Yeah! Ila angerudisha ela yangu mipia nime ipatia maumivu..Ukiwa na upungufu wa pesa utaona unaonewa kwenye kila jambo bila kujua alipata maumivu gani akaamua kulipa peke yake. Huhitaji huruma maisha ndivo yalivo, hata kama ulihitaji wi-fi kufanya jambo muhimu kiasi gani lazima ujue kuna garama. Mkuu jikubali ishi level zako
Wewe una shida mahali. Nakushauri tafuta nyumba ingine.Ishu ni ya fiber ila plane B yangu kwa sasa Next month nalipia alafu nakuja kuiamisha geto kwangu akizingua naifungia mana namba nilisajilia mm
Nilichogundua vitu vya kuchanga ni vigumu lazima mmoja aww ndy mkuu wengine muwe wafuasi,Habari wanaJF,
Naomba ushauri wenu kuhusu jambo lililonitokea mimi na mwenye nyumba wangu, maana mpaka sasa sijui kama mimi ndiye mwenye makosa au kuna sehemu mwenye nyumba hakunitendea sawa.
Mwanzo kabisa, mwenye nyumba ndiye aliyetuletea wazo la kununua Wi-Fi ya pamoja. Tukakubaliana wapangaji na mwenye nyumba tuchangie fedha, tukainunua hiyo Wi-Fi. Kwa kuwa ile Wi-Fi ilikuwa ya kufungwa sehemu moja, tukaona ni bora ifungwe sebuleni kwa mwenye nyumba kwa sababu nyumba yake ni kubwa, lakini signal ilikuwa inafika mpaka chumbani kwangu na nilikuwa naitumia.
Makubaliano yetu yalikuwa kwamba tumechangia kununua hiyo Wi-Fi pamoja, na kila mwezi tungeendelea kuchangia gharama za kuilipia. Pia tulitegemea wapangaji wengine nao wachangie ili mzigo usiwe kwa watu wawili tu.
Baada ya muda, wapangaji wengine wakaanza kushindwa kuchangia na wengine hawakuwa wanajibu kabisa kuhusu suala la malipo. Mwisho wa siku, ikawa mimi na mwenye nyumba ndio tunabeba zaidi gharama za Wi-Fi.
Kisha mambo yakawa magumu kwangu kiuchumi kwa muda. Kuna kipindi nilikuwa nimeyumba kidogo kutokana na mambo ya kazi na changamoto nyingine za kifamilia, hivyo nikashindwa kuchangia kwa wakati kama kawaida.
Mwenye nyumba akaamua kulipia mwenyewe huo mwezi. Baada ya kulipa, akaniondoa kwenye Wi-Fi na akabadilisha password, hivyo mimi nikawa sina tena access.
Kitu kilichoniumiza zaidi ni kwamba Wi-Fi yenyewe tulinunua kwa kuchangia wote, mimi nilitoa hela yangu wakati tunainunua. Lakini baada ya mimi kushindwa kuchangia kwa mwezi mmoja kutokana na hali yangu ya kifedha, nikakatwa kabisa.
Wakati huo mwenye nyumba mwenyewe alikuwa bado anatumia Wi-Fi hiyo bila tatizo.
Mimi nikawa sina internet, mpaka nikawa nalazimika kutoka nyumbani na kwenda sehemu nyingine jirani, kama umbali wa karibu kilomita moja, ili nikalipe na kutumia Wi-Fi kwa ajili ya mambo yangu.
Baadaye nilijaribu kuongea naye kuhusu hili na kumuomba kama kuna uwezekano aniruhusu kutumia Wi-Fi hiyo angalau kwa muda wakati nikipanga mambo yangu ya kifedha. Kuna siku hata nilikuwa na Tsh 1000 nataka kuelekea kwenye wifi ya kuchangia buku ikabidi nijaribu kumwambia kwa sababu alikuwa naye anaelekea maeneo ya huko nikamwambia hapa kuna buku hapa vipi napata internet akachukua nikarudi kitaani kuperuzi...
Sasa swali langu kwa wanaJF ni hili:
Je, mwenye nyumba alikuwa sahihi kuniondoa kabisa kwenye Wi-Fi kwa sababu nilishindwa kuchangia malipo ya mwezi mmoja, wakati mimi nilikuwa miongoni mwa watu waliochangia fedha za kuinunua hiyo Wi-Fi mwanzo?
Faza Hausi nae mnoko! unataka kutumia huduma usiyoilipia?, Kiungwana tu angekurudishia hiyo pesa yako uliyochangia mununuzi ya Wi-fi ili iwe mali yake mazimaHabari wanaJF,
Naomba ushauri wenu kuhusu jambo lililonitokea mimi na mwenye nyumba wangu, maana mpaka sasa sijui kama mimi ndiye mwenye makosa au kuna sehemu mwenye nyumba hakunitendea sawa.
