Sasa ni Dhahiri kuwa Chadema Kinaenda kubakia Jina tu
Awali Kwa Chama hicho kusambaratika kabisa ilikuwa ni ngumu mno hata ingehamwa zaidi na zaidi,
Kwa mtego huu uliopo hata akitokea Nani kuwa M/kiti sababu M/kiti aliyepo hakuuona huo mlipuko unaokwenda Kutokea sasa, hivyo Chama hiki sasa hakina namna nyingine tena zaidi ya ushauri huu kuufanyia kazi endapo kuna mtu huko anataka kuendelea kuwa mbunge temu hii
Ni kuhama Tu, hakuna mbadala tena, kwa kuwa Upinzani uliopo sasa utakuwa si wa Chadema na CCM tena, Itakuwa ni Kati ya Chadema na vyama pinzani vyenzake, na Upinzani wa Aina hiyo ndio mbaya kuliko ule wa CCM na Upinzani
Inakuwa ni ngumu Kwa kiasi gani Kwa upande wa Chadema!!
Kwanza Vyama hivi, vimepokea wabunge Kutokea Chadema, ambao wengi Wao wamefurushwa Kwa kuonewa, ukiondoa vitabu vya Mwenyezi Mungu pekee, ndiko ambako kuna Ile usilipize Baya Kwa Baya, lkn huku kwenye siasa ni tofauti Kabisa hasa Ikitokea watu wanasaka madaraka, kuna wabunge waliotimuliwa wanahasira na Chadema ambao hawatakubali kirahisi Chadema aendelee kuwa Chama kikuu cha Upinzani, na ifahamike pia, nafasi ya Chama kikuu si Mali ya Chadema pekee
Kunahatari ya Vyama hivi kuungana na kuanza kuikomoa Chadema, na Kwa Chadema Kwa mwaka huu, ili ipate mbunge lazima ipiganie tume huru Kwanza, kiasi ambacho hivi Vyama vingine vinaweza kuamua kuikomoa Chadema Kwa kususia agenda hiyo, na Chadema akibaki peke yake na hata huko nje wanakopeleka mashitaka hayo yatapuuzwa Kwa kuwa Vyama vingine vitaonyesha kuunga mkono tume iliyopo vikidai havina Shaka na tume
Swala la Kampeni pia linaweza ni agenda za kuwaonyesha watu kuwa Chadema ni Chama kisichofaa huku Kukiwepo msukumo wa wale wabunge waliotoneshwa na Chadema Kwa kuwapiga nyundo za Maana kuonyesha ni Kwa namna gani Chadema hakifai kuungwa mkono, na hatari iliyopo inaweza Kutokea Vyama hivyo vikaamua kuungana na Campeni za CCM kuhakikisha Chadema haipati hata mbunge mmoja
Yetu macho