Bwana Bongo
Senior Member
- Dec 12, 2021
- 167
- 239
Wiki moja toka nichapishe chapisho kuhusu ni namna gani ya kujikinga na wezi unapokwenda sehemu zenye mikusanyiko ya watu wengi niliibiwa
Kwanza unachokisoma kwa watu mbalimbali humu unatakiwa kuchanganya na zako, as long as hakitakuwa na shida upande wako, maana kila mtu ana andika jambo kutokana na uzoefu wake
Wakati nachapisha kilikuwa kipindi ambacho, naweka pesa kwa ajiri ya kutimiza mahitaji ya mavazi,
Kwakweli ili nibidi nikaze uzi maana pesa niliyokuwa nikiipata na mahitaji vilikuwa vitu viwili tofauti, kwahiyo kuna wakati ilinibidi nisile kutwa nzima hivyo hivyo mpaka nikatimiza lengo
Siku iyo naamka kwa bashasha nikiwa na mdogo wangu, tunaenda zetu ilala boma kujipatia nguo ambazo kwa pesa yetu ndiyo zingetufaa, tunashuka zetu mitaa ya gerezani tukishika mitaa ya msimbazi mpaka uhuru hapo tena tukanyosha mpaka tulipofika ilala sokoni,
Nikajichanganya na watu kujifanya machinoo, jamaa anatangaza "Oya tatu bei, wapi tatu , tatu bei" nikatazama ile nguo iliyo nivutia kweli nikasogea nikimwambia anirushie alirusha nikaikagua nilipoona inanifa, nikaweka pesa nikamrudishia ili anipe chenji yangu, jamaa alidai kuwa chenji hana nisubiri, nilisubiri kitambo kidogo kabla ya kupigwa vikumbo viwili vitakatifu na nilipo peleka mkono katika mfuko niliyoweka pesa azikuwepo, hapo nikaomba chenji yangu haraka nikapewa. Shwainiii!😀