Who is Salim Ahmed Salim?

Who is Salim Ahmed Salim?

kaka kwani kampeni zimeshaanza? ok labda utupe nafasi uliyomfikiria kisha utushawishi kwa points za msingi,ni hayo tu mkuu
 
Wana JF,
Kwa muda nimewaza kuhusu huyu Mtanzania maarufu ndani ya nchi ya Tanzania, na hata kimataifa, ''Dr SALIM AHMED SALIM"

Tangu atoke kuiongoza Afrika (OAU), hatujamtumia vizuri kiuongozi.

Kwani hakuna nafasi muhimu katika Tanzania na hata Afrika masharaiki
ambazo huyu mheshimiwa angeweza bado kutumika?

AU KULIKONI?

kitu ambacho nimejifunza humu humu ndani ya JF, ni kwamba wabongo kumbe tuna division especially along the lines of religions sasa ukimpa nafasi mtu kama huyu i'm pretty sure some will moan udini regardless off what he can offer in the country.

aki-ya-mungu, aliejisemea mzungu umaskini a high percentage of poverty is cultural, than anything else. sasa naelewa na JF imenifunza mengi kuhusu mawazo yetu. kuna dada mmoja anaitwa a womenofsub humu ndani ndio kasema ukweli. atupendi ukweli wengi tumesha weka fixed thoughts, mawazo hayo atuendi popote.

KWAHERINI, CIAO, BYEBYE
 
..time to move on,nafikiri wamefanya ya kutosha acha wapumzike na wengine waingie na idea mpya.
 
Jamani tuwe wakweli na tuache kuwashangalia viongozi wa kitz wanapotwaa madaraka ya kimataifa kwa sababu tu ni watz wenzetu bali tuwapime kwa swali hili;WALIISADIA VIPI TZ WALIPOKUWA NA NYADHIFA HIZO KUBWA ZA KIMATAIFA?

Mzee Salim na nafasi kubwa kama zile zlizozishika kimataifa alitusaidia nini sisi watz achilia mbali hata majimbo ya kwao anapotoka maskini sana huko Pemba?Kule Kenya au Nigeria au hata majirani Rwanda , mtu wao akishika nafasi za kimataifa huwa ndiyo kipimo chake cha uzalendo kwa nchi yao!Mambo aliyofanya mama Mangale akiwa msaidizi wa mama Tibaijuka UN kwenye idara ya makazi hakuna asiyejua,ili hali mama Tibaijuka hajaisadia lolote tz kwenye nafasi hiyo,nam ni Kenya wanaopaswa kuingia mitaani kumchangilia mama Mangale na wala sio tz kwa mama Tibaijuka.Au nani asiyejua mambo makubwa aliyoifanyia Nigeria wakati Chief Anyauko alipokuwa kigogo wa Commonwealth

watz walishangilia sana kuteuliwa kwa mama Migiro kuwa naibu katibu mkuu wa UN,na tunajua sana kuwa pale UN kuna loopholes kibao za kupeleka maendeleo kwenu hasa kwenye nyanja za elimu na afya,lkn miaka inapita sasa bila kuonekana dalili zozote za mama huyu kutusaidia hata kwa kisima tu cha maji kule Nkenge kwa miradi ya UN,je bado tusimame kumshangiliA akija Dar kw asababu tu makamu katibu mkuu wa UN?

Tubadilike jamani,mtu akipata nyadhuifa kubwa apimwe tu kwa yale aliyoitendea jamii inayomzunguka, sio kushangilia tu kwa vile yu kapata nyadhifa!

Kama tu quote toka kwa Rais kipenzi wa USA hayati Kenedy alipotuambia mwaka 1961,"Ask not what your country can do for you;ask what you can do for your country"
 
DR. Makyao,
Samahani kama wewe si Daktari lakini jina lako limekaa kiDr. Dr.

Anyway kujibu swali lako kwa nini Salim hajapewa kazi ya maana Bongo, umesahau kampeni zilizoendeshwa na mtandao kwa niaba ya JK kumharibia jina na kumkashifu Salim? Sasa wewe huyu unadhani atakuwa na moyo wa kumpa hata U-Regional Commissioner wa Iringa? Sidhani.

Ninachosikia JK ni mtu wa kisasi na hajasahau jinsi Salim alivyokuwa anam-outshine kwenye medani ya kimataifa. Asingechaguliwa na AU kuwa Rappoteur wa Darfur basi Tanzania angekuwa anasahaulika.
 
