Whozu ananunua gari baada ya kulipwa Tigo Fiesta..

Whozu ananunua gari baada ya kulipwa Tigo Fiesta..

Be positive, hata haya hakuulizwa kaandika mwenyewe bila kuulizwa siku akijisikia kusema analipwa shilingi ngapi pia atasema bila kuulizwa.
Kwani Mark X hiyo bei gani haizidi hata mls 16, Sasa kwa Shows 13 hata angekuwa analipwa mils 1.5 bado angeinunua tu.
Angeandika kuwa kadhulumiwa huenda usingesema aweke mkataba uone unasemaje, ungewashambulia moja kwa moja anaodai wamemdhulumu.
Fiesta malipo yake haifiki milioni 1 labda amepiga show zingine huko na mapato ya YouTube
 
Huu uzi ushakuwa wa chai baridi kuna boya atapata sifa hapa kwa chai zake za stand
 
Dogo umepaniki sana,Mtu mwenye "MAPAGALE" matatu hawezi kupaniki kwa niliyoyaongea,inaonekana nimegonga mule mule ndio maana imekuuma,unashangaa kiwanja mil 50? Watu wananunua hadi mil 800.......Endelea kununua SKWATA zako huku JF,humu JF kila mtu ana nyumba na wewe unaendeleza UPOPOMPO wako wa kuwa na MAPAGALE matatu 😀😀😀😀😀.
Hahaha humu Jf Kuna vituko sana. Haya dogo kula kulala.
 
Fiesta malipo yake haifiki milioni 1 labda amepiga show zingine huko na mapato ya YouTube
Hakuna mwenywe uhakika wa Malipo ya Fiesta wanaojua ni wasanii na Clouds yenyewe. Ila mwenyewe kasema ni kutokana na show alizofanya Fiesta, sasa mimi ni nani nipingane naye?
 
Kwahyo kumiliki gari umeona ni kitu muhmu kuliko kujenga nyumba labda?

Mbna hakupostiwa kuwa kamiliki nyumba mmekimbilia gari.

Kumtangaza mtu kumiliki nyumba ni zaidi ya mara mia ya gari.

Muache upopoma.

Na sijaona mantiki ya mtu kumiliki gari huku umepanga halafu unategemea show za fiesta ndyo ununue gari na upost.

Sent from my TECNO-Y3+ using JamiiForums mobile app
Mkuu sasa kosa ni kutegemea kazi yake kumiliki gari? Mziki ndo kazi yake na kama ndiyo kazi ianyomwezesha kununua gari mbona safi tu.
Halafu kuna watu kwa nature ya kazi wanazofanya na vipaumbele gari inabidi iwe kipaumbele cha kwanza then ndo nyumba. Maisha siyo kuigana maisha ni mipango siyo lazima kila mtu afuate formula ya mwenzake ndugu. Huenda hilo gari likampa michongo zaidi ya kushusha mjengo bila stress.
 
aisee naona mi si mzalenda wa nyimbo za kwetu maana hata sijawahi kumsikia huyu jamaa
 
Lakini cha ajabu akishazidi kupata mafanikio kuna siku atakuja kusema huwa anadhulimiwa
 
Wabongo bana ni sawa na mjasiliamali aliyefanikiwa baada ya kuuza unga kwa kusaga mahindi kwa kutumia jiwe kisha akanunua mashine ya umeme mtu anajitokeza anaponda eti kwanini asingejenga ghala.

Piga kazi Whozu wabongo tumeumbiwa fitna.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kafanya shows zote, ana nyimbo mbili, hit ni moja tu, yeye ndiye aliyewashukuru waandaaji wa fiesta kwa kupata pesa ya kununulia hilo gari, Malipo ya show ni privacy yake tutajua kama yeye akiamua tujue. Ila cha msingi ni kama ndoto yake ilikuwa ni kumiliki chombo basi kafanikisha.
1. Follow
2. Gonga
3. Tunavesha
4. Huendi mbinguni
5. Usiombe

So far hizo ndo nyimbo zake hadi sasa, mimi namkubali sana hasa yale machepele yake.
 
Sasa wewe, umeona wapi mwanaume anasifiwa au kupostiwa kisa kanunua gari?

Shusha mjengo post ntamusaidia kushare,,

Halafu siyo kila michongo yake lazma utumie gari binafsi mbna bajaj zpo tena sana,

Unamiliki gari hata kununua mafuta unashndwa[emoji3]

#bado_sijanunua_gari_mjini_kuna_jam!

Back
Top Bottom