Wiki ya Huduma kwa Wateja: Taasisi gani ina Huduma Nzuri kwa Wateja mpaka unatamani wengine wajifunze kwao?

Wiki ya Huduma kwa Wateja: Taasisi gani ina Huduma Nzuri kwa Wateja mpaka unatamani wengine wajifunze kwao?

FANIKIWA MICROFINANCE BANK na BYPORT Wako vizuri sana kwenye huduma zao maana kila siku wanakutumia messeji kwa namba tofauti kuku-kumbusha huduma zao. Ili ukiwa na shida za kifedha usiteseke.
Nawapa maua yao.
 
At least TANESCO, MAKAMPUNI YA SIMU Kidogoooo. mnyonge mnyongeni haki yake mpeni wanajitahidi sana mapungufu ni ya kawaida. Kwa upande wangu NIDA, RITA wanajisikia sana wanaona ni kana kwamba washamaliza kila kitu hapa Duniani Customer care yao ni mbovu sana.
 
Fanyeni maboresho
Tuache kujaza token kwenye kile ki mita badala yake mtu akinunua umeme, mfumo ufanye update ya kupokea malipo automatically. Kama vile tunavyofanya malipo mengine ya serikali kupitia control number.
Habari ndugu mteja,

tunapenda kukufahamisha kuwa zoezi la mfumo mpya wa matumizi ya mita janja (smart meter) tayari limeishaanza kwa baadhi ya Mikoa nchini. Ili kujua ni lini eneo lako litafikiwa na kupata taarifa sahihi za ratiba ya ufungaji wa mita janja, tafadhali tembelea ofisi ya TANESCO iliyo karibu na makazi yako.^HN
 
At least TANESCO, MAKAMPUNI YA SIMU Kidogoooo. mnyonge mnyongeni haki yake mpeni wanajitahidi sana mapungufu ni ya kawaida. Kwa upande wangu NIDA, RITA wanajisikia sana wanaona ni kana kwamba washamaliza kila kitu hapa Duniani Customer care yao ni mbovu sana.
Habari ndugu mteja,

asante kwa kuwasiliana nasi, tumepokea pongezi yako, tunaenda hatua zaidi katika kukupatia huduma bora, tunakutakia wakati mwema.^HN
 
Wiki ya Huduma kwa wateja huadhimishwa Duniani kila mwaka katika wiki ya kwanza ya mwezi wa Oktoba kwa taasisi za serikali na kampuni binafsi kusherehekea, kutathmini na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi na wateja.

Ikiwa ni ukingoni mwa Wiki ya Huduma kwa Wateja, ni taasisi gani inaongoza kuwa na Huduma nzuri kwa Wateja mpaka unatamani nyingine zijifunze kutoka kwao?

HESLB Dar Es Salaam, huduma yao ni nzuri sana. Wanahudumia haraka sana tena kwa ukarimu.
Ni kama vile mfanya bihashara anavyomkaribisha mteja
 
Back
Top Bottom