Wife aliniamsha usiku wa manane ni mfuatie embe bichi kisa ana mimba

Wife aliniamsha usiku wa manane ni mfuatie embe bichi kisa ana mimba

Yani kuna mwanamke akishika mimba ndani ya nyumba wote mume na other family members wote mko kwenye shida.
Wote kama mko na hiyo mimba 👌👌👌
Mke atadeka huyo hadi kuchosha.
Nongwa na yeye kama zote .
Kujifanya kuchagua vyakula.
Jamani mimba sio ugonjwa.
Ujauzito ni baraka.

Kwanini unawaelemea wenzio kwa nongwa żako mama ?! 🤔🤔
 
Wengine hadi aje kujifungua familia nzima kama imejitua gunia la mawe mabegani.

Mwanaume usiwajulia wanawake wa aina hiyo utakosa utulivu wa nafsi.
Hata ukilala utakuwa kimagutugutu tu kila siku
Utapelekeshwa wewe ukome.
Mara ajifanye anaumwa kumbe mzima wa afya .
 
Wanawake Wana mbinu nyingi sana za kukutesa. Akiwa na mimba tumelala vizuri kabisa bila changamoto yoyote Ile.

Nashituka kutoka usingizini nashangaa kuona mwenzangu analia bila sababu.

Nauliza unaumwa kimya!! Uchungu umefika? Na hapo mimba Bado sana muda wa kujifungua wife yupo kimya.

Nikaanza kupapasa huku,kule na humo lkn wapi....

Kama dk 9 Hivi ndo ananiambia nahitaji embe la kutafuta Mimi.

Wakuu hapa Sasa niliishiwa ujanja nikasema ama amepata kifafa Cha ujauzito huyu embe saa7 hii natoa wapi!?

Nikajua huenda ana test mitambo. Basi nikaanza kujieleza kuwa napata wapi Sasahivi mke wangu watu wamelala na hapa ni mjini maembe Hadi kule mashambani?

Jibu sipewi analia tu. Nikaendelea kusema ukizingatia kipindi hiki sio msimu wa maembe kabisa natoa wapi Hilo embe vumilia tulale kesho nitafanya juu chini tupate.

Wakuu Kila nikimaliza kuongea naambiwa anataka embe bichi la kutafuna!!.

Aisee akili ikanijia hapa niende tu huko mashambani iwapo nitakoswa nikalale Kwa jirani hapana kwakweli sitaweza kukesha naliliwa usiku kucha Mimi.

Nikawasha pikipiki muda huo ni mishale ya saa7:37 Hivi usiku. Nikaenda Hadi shamba Moja Hivi la mzee wa kanisa flani.

Muda huo nilikumbuka sana umhimu wa tochi wakuu. Smart yangu sawa ilikuwa inawaka ila mwanga umesambaa hata haufiki mbali.

Nilizunguka miti kama 4 hakuna kitu. Ujue ni usiku na kumetulia kabisa. Nikajisemea Sasa naenda mti wa mwisho nikikoswa naenda kulala Kwa jirani yangu kwakweli.


Nimeenda huku namuomba Mungu nipate asee. Bahati nzuri nikaona kaembe kadogo na kachanga ni aibu hata kukachukua ila nikajisemea acha tu niende Nako haka haka kama ushahidi kuwa nimekoswa embe mke wangu.

Kipindi najaribu kuwasha pikipiki Ili nirudi haiwaki fanya Hivi na vile wapi nikaanza kusukuma nilitumia kama lisaa kufika nyumbani ukijumuisha na muda wa kuzunguka kwenye miembe almost masaa2 yanafika!!

Nikawa nimefika kaembe nimekaweka kwenye mfuko wa suruali nikafunga na zipi kabisa kasidondoke.

Nafika nyumbani namkuta kanisubiria Nje mlangoni kulia halii amekaa tu. Nilikuwa na hasira sana lakini nilijikaza tu.

Nikamwambia aisee embe nimekoswa kabisa nimezunguka nikaona haka tu kachanga.

Kalikwapuliwa chap kama mwewe anapita na kifaranga na kakatafunwa Hadi kale ka mbegu ka embe vinakuwaga vyeupe.