Mwanzo kabisa, mwenye nyumba ndiye aliyetuletea wazo la kununua Wi-Fi ya pamoja. Tukakubaliana wapangaji na mwenye nyumba tuchangie fedha, tukainunua hiyo Wi-Fi. Kwa kuwa ile Wi-Fi ilikuwa ya kufungwa sehemu moja, tukaona ni bora ifungwe sebuleni kwa mwenye nyumba kwa sababu nyumba yake ni kubwa, lakini signal ilikuwa inafika mpaka chumbani kwangu na nilikuwa naitumia.
a geangr
Makubaliano yetu yalikuwa kwamba tumechangia kununua hiyo Wi-Fi pamoja, na kila mwezi tungeendelea kuchangia gharama za kuilipia. Pia tulitegemea wapangaji wengine nao wachangie ili mzigo usiwe kwa watu wawili tu.
Baada ya muda, wapangaji wengine wakaanza kushindwa kuchangia na wengine hawakuwa wanajibu kabisa kuhusu suala la malipo. Mwisho wa siku, ikawa mimi na mwenye nyumba ndio tunabeba zaidi gharama za Wi-Fi.
Kisha mambo yakawa magumu kwangu kiuchumi kwa muda. Kuna kipindi nilikuwa nimeyumba kidogo kutokana na mambo ya kazi na changamoto nyingine za kifamilia, hivyo nikashindwa kuchangia kwa wakati kama kawaida.
Mwenye nyumba akaamua kulipia mwenyewe huo mwezi. Baada ya kulipa, akaniondoa kwenye Wi-Fi na akabadilisha password, hivyo mimi nikawa sina tena access.
Kitu kilichoniumiza zaidi ni kwamba Wi-Fi yenyewe tulinunua kwa kuchangia wote, mimi nilitoa hela yangu wakati tunainunua. Lakini baada ya mimi kushindwa kuchangia kwa mwezi mmoja kutokana na hali yangu ya kifedha, nikakatwa kabisa.
Wakati huo mwenye nyumba mwenyewe alikuwa bado anatumia Wi-Fi hiyo bila tatizo.
Mimi nikawa sina internet, mpaka nikawa nalazimika kutoka nyumbani na kwenda sehemu nyingine jirani, kama umbali wa karibu kilomita moja, ili nikalipe na kutumia Wi-Fi kwa ajili ya mambo yangu.
Baadaye nilijaribu kuongea naye kuhusu hili na kumuomba kama kuna uwezekano aniruhusu kutumia Wi-Fi hiyo angalau kwa muda wakati nikipanga mambo yangu ya kifedha. Kuna siku hata nilikuwa na Tsh 1000 nataka kuelekea kwenye wifi ya kuchangia buku ikabidi nijaribu kumwambia kwa sababu alikuwa naye anaelekea maeneo ya huko nikamwambia hapa kuna buku hapa vipi napata internet akachukua nikarudi kitaani kuperuzi...
Sasa swali langu kwa wanaJF ni hili:
Je, mwenye nyumba alikuwa sahihi kuniondoa kabisa kwenye Wi-Fi kwa sababu nilishindwa kuchangia malipo ya mwezi mmoja, wakati mimi nilikuwa miongoni mwa watu waliochangia fedha za kuinunua hiyo Wi-Fi mwanzo?
Maji tu.WIFI ya kuchanga ni migogoro tu, nakushauri pambana uchukue yako ,mtaendelea kugombana tu mwisho akupe notice ,maana sio siku zote utakua una hela ya kuchangia,
mpangaji mwisho wa mwezi unachanga 1.umeme,2,
Hii comment ina ashiria kua,wewe jamaa una nongwa sana,halafu una roho ngumu na mbaya sana,Yeah! Ila angerudisha ela yangu mipia nime ipatia maumivu..
Hurudishiwi kitu. Heshimu makubaliano yenu kuhusu malipo.Bora ange nambia au angenirudisha hela yangu
Sahihi mkuuNDIO, Mwenye nyumba yupo sahihi.
Lipia kifurushi kisha uendelee kutumia data, kama mlikubaliana hivyo basi inakupasa ufuate makubaliano.
Mwanaume usipende kutia huruma kwenye haya Maisha, huwezi kutoboa.
Be a Man, jifunze kujitegemea.
maji,umeme,king'amuzi,ulinzi shirikishi,takataka .hivi vyote vinalipwa mwisho wa mwezi, sasa kama WIFI tu inamshinda ,Maji tu.