Wikiendi ya Leo: Niulize Chochote Kuhusu Mimi Nitakujibu!

Mkatoliki lazima aamini Katika Mapokeo, Asipoamini hivyo bas kuna walakini katika ukatoliki wake!
Kumbe mnaruhusiwa kutumia jina Yesu ktk maombi. Basi ilikuwa ni hilo tu
 
Kumbe mnaruhusiwa kutumia jina Yesu ktk maombi. Basi ilikuwa ni hilo tu
Mkuu Yesu ndiye Mkombozi wetu, Kanisa katoliki limejengwa Katika yeye, Ndio maana Kila tuombapo Kwa Mungu Tunasema, Tunaomba hayo kupitia Bwana wetu yesu Kristu Mwanawe, anayeishi na Kutawala nawe Katika Umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu Daima na Milele!
 
Amina

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikuulize kuhusu wewe yupi? wa hapa jukwaani au wa mtaani?
 
Tazama jinsi ukuu was Mungu ulivyo!!

Kwa andiko lako nilitegemea utaambulia maswali yenye kukarahisha,mzaha na mengi yasiyofaa kama ulivyo kawaida kwa post kama hizi.

Hadi kudikia post ya 22 bado busara na HEKIMA YA MUNGU vimetawala mjadala.

MUNGU akubariki.


Swali. Ni neema gani anazikosa mkristo Mkatoliki ambaye ama kwa makusudi au kutojua anaamua kutofika kanisani kwake na badala yake kuamua kwenda kusali katika dhehebu jingine siku za ibada/misa huku akiendelea kujiita Mkatoliki?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akubariki Pia na wewe, Nafurahi na Nafarijika sana kwa Maoni yako Haya ya Kipekee..
 
Swali. Ni neema gani anazikosa mkristo Mkatoliki ambaye ama kwa makusudi au kutojua anaamua kutofika kanisani kwake na badala yake kuamua kwenda kusali katika dhehebu jingine siku za ibada/misa huku akiendelea kujiita Mkatoliki?
Mkuu Lucky star, Amri ya Kwanza ya Kanisa inasema Hudhuria Dominika Zote na Sikukuu zilizoamriwa, Katika Misa za Dominika Kuna Ekaristi, usipohudhuria lazima utaikosa hii Neema ambayo ndio uponyaji wa Roho zetu, Pili kama mtu huyo atakuwa anasali kwingine inakuwa ni ngumu kwake kuhudhuria jumuiya ndogondogo za kikatoliki kitu kitakachosababisha ashindwe kutambulika kama Mkatoliki kamili, kwa kitendo hichi inakuwa ni vigumu kwake kupata huduma za kikanisa kwa urahisi!
 
Barikiwa sana kwa jibu zuri lenye rejea hai

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sina swali ila hongera mkuu unajitahidi kutupa elimu ya dini ya kikristo

ubarikiwe sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…