Why Facebook Co-Founder Mark Zuckerberg is an Atheist?


Badala ya kutoa jibu la jumla namna hiyo.
Kama Una ukweli na unajua uandikacho ungemhoji hoja kwa hoja na kuonyesha hayo uyaonayo ni mapungufu kihoja.
Wewe rejea majibu yake sambaratisha hoja kwa hoja...
Haya twende kazi...
 

""Kwa hiyo amewapa uhuru sio, hawako chini ya sheria?""
 
Kwa hiyo amewapa uhuru sio, hawako chini ya sheria?

Ukichagua kuwa chini ya Sheria ya Mumgu huwezi kulawiti watoto...
Lakini unao Uhuru wa kuifuata sheria au kuiharifu. Vigezo na masharti kuzingatiwa...
 
Nani aliambiwa hilo agizo, unasoma biblia Kama kasuku.
Petro ndiye aliambiwa lolote atalolifunga duniani litafungwa hata mbinguni. Sasa nionyeshe wapi Petro alibariki mabwabwa muhudumu katika kutaniko la wakristo (kanisa)...

Wewe unachokifuata sasa si mnadai ni miongozo ya kale? Wewe ulikuwepo hapo kale? Si walipewa wengine hayo maagizo? Inakuwaje yanakuhusu wewe leo hii? Hayo aliyoambiwa petro hayahusiki kivipi?
 
Acha hoja za kitoto, unazungumzia Ukimwi @ family level ?

Sasa mkuu mpona unakuwa provoked kirahisi hivyo? Wewe humu umekuwa ukitumia maneno kama bwabwa, niliposema ni lugha za kitoto ukasema lugha anayotumia mtu si hoja, sasa wewe uliposema ukimwi ni kitu chema na mimi kukwambia familia yako ikiupata utafurahi unasema ni utoto.
Unachosahau ni kuwa mungu wenu ni wa upendo na amewaamrisha kumpenda jirani yako kama unavyojipenda, kwa hiyo pato la mzalishaji wa ARVs kuongezeka kupitia maambukizi ya wanafamilia wako ni jambo linalopaswa kukufurahisha wewe unaefuata amri za mungu wako.
Nadhani mpaka hapo umemuona mtoto ni nani?
 
Ukichagua kuwa chini ya Sheria ya Mumgu huwezi kulawiti watoto...
Lakini unao Uhuru wa kuifuata sheria au kuiharifu. Vigezo na masharti kuzingatiwa...

Kwa hiyo mapadri walio mashoga wako chini ya sheria ipi? Wao ndio waalimu na viongozi wa makanisa yao
 
Kwa hiyo mapadri walio mashoga wako chini ya sheria ipi? Wao ndio waalimu na viongozi wa makanisa yao

Muongozo wa MTU aitwaye Mkristo ni Yesu Kristo. Hivyo Kama unahoja yoyote dhidi ya Wakristo iwe ni kutokana na msingi wa maandiko ya Kikristo na sio kurejea social behavior. Za makundi yajiitayo ya Kikristo huku matendo yao yakikinzana na msimamo wa Yesu Kristo..
Sio mashoga pekee yao hata wezi na watendao kinyume na sheria ya Mungu wote wanatumia Uhuru wao wa kuchagua ubaya dhidi ya wema...
 

Kama ushoga si mihimu katika kujadili swala la imani yako, mbona ni wewe ulielianzisha hilo, mbona unajipinga? Au lina umuhimu pale wewe unapoamua kulileta na unaisha pale unapoamua?
 
Kama ushoga si mihimu katika kujadili swala la imani yako, mbona ni wewe ulielianzisha hilo, mbona unajipinga? Au lina umuhimu pale wewe unapoamua kulileta na unaisha pale unapoamua?

Wapi nimehusisha ushoga na umuhimu wake kwa imani yangu ?
Imani yangu swala la ushoga ni ukengeufu ya kimaadili ya kibinadam...
Huwezi kuwa shoga na ukawa Mkristo wakati huo huo ! Ama uamue kuwa shoga ujitenge na Kristo au uwe wa Kristo ukijitoa katika mambo ya kishoga.
Ni katika watu wanaoamini uwepo wa Mungu ndiko kuna maadili na ushoga ni kinyume na maadili nje ya Mungu kila kitu ni sawa hakuna kitu inaitwa maadili.
 

Unapoamua kuzungumzia atheism kwa mtazamo wa ushoga, ni jambo ambalo lina mjadala mpana unaojumuisha pamoja na imani yako ya mungu. Tukiishia tu kuujadili kwa upande mmoja tunakuwa hatuutendei haki kwa sababu umo katika makundi na ngazi zote za kijamii. Kwa hiyo ulipoliingiza katika mjadala , ulipaswa kulitambua hilo.
Si kweli kuwa kuamini katika mungu ndio msingi pekee wa maadili kwa sababu kuna wengi tu wanaofanya mambo ambayo ni kinyume na maadili ya kijamii huku wakiwa ni waumini wa mungu. Mfano mzuri kuna wauaji, wezi, wabakaji, walawiti wa watoto, wanaonajisi watoto, ambao imani yao katika mungu ni kubwa tu.
 

