Wiki ya Huduma kwa Wateja: Taasisi gani ina Huduma Nzuri kwa Wateja mpaka unatamani wengine wajifunze kwao?

Wiki ya Huduma kwa Wateja: Taasisi gani ina Huduma Nzuri kwa Wateja mpaka unatamani wengine wajifunze kwao?

AZAM na VODACOM nataka hela yangu, haiwezekani nikienda AZAM wanasema hela iko VODA na nikienda VODA wanasema ipo AZAM, narudia tena nataka hela yangu, mkiweza change changeni mnilipe 28k yangu nyau nyie.
 
Mfumo wa Tanesco. Kitengo cha huduma kwa wateja kipo vizuri. Hii ni kwasababu wameweza kushusha huduma zao mpaka ngazi ya chini kabisa kupitia whatsap group.

Wanajitahidi mashirika mengine wakajifunze

Nipo kwenye group moja huwa naangalia sometimes watu wanauliza vitu ambavyo usingetarajia watauliza lakini bado wanajibiwa .
Sasa mbona huku JF wametuwekea li roboti lao ndio linajibu? Waje nahuku wawe wanatujibu sio kuweka roboti
 
TTCL ni majanga, kuanzia meneja hadi mtu wa chini kabisa, unaomba huduma ya fiber unamaliza mwaka hujapata.
 
Mm nakumbuka marry alinihudumia vizuri akanambia we acha apa nakufanyia mwenyewe uje uchukue siku flan afuu sauti yake tabasamu macho😁😁

bahat mbaya alikuwa ameolewa🥺 nilikuwa tayar kumwacha uyu wangu mwenye komwe nimchukue marry
 
Mfumo wa Tanesco. Kitengo cha huduma kwa wateja kipo vizuri. Hii ni kwasababu wameweza kushusha huduma zao mpaka ngazi ya chini kabisa kupitia whatsap group.

Wanajitahidi mashirika mengine wakajifunze

Nipo kwenye group moja huwa naangalia sometimes watu wanauliza vitu ambavyo usingetarajia watauliza lakini bado wanajibiwa .
Wakati January makamba about source kitengo cha Huduma Kwa wateja mlikuwa mnamtukana ni Tapeli.


Leo Kila mtu humu anasifia Huduma Kwa wateja ya tanesco bila kumpa maua yake January makamba
 
Ndugu mteja,

Asante kwa pongezi, tunaenda hatua zaidi katika kukupatia huduma bora.^NI
Fanyeni maboresho
Tuache kujaza token kwenye kile ki mita badala yake mtu akinunua umeme, mfumo ufanye update ya kupokea malipo automatically. Kama vile tunavyofanya malipo mengine ya serikali kupitia control number.
 
Back
Top Bottom