Will a weakened America emerge victorious against communist China?

Will a weakened America emerge victorious against communist China?

Kwangu naona US kaimarika zaidi kwenye systems zake za kidunia na kwa vile ndio muaisi wa Globalization bado anagusa kila sekta muhimu duniani na anahusika na kila kitu hata ambacho hakimuhusu. Sina rejea za wasomi ila nina sababu kama hizi:

Teknolojia zote.
US anaongoza kuwekeza kwenye tech mpya itakayoongoza dunia. Space inashindaniwa zaidi na makampuni ya Kimarekani kama SpaceX na Blue Origin. Nano technology na Artificial Intelligence bado US yuko mbele. Nchi zote zilizotawala au kuongoza dunia ziliongoza kiteknolojia, China bado.

Kwenye electronics.
Tukiachana na uzalishaji ambao umegusia hasa tuje kwenye nani anamiliki hizo teknolojia za uzalishaji. Mwaka jana US alipoiwekea Huawei vikwazo nikashangaa kuona TSMC ya Taiwan inayoongoza kwenye foundry duniani nayo imelazimika kuendana na vikwazo kwa kigezo cha kutumia core American technology. Kampuni za processors, mifumo ya kompyuta, etc nyingi zaidi ziko US au ziko modeled kwenye mfumo wa US. Huawei na Samsung ziko vile kwa sababu ya kutumia American technology, wao ndio wanaruhusu competition wakiamua wanazuia.

Utulivu wa ndani.
CCP ndio inaongoza China tangu 1940s, hawa hawajakomaa lolote kisiasa bali wanatumia intimidation na nguvu nyingi. US wamekomaa sana hata hizi issue za BLM ni utoto mbele ya utengamano wao. China ina matatizo na Taiwan na Hong Kong, haina demokrasia wala mifumo imara na inategemea uwezo wa aliyepo madarakani. