Wiki sasa sina amani

Wiki sasa sina amani

Acha kuwadanganya watu humu yaani uzi mzima usiulize dalili za ukimwi zinaanza kuonekana baada ya muda gani maana ndio kitu cha kwanza mtu akipitia hali huanza kuuliza mara kwa mara.
 
Habari za muda huu ndugu zangu,

Wakuu nina week sasa nimekuwa na hali ya unyonge tangu nikutane na kopo la vidonge kwenye droo la huyu mwenzangu.

Hali ambayo imenistua zaidi hivi vidonge nina asilimia mia ni vya HIV.

Kuna siku nilimfuma anakunywa kwa siri nikauliza akasema ni dawa za vidonda vya tumbo..

Wakuu nina wasi wasi sana maana hata ishu ya kupima yeye ndio alifosi mimi nikapime nimletee majibu.

Baada ya kusema hivo nikajiwekea asilimia mia kua yeye yupo salama..

Ila mpaka sasa nimekua na wasi wasi mno.

Nataka kujua yafuatayo wakuu wenye experience hivi mtu anayetumia dawa vizuri kabisa ni kweli hawezi kuambukiza au ni story za vijiweni...?

Na ile ya kusema kuna watu hawapati virusi ni kweli au ? maana mpaka sasa naona nipo poa kabisa...

Wakuu ni week sasa hata hamu ya kula chakula cha usiku sina mpaka ananistukia sasa...

Najuta.... Kitu kinachoitwa kupima kwa sasa HAPANA
Wewe ni Poor brain kweli🤣🤣.sasa unaogopa nini kama ulipokuwa unapanda mchongoma ulitegemea kuota mpera
 
Back
Top Bottom