===
ILANI:
Sina shida kabisa kama watu hawa wamelipa pesa walizosema watalipa ila endapo hawajatoa pesa na wamekuja kutafuta kiki kwetu ni vyema tuwachambue kwa umakini. Aidha, napata shaka kuwa kuna mtu nyuma ya kampuni hii ambaye soon tutamjua na tutajua lengo lake.
===
Mkuu
Mkirindi,
Mimi Intelligence ya siku hizi inanishangaza inavyofanya kazi yake. Hakuna kitu kinasikitisha kama kuwa na Idara ya Usalama inayohangaika kudhibiti wananchi kwa maslahi ya 'tabaka tawala' badala ya kulinda maslahi mapana ya Taifa.
Ninachokijua mimi ni hiki:
1) Kampuni ya INDO Power Solutions imesajiliwa nchini Kenya mwaka 2016 ikionyesha inamilikiwa na watu wawili:
a) Joyce Waithira Gatoho na
b) Alice Wanjiku Gatoho
View attachment 1010458
Lakini, kinachoshangaza kidogo hapa ni kuwa pamoja na uchanga wa kampuni hii; Joyce anayedaiwa kuwa shareholder ni marehemu kitambo sana. Sasa, endelea kunisoma chini uelewe nini maana yake
View attachment 1010459
Ukisoma hapo juu utabaini kuwa Alice kwa mantiki hii ni sole shareholder ambaye akijua wazi kuwa Joyce hayupo hai (kwa nia ovu naweza kusema) aliamua kutumia jina lake ili atimize azma yake.
Taarifa za kampuni hii ambazo nimezipata ndani ya dakika 25 hivi nilitarajia vyombo vyetu vingeweza kuzipata kwa urahisi na kuepusha aibu mbeleni.
2) Twende kwa huyu ndugu Brian Mutembei
Namfahamu huyu jamaa kwa uzuri tu. Brian ni dalali maarufu na kwa waliokaa katika jiji la Nairobi watakuwa wanamfahamu.
Dalali huyu ni mtu wa karibu na Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto (ambaye wakenya wanamjua kama mmoja wa watu mafisadi wa kutupwa).
Brian ana rekodi ya makosa ya jinai na amewahi kufungwa. Kumbukumbu zake zipo kila sehemu (mtu akijiongeza):
View attachment 1010461
Aidha, dalali huyu anajulikana kwa mbwembwe zake za kumwaga mafedha kuonyesha 'jeuri ya pesa' hivyo siwezi kumtofautisha na kina "Ndama Mutoto ya Ng'ombe" au "Jackie Pemba" hivyo yeye kutumika kwenye hili deal haishangazi.
Simsingizii, soma
hii story (event hii nzi wetu alikuwepo) na utaona maneno haya hapa:
View attachment 1010475
Naishia hapa kwa leo.
UPDATE, Feb 9, 2019
View attachment 1018644