Date::2/7/2009
Kunguni waliupekecha ujamaa TanzaniaMwinyi
Katika mkutano huo pia Mwinyi alivaa sura ya ubaba wa taifa kama alivyofanya akiwa Mbeya Vijijini, alipowataka wapiga kura kuchagua kiongozi wanayeona anafaa bila kujali vyama, pale aliposisitiza ushirikiano baina vyama vyote vya siasa, akiwataka wana-CCM kuimarisha uhusiano na vyama vya upinzani.
Alisema wapinzani sio maadui, na kwamba Watanzania walikubali wenyewe mfumo wa vyama vingi, yeye akiwa mwasisi wa mfumo huo, licha ya kwamba asilimia 80 walikuwa wameukataa maoni ya asilimia 20 ya watu waliohojiwa yalikubaliwa.
Lakini rais huyo mstaafu tangu mwaka 1995, aliwatupia wapinzani dongo la kushindwa kwao kukua: "tangu wakati huo wamebaki na asilimia 20 zao na CCM imebaki na ushindi wake wa asilimia 80," alisema.
.
Hapa Mzee Mwinyi umesema kweli wakuchaguliwa ni yule anayefaa. Lakini kwa hili la wapinzani kubaki na 20% ni kwamba bado CCM inapekechapekecha upinzani kama Kunguni kwa sheria mbovu, tume ya uchaguzi, kuiba kura nk