Ulikuwa na hoja ya msingi ya kumjibu Zito ila nadhani hukuelewa au hata kama umeelewa basi umefanya makusudi.
Mtu afe 2001 mwingine azaliwe 2016 tuseme baba yake ni yule aliefariki 2001? Hapo inakuwa haiwezekani lakini kama aliezaliwa 2016 na anatoka familia ya yule aliekufa 2001 hiyo inawekezekana.
La msingi hii biashara isiwe na vidonda ndani yake ila kikubwa korosho zinunuliwe na wakulima wafaidi mavuno yao.
Kampuni hii tukiacha siasa na upofu tulionao katika mazuri na mabaya, inawalakini.
Nimeona inatangaza Alibaba Kama dalali wa Korosho.
Tujenge Tanzania yetu, tushirikiane na tuhoji pamoja haya mambo ili sote tunufaike na juhudi halali za kuwakomboa wakulima