Lakini kama serikali inamtunza kumpa fungu lake...anakuwa kama mshauri tu inatosha maana kaama kazi amefanya kubwa sana...apumzike sasa...hata hy ya darfur inamtosha pia keep busy akija Nyerere foundation inamtosha pia...
 
DR. Makyao,
Samahani kama wewe si Daktari lakini jina lako limekaa kiDr. Dr.
Anyway kujibu swali lako kwa nini Salim hajapewa kazi ya maana Bongo, umesahau kampeni zilizoendeshwa na mtandao kwa niaba ya JK kumharibia jina na kumkashifu Salim? Sasa wewe huyu unadhani atakuwa na moyo wa kumpa hata U-Regional Commissioner wa Iringa? Sidhani. Ninachosikia JK ni mtu wa kisasi na hajasahau jinsi Salim alivyokuwa anam-outshine kwenye medani ya kimataifa. Asingechaguliwa na AU kuwa Rappoteur wa Darfur basi Tanzania angekuwa anasahaulika.

JASUSI,
Hayo sikuyajua ndugu yangu.
Ehee!
Kwa hayo mawazo yako, naelewa alichotaka kugusia mwana JF mwenzetu bwana BLURAY.

Kumbe ni athari za hicho kiitwacho mtandao?

Politics can be a very bad game sometimes.
 
Malafyale we vipi!
Upendeleo wa mawaziri mpaka kwa figure za kimataifa?

Jamaa walimfungia vioo asionekane, asingeweza kufanya lolote. Hukusikia sumaye alimsitisha kuchangisha fedha za mfuko wa taasisi ya julius?
 
Wana JF,
Kwa muda nimewaza kuhusu huyu Mtanzania maarufu ndani ya nchi ya Tanzania, na hata kimataifa, ''Dr SALIM AHMED SALIM"

Tangu atoke kuiongoza Afrika (OAU), hatujamtumia vizuri kiuongozi.

Kwani hakuna nafasi muhimu katika Tanzania na hata Afrika masharaiki
ambazo huyu mheshimiwa angeweza bado kutumika?

AU KULIKONI?

Jamani tunahitaji mawazo mapya kwenye medani za siasa nchini kwetu. Kung'ang'ania wazee wa mwaka 47 ndo maana tunadumaa kimaendeleo. Tunahitaji vijana wanaoweza kusoma alama za nyakati na kutuongoza kuelekea kwenye maendeleo ya uhakika. Sio kung'ang'ania wazee ambao sifa pekee ni utiifu kwa chama.

Akina Salim, Kingunge, Mzee John waachwe wapumzike. Tuangalie rika la akina Dk Mwakyembe, Zitto, Anne Kilango, Mnyika na wengine.
 
Ndugu zangu watz,
Napenda kuwaambia watz wengi wanafanya makubwa nje lakini si hapa kwetu. Sijui kwa nini hatujifunzi, nchi nyingi za africa zinawatumia watu wetu, nasi tumekubali kutumika bila kuleta 'return' huku tutokako.

Napenda kuwapa kionjo wa-tz wenzangu, mimi binafsi kuna mtandao mmoja wa unafanya kazi nchi mbalimbali Africa. Nipo ktk mazungumzo nao ili uweze kufanya kazi hapa Africa. Cha kushangaza, ktk mtandao huu, nikakuta mwenyekiti wake ni Mtz lakini yeye hajaweza kushawishi kuwa usaidie Tz.

Siku nikifanikia kuleta huo mtyandao/shirika hapa bungo, nitawaibia strategy. Kwa sasa nisipige kelele sana ndege asije akakurupushwa.

Kwa wenye imani, tuombeane.
 
malafyale we vipi!
Upendeleo wa mawaziri mpaka kwa figure za kimataifa?
Jamaa walimfungia vioo asionekane, asingeweza kufanya lolote. Hukusikia sumaye alimsitisha kuchangisha fedha za mfuko wa taasisi ya julius?

Haya ni makubwa.
Hatukujua siri hizi.
Kama ni kweli, inatisha.
 
Wana JF,
Kwa muda nimewaza kuhusu huyu Mtanzania maarufu ndani ya nchi ya Tanzania, na hata kimataifa, ''Dr SALIM AHMED SALIM"

Tangu atoke kuiongoza Afrika (OAU), hatujamtumia vizuri kiuongozi.

Kwani hakuna nafasi muhimu katika Tanzania na hata Afrika masharaiki
ambazo huyu mheshimiwa angeweza bado kutumika?

