Mzizi wa Mbuyu
JF-Expert Member
- May 15, 2009
- 7,375
- 6,958
Hizo ni habari za kwenye vijiwe tu. Kwa mwaka 1980 kazi ya kuwa katibu mkuu wa UN ilikuwa kubwa kuliko kugombea kuwa rais wa Tanzania. Pia viongozi wengi wa Africa na pia dunia ya tatu walikuwa mbele kumtaka Salim agombee.
Nyerere alifanya juhudi kubwa ili Salim awe katibu mkuu wa UN.
Watu sasa wanatafuta ubaya wa huyu mzee ili wamlaumu; ukweli ni kwamba kwa kiongozi wa miaka ya 60 mpaka early 80, mwalimu alikuwa kiongozi bora sana. tuache kulinganisha na sasa kwenye dunia ya utandawazi. Wakati ule ilikuwa hata ngumu kujua kitu mbali na vile ambavyo wapambe walikuwa wanakuambia.
Ni kweli Nyerere alifanya makosa pia lakini yalikuwa machache ukilinganisha na viongozi wengine wengi.
Asante mkuu, nimekupenda na kukuheshimu sana! Sasa hawa wanaomlaumu mwalimu , wengine wanamtukana matusi kabisa!! eti bwana, wanalengo gani?
Kufanya makosa ni hali ya kibinadamu, hata yeye alikiri hivyo. Walitaka mwalimu afanye zaidi ya nini? yaani basi tu! lakini wanaomtukana mwalimu laana i juu yao!