Mahondaw
JF-Expert Member
- Apr 9, 2013
- 75,495
- 185,562
Siku unipelekepo huko Mafia nikasafishe macho loš
Siku unipelekepo huko Mafia nikasafishe macho loš
Kuna rafiki yangu alipata kazi Bank moja tawi la huko nilishangaa gafla akaacha kazi akaondoka huko.Wageni wakifika huku hawakai mda mrefu, maana figisu ni za hali ya juu..
Sasa wewe ulikwrnda kufanya njni huko?Jamii yoyote inayojali "mimi" badala ya "sisi" hujenga mazingira ya mgawanyiko, kutoaminiana, na kurudisha nyuma juhudi za pamoja hasa kwa wale wanaohamia maeneo mageni ili kuazisha maisha mapya.
. Ni wazi kuwa kila jamii ina tabia na hulka zake. Lakini kwa muda niliokaa hapa Mafia, nimegundua jambo moja la kusikitisha ā watu wengi hapa wamejengeka katika mfumo wa uchoyo na ubinafsi wa hali ya juu.
HIZI NI TABIA ZA WATU WA WILAYA YA MAFIA
1. Ushirikiana wa hali ya juu, na ukipigwa kitu kizito huku yakupasa uludi bara moja kwa moja ili kupangua mashambulizi.2. Ni wilaya yenye samaki wengi sana lakini kama siyo mzawa wa Mafia utawasikia kwenye taarifa ya habari maana ni wachoya haswa, mafia ni wilaya ambayo unaweza kuwa na million mfukoni lakini ukalala na njaa.3. Wageni wote kutoka bara huitwa MBWA, hii ilihubiriwa na misikiti fulani hapa Mafia kipindi cha nyuma kidogo.4. Kama ni mtumishi wa serikalii, moja kwa moja unawekewa uadui na wenyeji, maana hawataki kabisa watu wageni kuja kufanya kazi Mafia5. Ni watu wenye tabia ya kuwabambikizia kesi watu wageni ( kesi ya kwanza (i) kufanya ngono na wanafunzi, (ii) kutembea na mke wa mtu, (iii) wakishindwa pande zote tajwa hapo juu, wanahamia kwenye tabia namba moja.6. Kama ni mgeni sahau kupata ardhi ya kujenga, vinginevyo wawe wamekupenda kutoka rohoni mwao na umejadiliwa kwa miaka kadhaa midomoni mwao kuwa unafaa kuuziwa ardhi au laa! .7. Ukifika mara ya kwanza, lazima utajulikana kuwa wewe ni mgeni maana idadi ya watu ni chache sana, hivyo hata Ukifanya kosa linasambaa mpaka kwa viongozi wa juu.8. Milango ya nyumba haifungwi na kufuri maana wanaamini kila mtu aliepo mafia ni mchawi, hivyo usalama ni asilimia 100000%9. Maduka hufunguliwa kuazia mida ya Saa nne asubuhi kwa sababu ya Uvivu walionao,10. Ukiachana na uvuaji wa samaki na dagaa, Kilimo chao ni mchele kiasi, njugu na nyanya kidogo, vitu vingine vyote vinatoka bara.11. Kuna baadhi ya vijiji wanaamini duniani kuna dini moja tu ambayo ni Uislam.12. Ni wilaya ambayo ina kilometers chache za lami sidhani kama hata 200 zinafika, na usafiri mkubwa kwa wale ambao hawana usafiri wao ni boda boda. Maana magari ya abiria sidhani kama yanafika 8.13. Vijana na wazee wa mafia wanapata hela nyingi sana kwenye uuzaji wa samaki lakini nyumba zao zimeezekwa na makuti, huku hela zao zikiwa zimabaki tu mifukoni bila matumizi yoyote yale.14. Mafia ni wilaya yenye ukosefu wa starehe za kidunia ( wadada kutoka bara Sasa wamegundua chimbo, maana naona wanakuja kwa kasi sana kutoa huduma ya utelezi wilayani mafia.15. Mafia ni wilaya ambayo iliwahi kumiliki mbunge mjinga zaidi "Ndugu KIMBAU" alikaa kwenye ubunge mda mrefu bila hata kujenga nyumba ya kuishi, Rais mustaafu KIKWETE Alivyoenda mafia aliomba aende kumtembelea mbunge huyo nyumbani kwake, mbunge kwa vile alikuwa hana nyumba aliamua kumpeleka Rais msikitini.Hii ndo wilaya ya Mafia na viunga vyake.
