Ishmael nimemhoji akadai ameleta majibu. Lakini majibu yake huwa haysonyeshi uhusiano na kile nachohoji labda uwe mtu ambae una mtazamo kama wenu.
Anadai mungu ndie chanzo cha vitu vyote, ukihoji ni ushahidi gani unaoonyesha hilo anaanza kujikanyaga na kutumia lugha ambazo binafsi sioni kama zina mantiki. Akielemewa anaanza kucopy maandishi ya watu, nayo hayana ufafanuzi juu ya uhusiano wake na uwepo wa mungu lakini bado anakuwa na ubishi usio na msingi, ni jambo lisilojenga.
Jenga hoja, na mimi nilete hoja, kutumia lugha za mtaani ni jambo ambalo kila mtu analiweza lakini faida yake iko wapi kama si kujionyesha ulivyo na mapungufu?
Sasa hebu nipatie majibu.
Badala ya kutoa jibu la jumla namna hiyo.
Kama Una ukweli na unajua uandikacho ungemhoji hoja kwa hoja na kuonyesha hayo uyaonayo ni mapungufu kihoja.
Wewe rejea majibu yake sambaratisha hoja kwa hoja...
Haya twende kazi...