Nilishangaa Sana. Hapo hapo tukaanza na story na vicheko ila moyoni ukinifunua nime mind vibaya mno.

Akauliza kwanini pikipiki umekuja unaisukuma mafuta yameisha. Nikamwambia hata sijui imegoma tu pindi naanza kurudi.

Kesho yake nikagundua kumbe nilizima kwenye Ile batani ya stop engine asee nilijidharau sana.

Nilikaa nae nikamwambia kama mimba Yako inakupelekesha Hivi. Ukija kuniambia Tena nitaenda mazima sitarudi nitalala nitakapo lala asee siwezi kwenda kwenye miembe inayo ogopeka vile halafu usiku wa manane je niking'atwa na nyoka utapata faida Gani?

Nikamwambia msimamo wangu ndo huu. Sitakaa nifate Tena Kwa sababu nilkuwa sijakumbia nimekuambia Sasa Jana umeniuzi mno.

View attachment 3136351
Vitu vingine ni kuendekeza ujinga, na wewe ulivyo kilaza ukaenda kutafuta maembe usiku? Mbaya zaidi utakuta hata hiyo mimba sio yako. Kuwa na akili wewe acha utoto.
 
Halafu hii ni kama wote anaweza kukwambia anahamu na kitu flani ukileta anabadiri gia anakwambia hamu imekata.au akununie tu.



Kuna mimba Tena ya mtoto wa3 nguo zake alikuwa havai ni nguo zangu tu mashat ya mikono mirefu ama mifupi nikajiuliza Nini hiki?

Ukienda chooni usiku unafatwa unakata gogo anakuongelesha asee mkuu ni mengi sana yakusema
Ndo maana inatakiwa mtu uoe umekomaa akili
 
Mi nilimuuliza "Unadhani wewe ndiye mwanamke wa kwanza nayemuona akiwa na mimba?"

Kabla hajajibu nikaongezea " You got to be rational, andika cravings zako nije nazo nikitoka job. Keep it smart"
Jibu: Okay babe.
Na mtoto akazaliwa bila kusumbuana.
 
Mi nilimuuliza "Unadhani wewe ndiye mwanamke wa kwanza nayemuona akiwa na mimba?"

Kabla hajajibu nikaongezea " You got to be rational, andika cravings zako nije nazo nikitoka job. Keep it smart"
Jibu: Okay babe.
Na mtoto akazaliwa bila kusumbuana.
Mkuu hata Mimi niliwaza nitumie uanaume nikaona hapa nitaliliwa zaidi.
 
Vitu vingine ni kuendekeza ujinga, na wewe ulivyo kilaza ukaenda kutafuta maembe usiku? Mbaya zaidi utakuta hata hiyo mimba sio yako. Kuwa na akili wewe acha utoto.
Hapa Kila mtu ana mzigo wake mkuu. Kama hujawah ambiwa unaweza sema lolote. Kuhusu mimba hata sisi tumezaa Nje hivyo yote heri mkuu
 
Wengine hadi aje kujifungua familia nzima kama imejitua gunia la mawe mabegani.

Mwanaume usiwajulia wanawake wa aina hiyo utakosa utulivu wa nafsi.
Hata ukilala utakuwa kimagutugutu tu kila siku
Utapelekeshwa wewe ukome.
Mara ajifanye anaumwa kumbe mzima wa afya .
Nilimwambia ni mwisho asirudie. Hajawahi fanya Tena!!
 
Yani kuna mwanamke akishika mimba ndani ya nyumba wote mume na other family members wote mko kwenye shida.
Wote kama mko na hiyo mimba 👌👌👌
Mke atadeka huyo hadi kuchosha.
Nongwa na yeye kama zote .
Kujifanya kuchagua vyakula.
Jamani mimba sio ugonjwa.
Ujauzito ni baraka.

Kwanini unawaelemea wenzio kwa nongwa żako mama ?! 🤔🤔
Mimi nilipiga marufuku kula Pemba. Akawa anafatia madongo ya kichuguu mengi . Nilijua ataugua lakini wapi.
 
Back
Top Bottom