Wife kaniambia anampenda Mungu kuliko mimi

Wife kaniambia anampenda Mungu kuliko mimi

Inategemeana ni mungu yupi asijekuwa kiongozi wa dini. Mtoa mada una hoja japo punguza hasira kwanza. Linapokuja suala la ndoa hata Mungu analiheshimu tena sana. Huwezi tumia Mungu kuacha kumheshimu Mume, kuhudumia familia mahitaji ya msingi, kumtosheleza mke au mume ati kisa ibada la hasha. Hapo Mke kakosa hekima kabisa na anastahili baraza. Ni Mke kiburi anayejificha kwa Mungu.
Kuna mama mmoja nilisikia shuhuda hii. Mumewe alimzuia mambo ya ibada kabisa alichomjibu ni hiki "Yesu nampenda na wewe nakupenda pia sitowaacha". Kila alipokuwa akijbu hivyo kipigo kilitembea lakini siku zote aliendelea kujibu hivyo mwishowe mume alisalimu amri mpaka leo wako wote wakimtukuza Mungu.
Swali la mtego unawezaje kuishi na mtu anayetoa misimamo chanya bila ya kutumia hekima ili asimkwaze asindananaye?. Nadhani tumsaidie mtoa mada kujibu hili swali na sio kumshambulia ati apambane na Mungu.
 
Amri ya kwanza: Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote...
 
Back
Top Bottom