. Yeah kwa wageni mazingira siyo Rafiki kabisa huku ...Kuna rafiki yangu alipata kazi Bank moja tawi la huko nilishangaa gafla akaacha kazi akaondoka huko.
Halafu jamaa yangu alikua ni wa dini yao .. Yeah kwa wageni mazingira siyo Rafiki kabisa huku ...
. Kila mwaka ma-gape ya kazi lizima yawepo tu kwa sababu wafanyakazi hawakai kwa mda mrefu.
Karibu aana mafiaKulingana na kazi niliyo nayo, hata hapo ulipo kuna siku nitafika tu mkuu..
Sawa, lakini tunakosa kabisa uono wa kuweza kuunganisha viwanda na mashamba vinavyozunguka katika huu mkanda wa Pwani na fursa za kibiashara za Dar?Kibaha inakuja kasi sana
Navijua hadi vijiji vya kule mpuguso, lusungo nakadhalikaHadi huko unapajua kaka ushirika tukuyu ndani ndani huko.....
Mwakaleli
Bila kuiona Pangani huu uzi ungekuwa fekipangani pia pako hivyo hivyo. hata hawafungi milango wanapoondoka. wanaweza kuuacha wazi.
. Sema umeandika notes ndefu lakini sijaelewa ulichokiandika zaidi ya kuita wana jf ni vilaza....Ukitaka kujua hivi sasa JF imejaa Vilaza ni jinsi walivyoamini kila ulichoandika! Wewe Nyafwili ni MUONGO, tena MUONGO WA KUTUPWA! Mfano mdogo tu, bila aibu unadai eti kwavile Kimbau alikuwa hana nyumba ikabidi amkaribishie Kikwete msikitini!! Na kuhusisha Mafia na "hata 200KM za lami...." inaonesha hata Mafia yenyewe huijui! Eti ukienda hotelini kama mgeni hupewi samaki hupewi- kheee!! Ulienda Mafia ipi wewe?! Suala la eti vijiji vingine wanadhani dini ni Uislamu tu ni uongo mwingine kwa sababu binafsi nimezunguka Mafia yote, na wilaya ndogo sana ambayo wanakijiji wake lazima wawe wamefika mjini. Na ukifika tu Kilindoni ambako ndo makao makuu ya wilaya, fasta unakutana na makanisa. Kwa mfano, enzi hizo mie bado nilikuwa Mkatoliki na kanisa letu ndo kidogo lilikuwa "kando" kidogo na mji lakini ile kuteremka tu airport umbali mfupi tu nikakutana na kanisa la KKKT. Nimeenda mbele kidogo tu, nikakutana na baa, na hapo hapo nikamla mdudu. kitu ambacho sitasahau kwenye ile baada walikuwa wanauza samaki ya kuchoma wenye ndimi; watamu ile mbaya! Sasa sijui Mafia uliyoenda wewe ni ipi!
Hivi kuna kilaza aliyekuamini suala la eti milango ya nyumba haifungwi kwa kufuli?! Hizo starehe za dunia unazosema wewe ni zipi?! Mfano mdogo tu nimekupa hapo juu kwamba ukitoka airport, ukitembea umbali mfupi tu unakutana na bar, ukitembea tena mbele kidogo unakutana na baa nyingine. Siku ya kwanza nafika tu mwenyeji wangu akanipeleka disco, sikumbuki ule ukumbi unaitwaje lakini nilikuta nyomi ambalo binafsi lilinifanya nishindwe kukaa ndani! Kwa wenyeji wa Mafia labda watakuwa wanaufahamu huu ukumbi; nadhani haupo mbali sana na maeneo ya uwanja wa ndege au mitaa ya Ismailia. Sasa starehe zipi unazosema wewe? Au kwa mji mdogo kama Kilindoni ulitarajia ukute makahaba wamejipanga barabarani kama ilivyo kwenye miji mikubwa?! Kuna starehe ipi kwa maskini ukiondoa pombe na wanawake?! Sasa ikiwa hadi baa zipo, kumbi za disko zipo! Hivi ni wapi tena unatarajia ukute wanawake zaidi ya maeneo kama hayo ambayo kwa necha yake tu pombe zipo?!
Labda posho.Na ile Magufuli alisema atawapandishia toka TZS 300,000/= ni nini???