia, eti mtu akitoka safari zawadi kuuubwa ni sabuni ya Lifebuoy, Lux, Imperial leather au Colgate? ...tuliokogea sabuni za 'magwanji' cha moto tulikiona kwa muasho.
...Basi mpaka nyembe ya Topaz nayo ilikuwa ngumu kuipata? maduka yamejaa vibiriti na majani ya chai tu?...
...yaani ilifikia hata shuleni, watoto wanavaa katambuga na mashati ya 'maradufu'? umasikini gani ule? Ukibahatika kuvaa shati la tetroni basi usipite karibu na moto.
...Kwa waliopitia boarding school nadhani mtakumbuka
full-suit, ...enhe ule ugali wa yanga na dengu! huchelewi kutoka povu kinywani ukiufakamia!
...kuletwa Stella Artois angalau basi watu walipata vionjo vipya badala ya Pilsner, Safari, Ndovu na Kilimanjaro wakati huo, maana
hang-over za hizo beer ukiamka umeze tembe.
...angalau basi hayo majenereta ya umeme yalikuja'tufaa majumbani badala ya mishumaa ambayo pia ilikuwa kimeo! ajabu yenyewe hata sukari ya nchini ilikuwa kimeo kuipata, wananchi tukalazimika kunywa chai na sukari guru.
...sioni tofauti ya Tanzania ya wakati ule na yanayowakumba wazimbabwe huko nchini kwao sasa.
...acheni nyie bwana, Mzee Ruksa pamoja na mapungufu yake (yalokuwa nje ya uwezo wake), ametukomboa!