Umesema yote. CDC na WHO wanafanya approach ambayo ni suitable au ambayo ni befitting na mfumo wa utawala wa Awamu ya 5. Kwenye awamu hii kuficha takwimu au kuchakachua takwimu imekuwa ndiyo norm. Wenyewe wanaita MATAGA.
Dr Mwele Malecela (PhD), alifukuzwa kazi kama mbwa kwa kufanya kazi kwa weledi. Aliposema kuna dalili za ugonjwa wa Zika mwaka 2016 akaonekana ana dhalilisha nchi. Professionally baada ya pale ilipaswa kuchukua samples na kwenda ku-test laboratory wakati tahadhari ya kuzuia maambukizi zikifanyika.
Baada ya Dr Mwele kuondoshwa NIMR sidhani kama aliyechukua nafasi ile anatekeleza majukumu yake. Anaweza akawa ana weledi lakini anaogopa yasimpate yaliyompata Dr Mwele. Wakati wa Dr Mwele hata Mtanzania wa kawaida alijua kuna NIMR ila kwa sasa sidhani.
Kama NIMR ingefanya kazi zake kwa uhuru na kadri Sheria inavyotaka basi tusingesumbuliwa kiasi kile na ugonjwa wa homa ya Dengue.
Homa ya Dengue imeua watu kwa maelfu kuanzia mwaka jana hadi katikati ya mwaka huu wa 2020. Nina uhakika wataalamu walikuwa wanajua lakini nani aseme kuwa ni homa ya Dengue. Wanaogopa kutumbuliwa kama Mwele, wamewaachia wanasiasa ndiyo washughulikie.
Likewise kwenye hiyo Ebola, ndiyo maana hawa WHO wameita unknown disease.
Nashauri kwenye vitu serious kama takwimu au dalili za uchumi na ugonjwa Serikali iache 'rigging', unaweza uka 'rig' takwimu za election ila huwezi ku 'rig' takwimu za uchumi na afya.