Who is Salim Ahmed Salim?

Who is Salim Ahmed Salim?

Wakuu wameongea mengi hapo juu ya msingi, kuhusu suala la Palestina Wamarekani walimkaba Salim kwamba atakuwaje Katibu Mkuu wa UN wakati nchi yake iko partial kabisa katika mgogoro wa Palestina, kwamba Tanzania ilikuwa inaunga mkono kwa wazi kabisa PLO na haikuwa hata na uhusiano wa kibalozi na Israel, kwa hiyo hilo kama moja ya migogoro mikubwa kabisa, Marekani iliitumia turufu hii kumkataa Salim kwamba hatakuwa na credibility kwenye hili suala nyeti.

Salim alijaribu sana kujibu hili swali lakini hakuweza kuwa convincing enough, kwani issue ilikuwa wazi.

Wamarekani tu na interests zao. Mbona Marekani ina side na Israel wazi wazi? Wamarekani wao wali taka katibu mkuu atakaye serve interests zao or at least yule ambae asinge ingilie interests zao.

Kama Tanzania ingekua ina side na Israel ungeona jinsi Marekani wange msupport Salim na wala the issue of credibility would have never been a problem for them.
 
CV ya Salim imesheheni!! Anaweza hata akawa Rais wa Marekani acha Tanzania. Ndio maana alikuwa tishio kwao!!!

Bibi Ntilie please...huyu Salim huyu hajui kupanga hoja zake. Huwaga ana ramble sana na ku veer off mada kwa sana. Ukimsikiliza anaongea utaishia kupiga miayo tu ndio ataweza kuwa raisi wa Marekani huyu?
 
CV ya Salim imesheheni!! Anaweza hata akawa Rais wa Marekani acha Tanzania. Ndio maana alikuwa tishio kwao!!!

Hapo pekundu ina tegemea. Politics, socio-politics na priorities etc. za Marekani na Tanzania ni tofauti sana. The kind of leader America needs is not necessarily the kind of leader Tanzania needs.
 
Wayne said:
Katika kuweka kumbukumbu sawa,naamini kipindi cha Dr. Boutrous Ghali ndipo mkataba wa amani wa camp david uliposainiwa na Jenerali Yitzak Rabin akiwa kama Waziri Mkuu wa Israel na Yasser Arafat kama kiongozi wa PLO,tukio la kupeana mikono ya kuashiria amani lilifanyika chini ya Rais William Jefferson Clinton.

I stand to be corrected.

Wayne,

..mkataba wa Camp David ninaouzungumzia mimi ni ule wa mwaka 1978.

..ulikuwa mkataba wa amani kati ya Egypt na Israel. mkataba huo ulitiwa saini na raisi Anwar Sadat wa Egypt na waziri mkuu Manachem Begin wa Israel, chini ya uangalizi wa Raisi Jimmy Carter wa USA.

..Butrous Ghali wakati huo alikuwa minister of state foreign affair wa Egypt. kama sijakosea alikuwa ndiyo chief negotiator wa Egypt.

..sasa Butrous Ghali alikuja kugombea ukatibu mkuu UN miaka ya 90. nadhani kilichowafanya Wamarekani wamuunge mkono ni mchango wake ktk mazungumzo ya Camp David na the fact kwamba he is a Coptic Christian frm Egypt.

.
 
Mikael, siku zote nilikuona u-mstaarabu sana. Kumwita Kikwete Jangala badala ya Jakaya inahusu nini? After all mwenzio ni President of the United Republic of Tanzania whether you like it or not?

hii ni free forum mamaaa.....

so what akiwa president ndio nini....akichanwa si anatoka damu kama mimi...anakula kama mimi [hata kama mimi nakula mlo mmoja]....na mwisho wake ni kama wangu dunia hii...

heshima haiombwi ..bali huja yenyewe....ukiwa baba ..unaheshimiwa kwa ajili ya huduma unayotoa anzia kwa mke....hadi kurudi bega moja juu na kifurushi cha kitoweo cha watoto....kama yote huwezi ndio ..utakuwa baba ..lakini watoto wako watakuita kimoyomoyo BABA OVYOOOO!!...umenisoma nadhani!!!

huwezi kumlinganisha yeyote na huyu sijui naniii huyu...jangala michosho kiwete...eti kwa ajili ..sijui akiongea watu wanalala .....sikujuwa kumbe mwaka 2005 ulichagua mchekeshaji ..sasa kwanini akiitwa jangala uje juu....nadhani ....HATA ZE KOMEDY WANAWEZA URAIS..kwa kuwa wakiongea hata walevi hawalali.......wengine huluita ZE comedy!!
 
