Who influenced Nyerere: His Ujamaa Philosophy and Azimio Principles?

Mkuu heshima mbele sana, elimu ni kichwa cha mtu na sio utoto wa rais, Magige ni Electrician tena wa Mlimani enzi zile, Madaraka anamiliki Masters, shule walisoma hizi zetu kama sisi makabwela lakini at the end of the day, kilicho-matter ni akili kichwani kitu ambacho it does not matter wewe ni mtoto wa nani, kama unazo unazo kama huna huna!

Siasa nyingi za Mwalimu hazikuwa safi kwa muangalio wangu na wako, lakini are better off now as a nation kiuchumi kuliko under Mwalimu? Au uhuru wa kuongea peke yake unatosha? Hivi ni kweli tuko huru kuongea?

I mean tumetoka kwenye one misery tumeingia kwenye misery mpya, lakini mazingara tofauti, hakuna sababu ya kulumbana hapa maana kina Kikwete, Lowassa, Rostam, Mkapa na Karamagi, wakiona hii mijadala watalala vizuri sana usingizi wao!

FMES,mi sikutaka kuchangia point ya huyo bwana kwa sababu bado nilikuwa nacheka.
 
mwalimu ni mdesaji mzuri wa michanyato ya falsafa mbalimbali, na kiutendaji alikuwa ni mdesaji pia.

nakumbuka ule mwimbo mzuri wa wa wakati ule ''eh eh sasi jabela mwitu; naye akadesa oh oh TANU yajenga nchi....." na ukawa pambio kwa shughuli za wadanganyika wale.

Ukijenga falsafa, lazima uwe na nguzo ya wanafalsafa wadogowadogo ambao wanaweza kuitafsili falsafa yako na kuitelemsha chini katika ngazi ya kaya. hilo halikuwepo na hapo muheshimiwa alikuwa anacheza RAMBO style... "one man army" Tuchukulie mfano mdogo, tunasema kampuni fulani imefanikiwa katika kuongeza faida katika mradi wake (ROI) ni kwakuwa ina CEO makini ambaye amezungukwa na wakurugenzi makini.... na kila mmoja kwa nafasi yake huwa na maano yaleyale ya CEO wake. Hilo kwa Tanganyika ya mwalimu lilikuwa ni mazingaombwe tu.... ali zawadi kuja...wanasema kuja... siri yote alijua yeye... waliochini yake walipokea maono yake kwa kumpigia makofi tu na si kwavitendo. Ndio maana katika moja ya hotuba zake za mwisho mwisho mwalimu alirejea kulizungumzia azimio la Arusha na kusema kuwa haoni tatizo lolote katika misingi yake.... haina makosa kabisa.... Tatizo lilikuwa ni katika kuitafsiri hasa kwa watendaji wake...
 
...If in your eyes he fell short basi kawaachieni mantle. Kuna usemi wa siku nyingi Marekani kwamba usimkosoe Mhindi wa asili mpaka umetembea kwenye moccasins zake. The same applies to Julius. Tanganyika ya 1961 si Tanzania mliyozaliwa ndani yake. Hilo vijana shurti mlielewe ama mtajikuta mnafanya makosa ya ajabu kabisa kuliko hata yale mnayomhukumu Julius.

Basi msiwe mnabisha kwamba hakuharibu.
 
Mbona nimeshuhudia hapa vijana wakijaribu zaidi kulazimisha point zao kwa kuita wengine majina ya kashfa? Unaweza usikubaliane na mengi aliyoyafanya Mwalimu Nyerere lakini haingii kwenye kundi moja la kuitwa nduli kama Idi Amin. Unaweza usikubaliane na mimi lakini you do not have to call me names. Gonga hoja kwa hoja usiniite naive, because I have not called your points naive. So it goes both ways. Remember that when one finger points at me 4 are pointing at you. Changamoto kwenu vijana: kujeni na sera zitakazoiendeleza Tanzania. Nyerere did his best, amewaachieni mantle. Sasa tuambieni mna vision gani badala ya kukaa na kulalama tu miaka 23 tangu mzee wa watu aachie ngazi na 9 tangu aende kwa mola wake.

