Wilfred Mwalusanya Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Mbozi aachiwa huru baada ya kusota rumande kwa miezi 8

Amen [emoji123]
 
Mwendazake kaumiza familia nyingi mno aisee - kama kweli hukumu ipo huko mbinguni sijui muda huu ana hali gani....

Poleni sana, siasa zetu zilikuwa zimefikia kuwa ni mateso au hata kifo.
 
Mipolisi ya Tanzania bhana!!! Yaani inashindwa kabisa kusimamia haki na majukumu yao kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi!

Badala yake inafanya kazi zao kwa kupelekeshwa na ccm! Jana inaambiwa na Rais kuhusu upuuzi wao wa kubambikia watu kesi, ikaishia tu kutoa mimacho 😳 kama vile Kabudi akiwa katika ubora wake wa kuitetea serikali ya magufuli enzi hizo!!!
 
Hakuna kitu kibaya kama kupinda haki za mtu; kwa nini,kwa sababu hata Mungu mwenye haki Huchukizwa.Mama nimemsikia akisema hataki kusikia kesi za kubambikizwa katika utawala wake.Nawaomba wasilipuuze agizo la Rais kwa sababu Mungu huchukizwa na maonevu
 

Hii taarifa rais anayo? Yaani jaji alimchagua na kumuapisha jana kuwa jaji wa mahakama kuu ameshutumiwa kumpagizia mtu makosa na Mahakama ya serikali? Nadhani kuna haja ya uteuzi wake kutenguliwa!
 
Hii taarifa rais anayo? Yaani jaji alimchagua na kumuapisha jana kuwa jaji wa mahakama kuu ameshutumiwa kumpagizia mtu makosa na Mahakama ya serikali? Nadhani kuna haja ya uteuzi wake kutenguliwa!
Uchafu wote wa Biswalo Mganga mama anaujua
 
Nimemuwaza my wife wake tu, miezi nane sio mchezo kupambana peke yako na familia, usiku baridi linakutandika...kisa dhalimu mmoja tu!
Mungu tunakushukuru tena na tena kwa kutuondolea stone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…