Mkuu Gamba,
Heshima mbele, tatizo sio CV za viongozi wetu, isipokuwa tatizo ni CV za sisi wananchi wapiga kura, Salim ana CV nzito lakini tatizo ni kwamba urais hauamuliwi na CV peke yake, kwa bahati mbaya pamoja na CV yake kuwa nzito, alishindwa kwenye uchaguzi wa mgombea wa rais wa CCM,
Sasa kama Muungwana tu alimshinda kule CCM, je atawezaje kupambana na kina Freeman, na Lipumba? Na je akikutana na Dr. Slaa sio ndio itakuwa mauti kabisa kwetu CCM! Pole pole ndugu, urais ni pamoja na kushinda uchaguzi,
Salim ni kweli ana CV nzito, na pia ametuweka kwenye ramani ya Dunia politically, lakini tatizo hakuwa na political base nyumbani, kuanzia visiwani mpaka Bara, sasa uongozi wa kubebwa kama wake ulimalizwa na siasa za vyama vingi!
Otherwise, ni kweli CV yake ni nzito sana!