#COVID19 WHO yasema haina taarifa za COVID-19 kutoka Tanzania

kama unaamini hizo data ndo dawa za Corona.bora niendelee kuwa mjinga milele.
Ndiyo maana tunasema wewe ni mjinga usiye na hamu ya kuelimika. Tamaa yako ni kuwa mjinga wa kudumu. Mpumbavu = mjinga wa kudumu.
 
Kwani WHO ikipata taarifa za takwimu za COVID-19 kutoka tz wanasaidiaje? Mbona vifo vimezidi hata huko nchi za ng'ambo?
Kweli we ni.... Halafu unaweza kukuta ni kiongozi mkubwa na unataka uraisi. Hayo ni majibu gani?

Kwa hiyo wewe unaakili kuliko waliofikiria na kuunda chombo hicho. Hili ni tatizo la elimu na kuwa na PHD za badindia bila kusoma.

Watu wanafikiria afya za wenzao wewe unafikiria siasa. Mbona hukutani na barakoa yenye mzigo mkapambana?
 
Mwanachama
Kwa hiyo ulipouliza ulikuwa hujui masharti ya chama chochote ni pamoja na mwanachama kutoa taarifa zake zinazohusiana na shughuli za chama? WHO wangekuwa wameuliza habari za kwa nini Tanzania imetolewa mapema CHAN tungewashangaa, lakini unapohoji kwa nini WHO wanataka takwimu za Tanzania kuhusu Covid19 tunakushangaa wewe.
 
Kwani ni Sheria?.
Mbona hawataki takwimu za magonjwa mengine?
Kwanini Corona?
 
Kwani ni Sheria?.
Mbona hawataki takwimu za magonjwa mengine?
Kwanini Corona?
Kumbe hujui unachokiongea!!!! Malaria haitolewi takwimu? TB haitolewi takwimu? Kansa haitolewi takwimu? Ukoma hauna takwimu? Au unadhani Wizara ya Afya inapokusanya takwimu toka vijijini zinaishia Dodoma?
Kwa comment hii nakupa "Ignore" kuanzia sasa usinisemeshe.
 
Ngoja Acha kukimbia.na hizo takwimu za hayo magonjwa zinatolewa kila SIKU?
 
Namba inazidi kupanda Tu.
Hao WHO BURE KABISAView attachment 1707976
Je,idadi ya watanzania waliopoteza maisha kwa korona unaijua? Unaweza kukuta ni idadi kubwa kuliko hata hao unaowakejeli kwa kuwa hapa hakuna data!

To be honest,hiyo idadi ya wakenya waliofariki kwa korona ni ndogo sana ukilinganisha na watanzania waliokufa kwa ugonjwa huo. Naamini na wewe unajua hilo...ila kwa sababu unazozijua wewe,umeamua kuungana na wapotoshaji wengine ili watanzania waendelee kupoteza maisha kutokana na serikali kutoongoza mapambano ya janga hili.

Hebu acheni kuidhihirishia dunia ujinga wa mtu mweusi.
 
Sisi hapa ventilators,hakuna za kutosha,na wakati kwingine hata okisijeni inaadimika!
 
Kwani watu wakifa na Corona kuna ubaya gani?.
 
basi endelea kuamini unachoamini na Mimi niendelee kuamini NINACHOAMINI.kuna tatizo?
Tatizo lipo kwa kuwa unachoamini unawapotosha watanzania wengine hivyo wanashindwa kuchukua hatua sahihi za kujilinda na kuwalinda wengine dhidi ya maabukizi ya korona kwa kutumia maelekezo ya wataalamu wa afya.
 
Sasa kama unanisikiliza Mimi basi utapotea
Maana Mimi Imani yangu Corona ni ugonjwa wa PROMOTION nyingi.siamini kama Corona inaua.
Tatizo lipo kwa kuwa unachoamini unawapotosha watanzania wengine hivyo wanashindwa kuchukua hatua sahihi za kujilinda na kuwalinda wengine dhidi ya maabukizi ya korona kwa kutumia maelekezo ya wataalamu wa afya.
 
Sisi hapa ventilators,hakuna za kutosha,na wakati kwingine hata okisijeni inaadimika!
Hizo ni sehemu ya hatua ambazo serikali ilipaswa iwe imeshazichukua kuhakikisha wagonjwa wa Corona wanapata huduma stahiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…