Issue kubwa ya watu wasiofahamu mpira wanahusianisha Mpira na chenga, ndio Tatizo kubwa la humu jukwaani, na Hata huko mitandaoni kwenye site za changanyikeni,
1. Ronaldo katika peak yake kufunga Goli yard 30 ama 40 ni kitu Cha kawaida, na sizungumzii magoli ya kuchop kipa katoka unamchungulia, nazungumzia shuti la nguvu linalomshinda kipa Golini ambaye Hata hajatoka, mechi nyingi amefanya hivi mfano mzuri ni robo fainali UEFA mechi na Porto.
2. Ronaldo anaruka juu na kunata kwa sekunde, sijawahi ona Mchezaji anayefanya vitu Kama hivi, anaruka juu zaidi kushinda average NBA players, ambao Hawa wa basket Kuruka kwao ni Attribute muhimu.
3. Hana weakness ya kufunga, Kuna magoli ya penalty, magoli nje ya 18, Free kick, Goli la mguu wa kushoto, mguu wa kulia, Goli la kichwa, tiki taka etc kila Aina ya Goli linalofungwa na yeye anafunga, complete Forward.
4. Speed ya Ronaldo, ni Unreal, even at Age of 33, mwaka jana Kombe la Dunia jamaa alikuwa ndio fastest player, tulimuona Katika ujana wake akitanguliza mbele Mpira mshindane ujue kakuacha, na sio mbio akiwa katika hio speed anaweza fanya chochote iwe ni kupiga shuti, kupiga chenga etc.