Surely, you can never force your children to call you daddy !It is automatic and natural thing, because of what you are doing to them. Even sperm donors they know that those kids from their sperm cell they will never ever call them daddy!
 
Watanzania bwana, naanza kuamini kuwa tuko tofauti na binadamu wengine - how this came about, I must admit I have no idea at all. Tunaweza tukapewa sifa hata ya "non-existent person" tukamkubali kwamba "he is the best" hata bila kujua kama yupo ama hayupo. Tunaweza kuletewa chizi wa kutupwa lakini maadam hatujui histosia yake kwa ndani, lakini kwa kusadikishwa kuwa anafaa, tukamchagua na kumpa dhamana ya kuongoza taifa.

Tumewahi kumpa mtu uongozi eti kwa sababu ya upole wake, mwingine tukampa kwa sababu ya ukimya wake, mwingine kwa sababu ya tabasamu lake !! Na sasa tunadhani Salim angeweza kuwa hata Raisi wa Marekani kwa sababu ya unyenyekevu wake. Pamoja na kuwa ameweza kuwa kiongozi mkuu wa OAU, hakuna legacy yoyote aliyoiacha pale. Jamani katika hii karne kabla ya kumpa mtu uongozi lazima tujiulize kwa lipi.

Kinachofunga mwaka ni kuwa hata pale ambapo tunajua kabisa kuwa hapa hamna lolote bado wateule wakisema anafaa, asilimia 80% watajitokeza kumpigia kura. Simpendi Magufuli, lakini hakuna hata moja anayeweza kusema alishindwa kuthubutu kufanya kitu cha kukumbukwa katika jamii. Sikumpenda kabisa Mrema lakini aliweza angalau kujitutumua pale ambapo viongozi wetu wengi wangejinyamazia kama vile hawapo.

Sasa kuna ulazima wa kujiuliza hivi kuna mdudu gani ndani ya mioyo yetu - tuna tofauti gani na mnyama wa kufugwa ambaye humfuata bwanake kwa utiifu popote pale. Hulka ya ubinadamu inatutaka kuchambua kati ya mema na mabaya, chungu na tamu, kutathmini na kuchagua kukubali ama kukataa. Mpaka sasa tumeweza kuona uwezo wa viongozi tuliowachagua mwaka 2005, je tutawachagua hao hao kwenye uchaguzi ujao ?
Naamini kwa historia yetu hii ni ndoto - ndio ukweli unaouma.
Watu kama Dr. Slaa hawana nafasi katika jamii yetu - ndivyo tulivyo.
 
Una uhakika?

- Yaani sina uhakika kama Salim alikuwa na kundi? Au what?

- Yes, Salim alikuwa na kundi lililoachwa kwenye mataa na Mkapa, kwa sababu originally CCM ilikuwa na makundi makubwa mawili, moja la wateule wa Mwalimu ambalo Salim alikuwa ni member, na lingine la wasiokuwa wateule wa Mwalimu ambalo nalo lilimeguka na kuzaa Asilia na Mtandao wa sasa,

- Hivi ndugu yangu hujagundua mpaka leo kwamba some of ujeuri wa Mtandao ni pamoja na hasira zao dhidi ya siasa na maongozi ya Mwalimu?

Respect.

FMeS!
 
Mikael, siku zote nilikuona u-mstaarabu sana. Kumwita Kikwete Jangala badala ya Jakaya inahusu nini? After all mwenzio ni President of the United Republic of Tanzania whether you like it or not?

- Whaaat? How soon we forget! Yaaani Jangala ni worse kuliko Screw Muungwana? mayiiiiiiweeee! are you serious mkuu?

Respect.

FMEs!
 
Kila mwanasiasa ana kundi haswa hawa ambao wana seek nafasi kubwa ndani ya chama au serikalini.
 
Watanzania bwana, naanza kuamini kuwa tuko tofauti na binadamu wengine - how this came about, I must admit I have no idea at all. Tunaweza tukapewa sifa hata ya "non-existant person" tukamkubali kwamba "he is the best" hata bila kujua kama yupo ama hayupo. Tunaweza kuletewa chizi wa kutupwa lakini maadam hatujui histosia yake kwa ndani, lakini kwa kusadikishwa kuwa anafaa, tukamchagua na kumpa dhamana ya kuongoza taifa.

Na sasa tunadhani Salim angeweza kuwa hata Raisi wa Marekani kwa sababu ya unyenyekevu wake. Pamoja na kuwa ameweza kuwa kiongozi mkuu wa OAU, hakuna legacy yoyote aliyoiacha pale. Jamani katika hii karne kabla ya kumpa mtu uongozi lazima tujiulize kwa lipi.

