Wife aliniamsha usiku wa manane ni mfuatie embe bichi kisa ana mimba

Kuna jamaa nae aliagizwa tango saa 7 usiku, bahati nzuri akapata kwa wauza chips Maeneo ya kona bar, kufika nyumbani akaambiwa ale yeye ili wife asikie Sauti ya tango likitafunwa
Mkuu wengi watazani unachekesha Kwa vile Mimi kilinikuta Wala siwezi bishi. Maana kale kaembe kachanga mtuwenye akili timamu hawezi akala kwanza atakatupa huko.
 
Daah ni mateso
 
Ushauri wa bure: kwakuwa umegundua hilo jaribu kuyatafuta maembe ujaze ndoo kubwa uyaweke chumbani akijisikia kula usiku anamka anajichukulia mwenyewe...wasiwasi wangu akibadilisha akadai machenza hapo kimbembe tena.
Hii ni kipindi Cha nyuma mkuu Kwa first born wetu. Kwa Sasa hawezi maana nilimwambia asijaribu tena
 
Mkuu kale kaembe ukikaona hata kukatamani huwezi lkn kalirudisha furaha yake chap mno. Nilishangaa Sana.
Kiukweli wanawake wenye mimba kuna muda wanakera,mi wa kwangu aliniagiza samaki mda huo nna 6000/= mfukoni nikanunua samaki ya buku 5,mwanaume nikabaki na buku

Nilivyomfikisha yule samaki wife akasema hamu ya samaki imeisha dah
 
Kiukweli wanawake wenye mimba kuna muda wanakera,mi wa kwangu aliniagiza samaki mda huo nna 6000/= mfukoni nikanunua samaki ya buku 5,mwanaume nikabaki na buku

Nilivyomfikisha yule samaki wife akasema hamu ya samaki imeisha dah
Halafu hii ni kama wote anaweza kukwambia anahamu na kitu flani ukileta anabadiri gia anakwambia hamu imekata.au akununie tu.



Kuna mimba Tena ya mtoto wa3 nguo zake alikuwa havai ni nguo zangu tu mashat ya mikono mirefu ama mifupi nikajiuliza Nini hiki?

Ukienda chooni usiku unafatwa unakata gogo anakuongelesha asee mkuu ni mengi sana yakusema
 
Mimba bana inajua kupelekesha..😌

Hamna lolote ni makusudi tu.
Ni sababu ya mapokeo.
Yani alisikia na kuona wanawake wengine wakifanya hivyo Basi amejiwekea hivyo kwenye akili yake lakini sio sahihi.
Kutesa tu wanaume wa Watu jamani ! 🤔🤔🤔
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…