Wife hanijali mimi kabisa wala lolote ninalofanya

kyanyangwe

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2018
Posts
1,275
Reaction score
3,316
Kwema wakuu?

Nilikua nimekaa mahali ninakula msosi, kuna jirani yangu pembeni akawa anaongea na mkewe kwenye simu. Ebana wanavyoongea hadi raha yani. Mkewe anamuuliza jamaa siku yake imeendaje, anamuuliza anakula nini na pia amemsisitiza jamaa awahi kurudi home jion.

Kwa upande wangu, nikiishaondoka asubuhi home wife hana habari na mimi kabisa labda itokee tu emergency ndio anaweza kunitafuta. Yaani mimi naweza hata kukaa nje ya nyumbani mpaka usiku wa manane na wife wala hata asipige kuniulizia.

So nawaza, hapa napendwa au ni bora tu siku ziende?
 
Huna kismat wahii Fasta kwa mkali ooh ukichelewa itakula kwako si unajua dunia hiyi watu hawapendi uoe mzee mwenzangu
 
Hivi una Habari maswali ya “babe umekula nini”yanavyokera yakizidi kila siku.

Siyapendi
Ahaha mkuu wengine wanapenda sana hiyo,si unaona kama mtoa mada anavyotamani kuulizwa.

Btw nishawahi kuwa na mpenzi kati ya swali hapendi kuulizwa ni "umekula nini?" Ila kuna mwingine,akawa hadi ananisema sipo romantic kwanini siulizi mambo yake na siku yake,yani hata akienda job anataka niulize "ulifika salama?" So watu wanatofautiana sana.

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli watu wako tofauti lakini si kila siku muda ule ule unaniuliza swali lile lile kwa miezi sita mfululizo.hapana kwa kweli
 
Tayar uyo kuna mwingine anamkuna wakati haupo....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…