Naamini kwa historia yetu hii ni ndoto - ndio ukweli unaouma.
Watu kama Dr. Slaa hawana nafasi katika jamii yetu - ndivyo tulivyo.

- Hapo tupo ukurasa mmoja, ingawa mengi huwa hatukubaliani lakini hili tupo wote hapo, hakuna record.

Respect.

FMEs!
 
Nimesoma huu mjadala kiasi fulani nimejifunza vitu vingi; Ila kitu kinachonisikitisha ni tabia ya viongozi wetu kutokushare yale waliyojifunza na wananchi. Mtu kama Salim anatakiwa aandike kitabu kuelezea yale aliyoyafanya na pia aliyokutana nayo. Nadhani itakuwa a fascinating book to read.
 
Watanzania wangapi wana tamaduni ya kusoma vitabu?
 
Rufiji said:
Nimesoma huu mjadala kiasi fulani nimejifunza vitu vingi; Ila kitu kinachonisikitisha ni tabia ya viongozi wetu kutokushare yale waliyojifunza na wananchi. Mtu kama Salim anatakiwa aandike kitabu kuelezea yale aliyoyafanya na pia aliyokutana nayo. Nadhani itakuwa a fascinating book to read.

Rufiji,

..Salim Salim ruled out mpango wa kuandika a memoir, akidai kuna viongozi wengi sana amekutana nao kikazi, na kuna mambo mengi walizungumza naye wakitegemea kwamba hatayaweka hadharani.

..kwa msingi huo basi wanahistoria wanapaswa kuchukua jukumu la kuandika kuhusu ushiriki wa Salim Salim ktk siasa za ndani na nje ya Tanzania.

..tayari kuna vitabu vimeandikwa kuhusu Mwalimu Nyerere na Kawawa. wanahistoria wanapaswa kuandika kuhusu maisha ya Sheikh Abeid Amani Karume, na wa-Tanzania wengine maarufu.

Jasusi,Mwanafalsafa,FMES,....

..je ni kweli kwamba Mkapa alimuomba Salim Salim aje kuwa Makamu wa Raisi baada ya kifo cha Dr.Omari Ali Juma?

..maneno ya mitaani ni kwamba Salim alikataa offer ya Mkapa.

..Dr.Omari alifariki ukiwa umebaki muda mchache sana Salim Salim amalize term yake kama Katibu Mkuu wa OAU.

..kama Salim Salim angechukua nafasi ya Dr.Omar nadhani leo hii tungekuwa tunamzunguzia kama Raisi wa Tanzania.
 
Jokakuu,
Mkuu sii kweli kabisa Salim A. sali asingeweza kupewa nafasi hiyo hata kidogo hasa kuwa rais wa Zanzibar... huyu sii mwana mapinduzi wala hahesabiki ktk baraza la Mapinduzi. rais wa Zanzibar au makamu ni yule tu atayekubalika na baraza la Mapinduzi..

Kisha hata mimi ningependa sana salim aandike kitabu cha maisha yake hata kama hawezi basi atoe ruksa kwa mwandishi mmoja. Watu kama Kawawa, Malecela, Warioba na wengineo wengi wanatakiwa kuwa na vitabu vya maisha yao ktk siasa zetu.

Hii itatupa mwanga zaidi ya kule tulikotoka Kisiasa na wapi tunakwenda..
 
Rufiji,

..Salim Salim ruled out mpango wa kuandika a memoir, akidai kuna viongozi wengi sana amekutana nao kikazi, na kuna mambo mengi walizungumza naye wakitegemea kwamba hatayaweka hadharani.

..kwa msingi huo basi wanahistoria wanapaswa kuchukua jukumu la kuandika kuhusu ushiriki wa Salim Salim ktk siasa za ndani na nje ya Tanzania.

..tayari kuna vitabu vimeandikwa kuhusu Mwalimu Nyerere na Kawawa. wanahistoria wanapaswa kuandika kuhusu maisha ya Sheikh Abeid Amani Karume, na wa-Tanzania wengine maarufu.

Jasusi,Mwanafalsafa,FMES,....

..je ni kweli kwamba Mkapa alimuomba Salim Salim aje kuwa Makamu wa Raisi baada ya kifo cha Dr.Omari Ali Juma?

..maneno ya mitaani ni kwamba Salim alikataa offer ya Mkapa.

..Dr.Omari alifariki ukiwa umebaki muda mchache sana Salim Salim amalize term yake kama Katibu Mkuu wa OAU.

..kama Salim Salim angechukua nafasi ya Dr.Omar nadhani leo hii tungekuwa tunamzunguzia kama Raisi wa Tanzania.

