WHO yaitaka Afrika kujiandaa na usambazaji wa chanjo ya corona

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Shirika la Afya Ulimwenguni-WHO, Alhamisi limezisihi nchi za Afrika kuandaa mipango ya kusambaza chanjo za COVID-19 kadri zitakavyopatikana.

Utafiti mpya wa WHO uligundua kuwa nchi nyingi za Kiafrika haziko tayari kwa kile kitakachokuwa harakati kubwa zaidi ya chanjo barani humo.

Kupanga na kuandaa mikakati kutafanikisha au kuharibu shughuli hii ambayo haijawahi kutokea, na tunahitaji uongozi na ushiriki kutoka ngazi za juu za serikali na mipango thabiti, ya kina ya uratibu wa kitaifa na mifumo iliyowekwa, Dk Matshidiso Moeti, mkurugenzi wa kanda wa WHO wa Afrika, alinukuliwa akisema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Wataalam walionya kwamba wakati maendeleo ya chanjo yanapaswa kusherehekewa, ni hatua ya kwanza tu katika kutolewa kwa mafanikio.

DW
 
Yaani hata kwa mtutu wa bunduki, hachomwi mtu hiyo sindano ya chanjo 😂😂😂😂😂
Kuumwa waumwe wao halafu chanjo tuchomwe sisi? Hakuna panya wa majaribio humu, hata sisi ni binadamu pia 😂😂😂😂😂
Kama wanataka walete chanjo ya Ukimwi 😂😂😂😂
 
Mchangiaji wa kwanza kutoa comment konki yenye ujazo.

Kongole.
 
Kwani, kulikua na makubaliano yaliyofanyika kati ya mtoaji na mpokeaji wa £million 27 kuwa ukipokea mzigo wa pesa lazima uchukue na kuchoma watu chanjo ya covid-19?!
Ndio mimi najiuliza swali hilo hilo, kwamba moja ya masharti ilikuwa ni kuchoma watu chanjo au ni vipi?
 
Shirika la Afya Ulimwenguni-WHO, Alhamisi limezisihi nchi za Afrika kuandaa mipango ya kusambaza chanjo za COVID-19 kadri zitakavyopatikana.

Utafiti mpya wa WHO uligundua kuwa nchi nyingi za Kiafrika haziko tayari kwa kile kitakachokuwa harakati kubwa zaidi ya chanjo barani humo.

Kupanga na kuandaa mikakati kutafanikisha au kuharibu shughuli hii ambayo haijawahi kutokea, na tunahitaji uongozi na ushiriki kutoka ngazi za juu za serikali na mipango thabiti, ya kina ya uratibu wa kitaifa na mifumo iliyowekwa, Dk Matshidiso Moeti, mkurugenzi wa kanda wa WHO wa Afrika, alinukuliwa akisema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Wataalam walionya kwamba wakati maendeleo ya chanjo yanapaswa kusherehekewa, ni hatua ya kwanza tu katika kutolewa kwa mafanikio.

DW
Watu wengi wa ulaya na marekani wanaonekana kugoma kuchomwa hiyo sindano sasa wanataka kushawishi serikali za nchi za Africa kukubaliana nao kuhamasisha hiyo vaccine. Shenzi sana
 
Shirika la Afya Ulimwenguni-WHO, Alhamisi limezisihi nchi za Afrika kuandaa mipango ya kusambaza chanjo za COVID-19 kadri zitakavyopatikana.

Utafiti mpya wa WHO uligundua kuwa nchi nyingi za Kiafrika haziko tayari kwa kile kitakachokuwa harakati kubwa zaidi ya chanjo barani humo.

Kupanga na kuandaa mikakati kutafanikisha au kuharibu shughuli hii ambayo haijawahi kutokea, na tunahitaji uongozi na ushiriki kutoka ngazi za juu za serikali na mipango thabiti, ya kina ya uratibu wa kitaifa na mifumo iliyowekwa, Dk Matshidiso Moeti, mkurugenzi wa kanda wa WHO wa Afrika, alinukuliwa akisema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Wataalam walionya kwamba wakati maendeleo ya chanjo yanapaswa kusherehekewa, ni hatua ya kwanza tu katika kutolewa kwa mafanikio.

DW
WHO walete hela tu Africa tutanunua wenyewe tunapopajua
 
hawa hawa ambao leo wanapinga kupewa chanjo, siku wakiumwa wakitaka chanjo wakiambiwa hamna watakuja kufungua uzi humu kuilaumu sirikali 😀
 
Back
Top Bottom