Jasusi:

Nyinyi mliolelewa kwenye sera ndio mnaboronga. Vijana wengi tunaelewa kuwa tunaishi kwenye Globalization. Na katika Globalization, Mmarekani ambaye ameshindwa kulipa mkopo wake wa Nyumba anaweza kuiangusha investment funds ziliyopo China, Dubai au German. Na athari zake kuongeza bei ya mafuta, kupunguza watalii wanaokuja Tanzania na matokeo yake kumfikia babu yangu aliye kijijini ambaye hana uhusiano wowote hule na mkopo wa nyumba uliochukuliwa Marekani.

Unapozungumza sera, unazungumza mipango ya muda mrefu. Mipango ya muda mrefu sio cost effective na inayohitaji watu mahili katika management. Watanzania tuna upungufu mkubwa katika umahili wa management na hili ndio kitu kimoja tunachotakiwa kujifunza baada ya kuboronga kwenye siasa za ujamaa.

Nitajie mradi mmoja mkubwa tu ambao ulisimamiwa na watanzania na kumalizika bila matatizo na kuleta mafanikio kwa taifa bila kuwa na mkono wa nchi za kigeni?

Tanzania inahitaji viongozi walio Game Players. Ukiwa unacheza game kama vile chase au bao, katika kila step kuna njia zaidi ya elfu za kuchagua. Na uchanguzi wa step inayofuata unategemea sana na mchezaji unayeshindana naye.
 
Sasa vijana uwanja uko wazi kwenu Game Players kuingia mfanye vitu vyenu katika ulimwengu huu wa Globalization. Badala ya kukaa na kulalamika tu jikusanyeni mtuonyeshe sisi tuliopitwa na wakati kwamba mnaweza kufanya kweli. It is that simple.
 
In summary:

Mwalimu alijenga taifa la Tanzania, Warithi wake wanalibomoa

TANU ilijenga nchi, CCM ikabomoa kila kitu.....

Tanzanianjema

As if mwalimu hakuanzisha ccm...As if hakusema wananchi wenye mawazo tofauti na ccm ni wasaliti.
Jasusi bado hamjajibu kuhusu mwalimu kukabidhi nchi kwa Mkapa na kuuzwa moja kwa moja....Talking bout LEGACY...
 
Inawezekana Rev unayosema ni sawa lakini labda tufanya uchunguzi wa kina zaidi tunaweza kujua ni nini Julias Nyerere alikuwa anafikiria kwani mzee wetu yule ni vigumu sana kumtabiri kwani hata alipokubali Vyama vingi watu wengi walishanga inakuwaje Mhimizaji wa Chama kimoja yupo mbele kuimiza vyama vingi na wakati huo huo kupinga kwa nguvu zote ubinafsishaji hasa pale alipomjibu mwandishi wahabari wa western pale alipouliza swali kwamba mabanki yetu ni makubwa na yanahitaji kubinafsishwa, kwa wote wanaokumbuka Marehemu alimuuliza na yeye swali je NBC kipindi hiki ni kubwa kuliko Barclays.
 
Sasa vijana uwanja uko wazi kwenu Game Players kuingia mfanye vitu vyenu katika ulimwengu huu wa Globalization. Badala ya kukaa na kulalamika tu jikusanyeni mtuonyeshe sisi tuliopitwa na wakati kwamba mnaweza kufanya kweli. It is that simple.

