Wiki ya Huduma kwa Wateja: Taasisi gani ina Huduma Nzuri kwa Wateja mpaka unatamani wengine wajifunze kwao?

NSSF wako vuzur sana
 
Mfumo wa Tanesco. Kitengo cha huduma kwa wateja kipo vizuri. Hii ni kwasababu wameweza kushusha huduma zao mpaka ngazi ya chini kabisa kupitia whatsap group.

Wanajitahidi mashirika mengine wakajifunze

Nipo kwenye group moja huwa naangalia sometimes watu wanauliza vitu ambavyo usingetarajia watauliza lakini bado wanajibiwa .
 
Brela ni Taasisi ya hovyo natamani raisi na viongozi wote wa Jeshi , Polisi, Mgambo, na Kila mtu wamkamate mkurugenzi wa Brela achapwe viboko sana.


Brela wana usumbufu kuanzia kusajiri kampuni Hadi kufile taarifa zingine za kampuni kama Annual returns na Beneficial Ownership. Hapo sijataja kuabiri taarifa kadhaa za kampuni unaweza kukaa hata miaka.


Kama serikali wangejua NAMNA Gani BREla inaihujumu serikali kwenye issue za uwekezaji huyo mkurugenzi wake angekuwa either jela au nyumbani. Haiwezekani nchi inataka wawekezaji na tunafukuzana na dira 2050 halafu kusajiri kampuni iwe miezi 6. Kufile returns miezi mitatu.


Nina ushahidi ( Empirical Evidence ) na ninaweza kuzutoa kuonesha brela wakikatisha tamaq investors na kuhama nchi Kwa milolongo ya hovyo. Najua watabisha ila wajue ipo siku Hadi sauti zao zitamwagwa hadharahi.



Taasisi Bora Kwa Huduma Bora Tanzania ni TISEZA chini ya TERI. Huyu jamaa Sina cha kumueleza. Tembeleeni TISEZA mtaleta ushuhuda.
 

Bar ya Matako matako. Mteja unapewa na mwanadada mwenye makebo akusindikize ukalale.
 
Habari ndugu mteja,

Asante kwa pongezi, tupo kwaajili ya kuboresha huduma. TANESCO tunayaangaza maisha yako.^NI
 
Ndugu mteja, asante kwa kuwasiliana nasi.

Tunashukuru kwa Pongezi, tumepokea na tutazidi kwenda hatua zaidi katika kukupatia huduma bora.^NI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…