Wife aliniamsha usiku wa manane ni mfuatie embe bichi kisa ana mimba

Ndo maana vijana ambao hawajakomaa wanawapiga wake zao kama ngoma za kijiji
Kabisa.Siku napeleka kliniki nurse alisema Kuna maudhi flani flani utapitia katika kipindi hiki Cha mimba hivyo kuwa mvumilivu umvumlie mwenzio. Kweli bana ndo yakanikuta. Wanao tuonane eti tunaendeshwa nawaona ni wavulana tu kama wataalamu wa afya wanayatambua hayo maudhi kwanini nipinge?
 
Mimi tungekesha tunabishana siwezi kutoka usiku wote huo kwenda kutafuta Embe
Yamewahi kukututa mkuu? Kaka yangu alitorokwa kisa tu ana muangalia vibaya. Tena mwanamke akasema ndoa iishe tu. Kama utani Shem alienda kwao akienda kumfuata ama kupeleka matumizi nikusalimiana anaenda kulala Hadi aondoke basi nikawa napeleka Mimi tunacheka Hadi basi.
Siku Moja nikamwambia twende Kwa wazazi wetu akakubali ila Kwa kaka akakataa na Hadi alipojifungua akaenda bila hata kikao chochote.
 
Ndo ukubwa mzee
 
Uongo gani tena
Hiyo story ya embe. Ni uongo mtupu.

Hakuna mwanamke mjamzito akashikwa na hamu ya kitu cha kula kisichokuwepo au kisichopatikana kwa wepesi au mbadala wake.

Mjamzito kwenye kula mara nyingi hangoji kuletewa. Simu za siku hizi? Angeshaagiza embe na angeshajuwa wapi azipate, wala asingelia.

Mnadanganyana na wenyewe tupo hapa?
 
Kiukweli wanawake wenye mimba kuna muda wanakera,mi wa kwangu aliniagiza samaki mda huo nna 6000/= mfukoni nikanunua samaki ya buku 5,mwanaume nikabaki na buku

Nilivyomfikisha yule samaki wife akasema hamu ya samaki imeisha dah
Naomba niijibie hii. Kiukweli tunakuwa na hamu na huwa pia zinakata abruptly. Ila tu ni kutumia hekima na kumueleza mwenza wako unachokuwa unapitia ili awe anaelewa situation iliyopo. Ni vipindi vya mpito tu, though wengine huwa wanaexaggarate. Mi dada yangu alinikanyaga akaniambia ole wako nisikie unamnyanyasa shemeji na drama za mimba, we hutakuwa wa kwanza by the way kubeba mimba. So mi ninachoona ni kuwa kukosa hamu ya kula na little mood swings ndo zipo ila hazitoi sababu ya kumtesa mtoto wa mwanamke mwenzio.
 
Kweli bibie
 
Sio uongo hayo mambo yanatukuta wanaume
 
Ni kweli mjamzito anapitia nyakati ngumu kama kichefuchefu,kujisikia ovyo,uchovu nk lakini mambo mengine wanajiendekeza na mwanaume ukikaa kindezi hadi mavi utazoleshwa.

Mm wa kwangu alileta pigo hizo,mara usiku kucha namshika shika tumbo,mara nifuatie udongo,mara nifuatie mtoei baa fln mbali kichizi,mara leta vest zako ninuse nk nk,mwanzoni nikawa nafanya lakini baadae nikawa nikitumwa tu naishia baa,napiga mtungi wa kibabe,narudi usiku mnene,namkuta mpooole kashanimiss huku sina habari wala nn. Mbona alikoma
 
Huko kudekadeka kwao ndiko kunasababisha wengi siku hizi wanajifungua kwa njia ya uoasuaji Yaani operation badala ya njia ya kawaida ya asili.
Sababu they don’t keep active themselves kipindi chote cha ujauzito.
Kazi kulala tu na uvivu.
Kila kitu dadaaaa kalete kile , dadaaa nipo kile, dadaaa kachukue kile ulete.
Activeness utatoka wapi ya kusukumw mtoto leba ?!
Ni mwendo wa visu tu sasa.

Lakini mwanamke akiwa anajifanyia shughuli zake za nyumbani awapo home mwili inakuwa active tayari kusukuma mtoto atoke.
 
Nawakubali sana wanawake wanaojifungua kwa njia ya kawaida.
Though wengine ni sababu ya umaskini uwezo wa kulipa Hela za operation hawana inabidi wajitahidi kwa njia ya asili kuepuka gharama.
Lakini kuna wale Hela anayo lakini ni hodari yuko active anafanya kazi za nyumbani badała ya kuachia Mjakazi afanye kila kitu
 
Siyo yeye ni huyo aliye naye ndani yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…