Kama wazee kweli wangetoa nafasi kwa vijana kuleta maendeleo ndiyo wangekuwa na haki ya kusema hayo unayoyasema. Lakini tangu nikiwa mdogo mpaka sasa niko 36 years bado nasikia uleule usemi vijana Taifa la kesho. Akina JKN na team yake walianza kuongoza wakiwa kwenye 30s lakini hawakujua kuwa walikuwa ni vijana ila ni sisi tu tuliofuata nyuma yao. Ndiyo maana mpaka leo akina Malecela, Kingunge, Msekwa n.k. bado wamo tu wanataka kufia madarakani na bado watasema Vijana ni Taifa la leo. Unless unyweshwe maji ya bendera ya CCM kama akina Nchimbi, Matayo nk. ndiyo utaweza kupenetrate kwenye serikali ya CCM otherwise kama siyo mtoto wa kigogo sahau!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Vijana msingojee kupewa nafasi kwenye sahani. You seize the moment. Mwangalie kijana Obama anavyofanya vitu vyake Marekani. Hakusubiri kupewa nafasi, aliichukua akianza kama community organizer Chicago, akagombea ubunge wa jimbo hatimaye senate na sasa anayoyoma Ikulu.
Siyo lazima uwe CCM. Unaweza kujiunga na CUF au CHADEMA na kuanzia kwenye grassroots. Time is on your side.
 
Vijana msingojee kupewa nafasi kwenye sahani. You seize the moment. Mwangalie kijana Obama anavyofanya vitu vyake Marekani. Hakusubiri kupewa nafasi, aliichukua akianza kama community organizer Chicago, akagombea ubunge wa jimbo hatimaye senate na sasa anayoyoma Ikulu.Siyo lazima uwe CCM. Unaweza kujiunga na CUF au CHADEMA na kuanzia kwenye grassroots. Time is on your side.

Jasusi, taratibu braza. Hii ngoma bado kabisa na siku ya siku ikifika McCain anaingia White House kama analia vile.....
 
Nilijua tu kuwa hiyo kauli itakutoa msituni, kwi!kwi!kwi! But you gotta give him credit for his organizational skills, no?
 
As if mwalimu hakuanzisha ccm...As if hakusema wananchi wenye mawazo tofauti na ccm ni wasaliti.
Jasusi bado hamjajibu kuhusu mwalimu kukabidhi nchi kwa Mkapa na kuuzwa moja kwa moja....Talking bout LEGACY...

Kitu kinachoitwa Legacy kinawapiga chenga watu wengi. Na nitajaribu kuelezea kwenye posti ya kumjibu Jasusi.
 
Nilijua tu kuwa hiyo kauli itakutoa msituni, kwi!kwi!kwi! But you gotta give him credit for his organizational skills, no?

Hahahahaaaa...kumbe uliichomekea kwa makusudi eeh.....hahahaha.....haya bana.....

But yeah...he does get some credit....
 
Sasa vijana uwanja uko wazi kwenu Game Players kuingia mfanye vitu vyenu katika ulimwengu huu wa Globalization. Badala ya kukaa na kulalamika tu jikusanyeni mtuonyeshe sisi tuliopitwa na wakati kwamba mnaweza kufanya kweli. It is that simple.

Jasusi:

Ujana sio kitu cha msingi sana kama fikra zako bado zitakuwa kama mzee. Vijana wa Tanzania wengi bado wanazitumikia legacy za Nyerere kama benchmark ya maendeleo.

Kinachotakiwa Tanzania sio vijana bali Enlightenment Figures watakaowasha Renaissance yetu.
 
huwezi kuwasha renaissance pasipo kujenga fikra zako na kuweka msingi wa hiyo renaissance. Ni lazima uwe na principles ambazo zitakuongoza kuwasha renaissance (mwamko) hiyo.
 
Vijana msingojee kupewa nafasi kwenye sahani. You seize the moment. Mwangalie kijana Obama anavyofanya vitu vyake Marekani. Hakusubiri kupewa nafasi, aliichukua akianza kama community organizer Chicago, akagombea ubunge wa jimbo hatimaye senate na sasa anayoyoma Ikulu.
Siyo lazima uwe CCM. Unaweza kujiunga na CUF au CHADEMA na kuanzia kwenye grassroots. Time is on your side.

