Wilaya ya Handeni ina waganga wa jadi 6600, Kwamsisi inasifika zaidi

Wilaya ya Handeni ina waganga wa jadi 6600, Kwamsisi inasifika zaidi

Halafu unapewa sharti hakuna kunywa gambe!
Hapo sasa mtihani
Ila nataka uganga wa dili😂😂
Wa Kim Kimchongo
Kuna mwanangu mmja alikuwa anaenda afrika kusini kupiga deal hizo akiwa bongo anauza duka lake la sim na vifaaa vingine
Sema walikuja mshtukia akalaga kona

Ova
 
Acha utani mkuu tanga wilaya zenye shida ya maji Ni handeni ,kilindi na mkinga kidogo .

Kwengine kote maji yako bwerere .

Tanga mjini ndio mahali kwenye Safi na salama Tanzania. Nzima unaweza hata kunywa bila kuyachemsha usidhurike.

Kuna mahali lushoto mfano bumbuli nasikia hawalipi kabisa bili za maji na maji yanatoka kwenye mabomba .

Pangani maji yamejaa bwerere vile vile korogwe .

Case ya handeni na kilindi hizo wilaya zina uharibifu wa vyanzo vya maji ,ukataji wa miti kwa ajili ya mkaa inapekea ukame ukame kutawala.

Unataka mapenzi njoo msambweni ,magomeni,donge,Hadi mwakidila Kisha kisosora ,chumbageni,kwamichi Hadi kange utapewa mapenzi shata shata ,Mambo ya maji iliki ,kisosa acha bwana .

Tanga raha


Si kweli kwamba Handeni na Kilindi hakuna maji sababu ya uharibifu wa vyanzo vya maji.

Nakataa kata.

Hata ukataji miti siyo ukweli.

Usiwape excuse serikali yenye jukumu la kutuletea huduma muhimu ya maji wakapata sababu isiyo kweli.

Tumuogope sana Mungu.

Tangu Uhuru hadi leo Wilaya za Handeni na Kilindi hazina huduma muhimu ya maji.

Yani imeshindikana kabisa hata makao makuu ya Wilaya hizo maji hakunaga .

Hospitali ya Wilaya bomani maji shida.

Mashuleni pia maji ni shida
Kila mahali maji ni shida kubwa.

Mto ruvu uko jirani pale korogwe lakini Handeni na Kilindi hakuna maji tangu kabla na baada ya Uhuru hata sasa.
 
Hivi huko miaka ya nyuma Mbunge wao si ndio alikuwa Prof.Longwater?
 
Kwa msisi nishapiga dili jamaa alikuwa mganga akaniletea ndy sivyo,nlimtimbiga nkampora sim na sub ufa huko
Alinipiga mkwala nkamwambia kama yeye aliumba dunia basi afanye vyvyt
Kwangu

Ova
 
6,600 ni orodha ya waganga wakienyeji na wachawi, hapo inaelekea wote wameorodheshwa ila hajaelezea kama waganga na wachawi wote wanahudumu wilaya ya Handeni, na nivofahamu HANDENI ina uhaba wa Madaktari na maji lakini suali linakuja: je serikali inatambua uchawi na wachawi?
Kama imewasajili na kutoa idadi yao hao wachawi(pamoja na serikali kutotambua uchawi)kwanini isiwachukulie hatua kwa kosa la ulozi pia na kukwamisha maedeleo ya HANDENI?.
huyo mkuu wa wilaya anatafuta kiki na sidhani kama anauzoefu wa nyanja ya utumishi wa umma, bora apate ushauri kwa walomtangulia akina Godwin Gondwe
Kasema io idadi ni ya waganga sio wachawi. Waganga wanakuaga wamesajiliwa ndio maana kawatambua
 
handeni kirindi mtaa wenye nyumba 100 basi 85 niyumba za wachawi wanao jificha kwenye uganga chezea wazigua na wanguu
Kule naskia ni hatari sana. Watu sijui wanaishi vipi sasa!
 
Nna shamba langu kijiji cha kwasunga
30km kutoka mandera (mbele ya mto wami)

Kwa kule sijawahi kuski habari za kichawi
 
Wilaya ya Handeni imejipanga kuhamasisha jamii kuondokana na imani za kishirikina, badala yake ijikite kwenye shughuli za maendeleo kwenye ngazi za kaya na vijiji.

Wakati yakielezwa hayo wilaya hiyo inatajwa kuwa na jumla ya waganga wa jadi 6,600.

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Toba Nguvila alibainisha hayo baada ya kushtushwa na idadi hiyo na baadhi ya vijiji vyake, kikiwamo cha Kwamsisi kuwa na sifa iliyoenea ndani na nje ya nchi kwa kubobea kwa uchawi. Nguvila kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Muleba.

“Mahala popote nchini, mtu akitishia kwamba nitaenda Kwamsisi basi ataogopwa. Hatupaswi kuiendekeza sifa hii kwa sababu uchawi hauleti maendeleo,” alisema Nguvila na kuwataka kuondokana na sifa hiyo na wawe na sifa ya maendeleo.

Nguvila alitoa kauli hiyo alipozungumza na wakazi wa Kata ya Kwamsisi, baada ya kupokea mradi wa maji wa Kijiji cha Mkaramo uliojengwa kwa Sh143.3 milioni na Shirika la World Vision, akitaka waondokane na sifa ya waganga wengi na wachawi.

Nguvila alisema Wilaya ya Handeni ina fursa nyingi katika sekta ya Kilimo, mazingira, mifugo na madini ambazo zimekuwa zikiwafaidisha wageni na kuwaacha wenyeji katika lindi la umaskini, akisema hali hiyo lazima ibadilike.

Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kwamsisi waliozungumza na Mwananchi walisema imani ya kishirikina imetawala eneo lao na husababisha baadhi yao kushindwa kujenga nyumba za kisasa kwa kuhofia kulogwa na wanaojihusisha na uchawi.
Handeni itabakia maskini milele kwa ujinga wa imani za kishirikina. Nashangaa hadi leo mtu anahofu kujenga nyumba nzuri kwamba atalogwa.
 
Back
Top Bottom