AU KULIKONI?

Wako watanzania wengi na wenye uataalam wa kutosha, hawajapewa kazi pia.
Nafasi zimejaa ndugu.
Mpe pole Dk. Salim A Salim
 
..suala siyo serikali au chama kumpa nafasi/kazi Salim Salim.

..nadhani sasa hivi Salim Salim afikirie ku-base nyumbani na kuhamasisha maendeleo. hivi hajachoka tu kukaa nje toka alipoteuliwa Balozi akiwa na miaka 21?

..mzee mwenzake Cleopa Msuya amerudi kijijini Mwanga, na amesaidia kuanzishwa kwa Benki ya wananchi wa Mwanga.

..Salim naye anaweza kurudi Pemba akasaidia masuala kama kupiga vita uvuvi wa kutumia baruti, akasaidia kuanzisha Benki ya wananchi, akahamasisha ujenzi wa shule na vyuo vya ufundi etc etc.
 
Nadhani kwa sasa anapaswa kukaa na kutulia, tunataka mawazo mapya muda huu. Nafasi ambayo anweza kupta lakini si katika serikali hii ya wanamtandao ni kukaa na kushauri.

Hatujasahau yale mazuri aliyoyafanya miaka ya 80

KIJIJI BILA WAZEE......
 
Jamani tuwe wakweli na tuache kuwashangalia viongozi wa kitz wanapotwaa madaraka ya kimataifa kwa sababu tu ni watz wenzetu bali tuwapime kwa swali hili;WALIISADIA VIPI TZ WALIPOKUWA NA NYADHIFA HIZO KUBWA ZA KIMATAIFA?

Mzee Salim na nafasi kubwa kama zile zlizozishika kimataifa alitusaidia nini sisi watz achilia mbali hata majimbo ya kwao anapotoka maskini sana huko Pemba?Kule Kenya au Nigeria au hata majirani Rwanda , mtu wao akishika nafasi za kimataifa huwa ndiyo kipimo chake cha uzalendo kwa nchi yao!Mambo aliyofanya mama Mangale akiwa msaidizi wa mama Tibaijuka UN kwenye idara ya makazi hakuna asiyejua,ili hali mama Tibaijuka hajaisadia lolote tz kwenye nafasi hiyo,nam ni Kenya wanaopaswa kuingia mitaani kumchangilia mama Mangale na wala sio tz kwa mama Tibaijuka.Au nani asiyejua mambo makubwa aliyoifanyia Nigeria wakati Chief Anyauko alipokuwa kigogo wa Commonwealth

watz walishangilia sana kuteuliwa kwa mama Migiro kuwa naibu katibu mkuu wa UN,na tunajua sana kuwa pale UN kuna loopholes kibao za kupeleka maendeleo kwenu hasa kwenye nyanja za elimu na afya,lkn miaka inapita sasa bila kuonekana dalili zozote za mama huyu kutusaidia hata kwa kisima tu cha maji kule Nkenge kwa miradi ya UN,je bado tusimame kumshangiliA akija Dar kw asababu tu makamu katibu mkuu wa UN?

Tubadilike jamani,mtu akipata nyadhuifa kubwa apimwe tu kwa yale aliyoitendea jamii inayomzunguka, sio kushangilia tu kwa vile yu kapata nyadhifa!

Kama tu quote toka kwa Rais kipenzi wa USA hayati Kenedy alipotuambia mwaka 1961,"Ask not what your country can do for you;ask what you can do for your country"

eti aliisaidia vipi TZ kile chombo ambacho kinataka haki, inaonekana mtu kama wewe ukiwa kiongozi TZ utapeleka kila kitu jimboni kwako. yeye alikuwa kiongozi kazi yake ni kuangalia maswala ya africa na sio TZ peke yake.

muulize mama mongella alivyoribu kuleta zake akazania ni TZ ambako unaweza kufanya kitu bila kuulizwa
 
Ndo hivyo tena majuto mjukuu. Huyu bwana alipigwa vita mpaka akaitwa sio mtanzania, what a shame!!Sasa sisi tulio watanzania halisi ngoma inatuchezesha inavyotaka. Mambo yanaenda kwa mwendo wa konokono sijui lini tutafika. Kila kukicha hadithi ni zilezile za kila siku.Uongozi ni kitu muhimu sana.

Tuanze kuchagua watu wenye uwezo wa kuongoza na sio wapiga hadithi siziso kwisha.
 
Back
Top Bottom