Siyo suala la kuletewa kwenye sahani. Tatizo hawa jamaa wana zile siasa za zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa CCM. Wewe si ulishasikia jinsi gani watu wanapitishwa na wananchi kwenye kura za maoni halafu wanaenguliwa na NEC. Mfano mzuri nakumbuka ulikuwa wa Tatu Ntimizi, alikuwa wa tatu kwenye kura za maoni lakini NEC ikapitisha ikamuacha chaguo la watu. Prof. Maghembe alibidi asubili Mzee C. Msuya achoke ndiyo avutiwe pale. Mkuranga ilibidi waanzishe jimbo la uchaguzi ili Hussein Mwinyi awe mbunge..... Mifano ni mingi tu kama unataka. Masikini Danganyika!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mr. Zero,
Ndio maana nimeshauri muangalie vyama mbadala. Hamna haja ya kung'ang'ania CCM. Nakubaliana na mifano yote uliyotoa. Jiungeni na vyama vya upinzani msaidie kujenga upinzani na demokrasia halisi Tanzania.
 
huwezi kuwasha renaissance pasipo kujenga fikra zako na kuweka msingi wa hiyo renaissance. Ni lazima uwe na principles ambazo zitakuongoza kuwasha renaissance (mwamko) hiyo.

Naona ukupitia posti yote. Nimesema tunahitaji Enlightenment Figures. Hiyo ni principle ya kubwa.

Aliulizwa mwanafalsafa mmoja. Tupunguze vitu na watu wa nafasi zipi hili shule ibakie shule. Akajibu punguzeni vitu vyote na watu wote, lakini mkibakiza wanafunzi bado itakuwa shule.

Wakamuuliza tena je hao wanafunzi watafundishwa na nani? Akasema huwezi kuwa mwalimu bila kuwa mwanafunzi.

Kwa mtaji huu misingi, fikra na principles unazozitaka zitoke miongoni mwetu.
 
Watanzania tuna upungufu mkubwa katika umahili wa management na hili ndio kitu kimoja tunachotakiwa kujifunza baada ya kuboronga kwenye siasa za ujamaa

Mkuu haya maneno ni mazito, lakini kubali kuwa tatizo hili halikuletwa na Mwalimu, ila ni sisi wenyewe wananchi wa bongo,

USA it took mtoto wa mzungu na African man, yaani Jaluo kuwafundisha weusi kule kua matatizo yetu ya kuwa watumwa huko nyuma yasiwe kisingizio cha kutojiendeleza na kubeba resonsibilities zetu as people, na weusi tunaweza kuwa marasi wa US pia na kuleta mabadiliko, badala ya kukaa kulaumu mzungu to for this and that!

Na sisi bongo ufike wakati tujifunze kusonga mbele, maneno tumesema mengi mno labda sasa ni wakati wa kuonyesha kwa vitendo makosa ya Mwalimu, kwa kufanya yaliyo sawa kwenye kizazi hiki, ama sivyo Mwalimu ataendelea kututawala kama wazungu wanavyotawala vichwa vya weusi kule US!

Thanx to Jaluo, labda bongo tutampata the Jaluo likes hivi karibuni, kwa sababu Kikwete sio mwenyewe kama walivyotumabia manabii!
 
Naona ukupitia posti yote. Nimesema tunahitaji Enlightenment Figures. Hiyo ni principle ya kubwa.

Aliulizwa mwanafalsafa mmoja. Tupunguze vitu na watu wa nafasi zipi hili shule ibakie shule. Akajibu punguzeni vitu vyote na watu wote, lakini mkibakiza wanafunzi bado itakuwa shule.

Wakamuuliza tena je hao wanafunzi watafundishwa na nani? Akasema huwezi kuwa mwalimu bila kuwa mwanafunzi.

Kwa mtaji huu misingi, fikra na principles unazozitaka zitoke miongoni mwetu.

well, wako wapi hao "enlightment figures" na tutawatambuaje?
 
Back
Top Bottom