Sielewi tatizo lako liko wapi ! Maadili ni kwa Mungu pekee nje ya Mungu maadili unayapata wapi ? He ? Kwenye sayansi kuna kitu kinaitwa maadili (morals) kuzungumzia human behavior sioni ni kwa namna gani kunaondoa maadili kwa Mungu.
Kuna kitu umeambiwa kuhusu Free Will hivyo wanaochagua uovu badala ya wema wanawajibika kwa uovu wao sawa na waliochagua wema pia wanawajibika kwa wema wao.
Ni kwa namna gani waweza kujadili morals kwa mtazamo wa Atheist ?
 

Maadili ni nini? Mtu mwenye maadili anakuwaje?
 
Mabaya ya ulimwengu ni yapi ?
Ni mabaya kwa kipimo gani ?
Umindless wako usitumie Kama ndicho kitu cha kutambua mabaya, eleza namna MTU Mwenye mind anaweza tambua hayo uyaitayo mabaya....
Acha kurukaruka toa majibu Kama huwezi bonyeza ignore list

Mabaya ya umwengu ni yale yanayowafikia watu bila wao kupenda wala kuweza kuepuka.

Magongwa, matetemeko, tsunami, etc.
 
Maadili ni nini? Mtu mwenye maadili anakuwaje?
Maadili ni jumla ya mambo ambayo Mungu ameyaandika kwenye fikra za binadamu wote kwamba ni mabaya...
Na ameyaweka bayana kwenye maandiko ya vitabu vyake ambayo hata binadamu asiyewahi kusoma ama kujifunza kuhusu maadili anatenda vile sawa na aliyejifunza.

Kubaka ni kubaya kwa muujibu wa maadili ya Mungu.
Kulawiti ni kubaya katika mazingira yoyote Yale...

Kuua ni kubaya kwa mujibu wa maadili...
Nk nk nk ...

Mwenye maadili ni yule sio Tu kwamba hatendi yaliyokinyume na maadili Bali hukemea na kufundisha kuhusu maadili mema.
 
Haya mambo kuna kipindi yafikie tamati kwa kukubali kutokubaliana...

Nyie mnaomtetea Mungu mnamdhalilisha, na tatizo mnatetea huku mnatukana, maneno kama Bwabwa, si maneno mazuri, pia kuna mwingine kasema UKIMWI ni jambo zuri as longer as ARV's zinauzwa, ufikiri wa namna hii ni mbaya sana....

Hapa kuna mambo mawili katika kuelewa uwepo wa kitu, eidha kujua ama kuamini,....

Katika kuamini mara nyingi hakuhitaji uthibitisho wa nje, yaani kuthibitisha na mtu mwingine aone, Katika kuamini, uthibitisho ni self evident, mambo niliyotendewa au kuexperience within my self.....nikishasema naamini ( Doxa) ukiniomba proof ntakushangaa....

Kuamini uwepo wa kitu, kuna maana mbili, hicho unachoamini kinaweza kuwepo au kutowepo....

Kujua kunahitaji Uthibitisho, kujua kunaenda mbali zaidi, kwa maana unaweza kuelezea, kujaribu, kuona, kugusa, nikiomba unielezee kwa nini ndege inapaa, unaeleza kwa maana unajua, sio kuamini!

*************************

NB:, Uwepo wa Simba mwenye Kichwa kinafanana na cha binadamu Hifadhi ya wanyama Saadani au Ruaha, kwa wewe au yeyote kutomuona haimaanishi huyo Simba hayupo.....

Simba anaendelea kuwepo tu!......

Anayeamini aamini, anayejua alete uthibitisho....
 
Mabaya ya umwengu ni yale yanayowafikia watu bila wao kupenda wala kuweza kuepuka.

Magongwa, matetemeko, tsunami, etc.

Magonjwa huwafika watu bila kupenda ?
Matetemeko pia huwafika watu bila kupenda ?
Tsunami huwafikaje watu pasipo kupenda ?
Jaribu kueleza kwa namna ambayo MTU anayefikiri magonjwa ni mazuri kwa pharmaceutical industry aelewe. Sio unalundika tuu.

Maana Kama unakula pasipo hekima, hufanyi kazi, unaugua kisukari kwa Atheist wewe hilo ni kosa la mungu.
Wakati Mungu aliwapa watu wake utashi wa kimaarifa kujua siri zake na kujua mienendo myema ambayo ni muhimu kwa afya na mibaya ambayo ni mibaya kwa afya.
Ni muhimu binadam aliyeumbwa na Mungu na kupewa hekima ajue ni kwa mazingira gani hatakiwi kuishi kwenye ukanda wa matetemeko au Tsunami.
Mungu hakuumba binadamu wawe Kama misukule aliwaumba na hekima waitumie kutambua hekima na maarifa juu ya siri za uumbaji wa Mungu.
Hivyo kuita kuna jambo baya ulimwenguni ni upungufu wa hekima na kutojitambua kwa nini uliumbwa.
 

Maandiko yapi aliyoyatoa Mungu? Waislam wana maandiko tofauti na wakristo na yanakinzana kwa kiasi kikubwa na maandiko ya wakristo m.f kuna waislam wenye msimamo mkali wanaoamini kuwa kuchinja watoto bila hatia, kuua wazazi watu wasio na imani kama yao na kujilipua ni jambo jema, sasa hayo pia utaita ni maadili?
Katika taaluma mbalimbali, kuna miongozo na kanuni zinazofuatwa na walio katika taaluma hizo, mungu wenu ameionyesha wapi hiyo misingi na miongozo ya kimaadili katika taaluma hizo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…