Wiki ya Huduma kwa Wateja: Taasisi gani ina Huduma Nzuri kwa Wateja mpaka unatamani wengine wajifunze kwao?

Nipo kinyume na mada

NMB na NHIF Nina mwezi sasa kila nikipiga huduma kwa wateja wananambia mhudumu anaongea na mtu mwingine
NHIF ni kama wanatoa huduma za TASAF yani wao ndio wanakupa hela wewe takataka wale
 
TANESCO wapo vizuri sana sana na tungekuwa na Taasisi za Serikali kama ilivyo TANESCO tungekuwa mbali kama Taifa.
TANESCO hingereni sana
 
TANESCO wapo vizuri sana sana na tungekuwa na Taasisi za Serikali kama ilivyo TANESCO tungekuwa mbali kama Taifa.
TANESCO hingereni sana
Habari ndugu mteja,

asante kwa kuwasiliana nasi. Tumepokea pongezi zako na tunakushukuru kwa kutambua juhudi zetu katika kuboresha huduma zetu. TANESCO tunayaangaza maisha yako. ^HN
 
Baadhi ya hiyo mikoa ni ipi
 
TANESCO nawapa maua yao!! Customer service ni A+!
Habari ndugu mteja,

asante kwa kuwasiliana nasi. Tumepokea pongezi zako na tunakushukuru kwa kutambua juhudi zetu katika kuboresha huduma zetu. TANESCO tunayaangaza maisha yako. ^MY
 
CRDB tawi la Mbezi Louis pale. Kuna dada alinipokea kwenye kadirisha kadogo hivi. Kulikuwa na vyeti vingi kuonyesha kwamba alikuwa ametunukiwa tuzo ya best customer service mara nyingi.

Yule dada alinisikiliza vizuri kwa sauti ya upole na heshima sana mpaka nikashangaa. Japo hakuweza kutatua shida yangu lakini alinipeleka ndani huko kwa mtu mahususi na akaniambia nikimaliza hapo nipite dirishani kwake kumjulisha kama shida yangu imetatuliwa. Nilipita kweli kumjulisha akaniaga kwa bashasha sana na CRDB is here for you juu. Na kadi yake akanipa.

Najua CRDB ni benki ya hovyo na nilikuwa na mpango wa kutemana nayo mazima lakini binti yule alinifanya nikaahirisha hilo zoezi japo kwa muda tu.

Mashirika haya wangejua umuhimu wa customer service aisee wangewekeza sana huko maana ni sehemu ya muhimu sana!
 
ASA, TARI, TALIRI, TFRA, EWURA, TANESCO, TTCL
Habari ndugu mteja,

asante kwa kuwasiliana nasi na tumepokea pongezi zako. Tunaenda hatua zaidi katika kukupatia huduma bora. Tafadhali endelea kufurahia huduma zetu. ^MY
TANESCO NAMBA 1
Habari ndugu mteja,

asante kwa kuwasiliana nasi na tumepokea pongezi zako. Tunaenda hatua zaidi katika kukupatia huduma bora. Tafadhali endelea kufurahia huduma zetu. ^MY
 
inaonekana mnafurahia sana hizi pongezi , maana mnajibu mara mbilimbili sasa 🤣
 
inaonekana mnafurahia sana hizi pongezi , maana mnajibu mara mbilimbili sasa 🤣
Walizikosa muda mrefu. Hapa Menejimenti za Taasisi nyingine za Serikali wajifikirie na kujipima, nafikiri wanaona namna ilivyo raha kufanya kazi nzuri.

Kuna TTCL - Hawa ni kama wamekalia mgodi na hawajui wafanye nini. Internet yao ya faiba ni nzuri sana lakini ni kama wanakwambia hawana haraka ya fedha yako. Naomba kama kuna Mtu alishawahi kuunganishwa na huduma ndani ya kipindi cha wiki moja. Halafu sababu zao rahisi tu 'router zimeisha'. Ni sawa na mwenye basi akwambie leo hakuna safari kwa sababu tairi hakuna. Kiukweli ukiona umehudumiwa vizuri ujue ni jitihada binafsi za mfanyakazi na si nature ya Taasisi.

NHIF - Kuaminisha umma kuwa ukiwa na bima unapata dawa na huduma zote kumbe ni vinginevyo, matokeo yake Vituo vya afya kuonekana ni wezi.

Brela - Kwanza hujui ni lini usajili wako wa kampuni au jina la biashara utakamilika. Pili, ukisajili jina la biashara kama utaratibu wao unavyoonyesha - 'ku-screen' kama jina unalotaka kutumia linatumiwa na mwingine. Na likipitishwa na kulipia usishangae unarudishwa kufanya marekebisho. Angalia mfano hapo chini;



Dear, .........................

Please be informed that BRELA processed the Application No G-----------, for Registration of new business name submitted on 28/01/2024 --- via the BRELA system.
The application was returned to you for additional information / correction to be submitted for the same application. Comments of BRELA:
1) Similar------, kindly propose another name
We kindly ask you to update the same Application in the BRELA system and submit it to BRELA for processing.

Instruction how to find the same application: after logging to BRELA system, you can find the Application in the 'My list' menu item (please use "Tracking No" = G230126-0060 filter). Click here to proceed
This is an automatically generated email, please do not reply. If you received this email by mistake, please contact BRELA ORS help desk for assistance.
Regards,

Online Registration System

Business Registrations and Licensing Agency

Contact: orsinfo@brela.go.tz



Sasa kama ilishapita na kwamba ufanano hauzidi 50% kwa nini nifanye tena mabadiliko. Kwamba hata system yenyewe haimaniki mpaka binadamu apitie tena!!

Ingekuwa na halmashauri ni Taasisi nafikiri server za JF zingejaa.

Kuna hili
 
Reactions: Lax
taasisi zembe zembe zote ni kuziburuza kwa lazima tu mpaka watakapokaa sawa. TAnesco inashangiliwa sana kwakua imeonesha progress nzuri sana
 
Uzi mzuri hongera sana,napendekeza kwa taasisi za umma waige kuboresha huduma zao kama wanavyofanya NSSF
 
Taasisi ya wadada wa kumbi za starehe ukilipia bill lazima wakupe nishati.Tanesco unalipia lakini bado wanakata nishati na kuniacha gizani.
 
taasisi zembe zembe zote ni kuziburuza kwa lazima tu mpaka watakapokaa sawa. TAnesco inashangiliwa sana kwakua imeonesha progress nzuri sana
Habari ndugu mteja.

Asante kwa kuwasiliana nasi na asante kwa pongezi, tupo kwaajili ya kuboresha huduma zaidi. TANESCO tunayaangaza maisha yako.^RS
 
Benjamin mkapa hospital nilipata huduma nzuri mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…