JK-hata mimi hizo tetezi nilizisikia na lengo la Mkapa lilikuwa ni kuja kumuachia nchi lakini Salim akaja kuleta mapozi na ndiyo maana alipojitokeza mwishomwisho Mkapa akamuona hana maana,pamoja na pressure za ccm zanzibar,akaona aweke zengwe tu aondoke.

Ndiyo maana baada ya ule mchuzo hawa wenye madai haya wakasema Salim hana sababu ya kumlaumu Mkapa.
 
Mtarajiwa,
Ni habari ulizozisikia lakini hazina ukweli kabisa.. Salim alitakiwa kusimama kama mgombea wa urais wakati wa Mkapa (chaguo la Nyerere).

Akatolewa nje na baraza la mapinduzi iweje tena ampe kazi sehemu ambayo kura zote zilimkataa Salim..basi huyo Mkapa mwenda wazimu.

Kisha zaidi ya hapo Salim ni mjamaa mtu ambaye Mkapa asingemhitaji kabisa...na ndio maana walimtupa nje kabisa baada ya Nyerere kuondoka..
Jamani kuweni na hoja ambazo zinaleta mjadala...
 
Mtarajiwa,
Ni habari ulizozisikia lakini hazina ukweli kabisa.. Salim alitakiwa kusimama kama mgombea wa urais wakati wa Mkapa (chaguo la Nyerere).. Akatolewa nje na baraza la mapinduzi iweje tena ampe kazi sehemu ambayo kura zote zilimkataa Salim..basi huyo Mkapa mwenda wazimu..
Kisha zaidi ya hapo Salim ni mjamaa mtu ambaye Mkapa asingemhitaji kabisa...na ndio maana walimtupa nje kabisa baada ya Nyerere kuondoka..
Jamani kuweni na hoja ambazo zinaleta mjadala...

Mkandara mkuu unalosema inawezekana ni kweli lakini hatuwezi tukasema 100% kuwa hawa ni waongo kwa sababu hatujui chanzo chao cha habari.Ni maneno ya mtaani na mimi siyaamini 100% isipokuwa nilitaka kuthibitisha maneno ya joka kuwa hata mimi niliwahi kusikia.

Ukisema Salim ni mjamaa,mbona hata Kingunge anajifanya mkomunisti wakati ni mjasiliamali mzuri tu ana makampuni. Inawezekana na Salim angebadilisha muelekeo nae na kwenda kwa soko huria!
 
Last edited:
Mtarajiwa,
Ni habari ulizozisikia lakini hazina ukweli kabisa.. Salim alitakiwa kusimama kama mgombea wa urais wakati wa Mkapa (chaguo la Nyerere).. Akatolewa nje na baraza la mapinduzi iweje tena ampe kazi sehemu ambayo kura zote zilimkataa Salim..basi huyo Mkapa mwenda wazimu..
Kisha zaidi ya hapo Salim ni mjamaa mtu ambaye Mkapa asingemhitaji kabisa...na ndio maana walimtupa nje kabisa baada ya Nyerere kuondoka..
Jamani kuweni na hoja ambazo zinaleta mjadala...

Bob,

Katika Tanzania kila kitu kinawezekana. Kumbuka Gharib Bilal ndo alikuwa mshindi wa kura za maoni za urais kule ZANZIBAR na wala si KARUME. Dodoma wakapindua matokeo. Hawakujali kwamba KARUME anakubalika au la au kwamba CUF ingechukua nchi kwa sababu hiyo.... so swala la SALIM..kama CCM ya Mkapa ingeamua kumpa nafasi wangempa..regardless what these folks in Zanzibar would say.

Salim hakubaliki ZANZIBAR lakini usitegemee kama angesimamishwa na CCM, kwamba angekosa kura..wengi wa viongozi tena wa ZANZIBAR wangemsupport..hata kwa kinyongo au shingo upande.

Ukweli ni kwamba CCM bara kama wakiamua kitu CCM Zanzibar si rahisi kukataa..na Infact hawawezi kukataa..hiyo jeuri hawana..maana hata rais yeyote wa Zanzibar lazima awe na support ya wakulu Dodoma na Dar ES salaama.

Who is willing to risk that..eti aende kinyume na matakwa ya CCM Dodoma? Not these politicians of our era.
 
Wana JF,
Kwa muda nimewaza kuhusu huyu Mtanzania maarufu ndani ya nchi ya Tanzania, na hata kimataifa, ''Dr SALIM AHMED SALIM"

Tangu atoke kuiongoza Afrika (OAU), hatujamtumia vizuri kiuongozi.

Kwani hakuna nafasi muhimu katika Tanzania na hata Afrika masharaiki
ambazo huyu mheshimiwa angeweza bado kutumika?

AU KULIKONI?
 
Back
Top Bottom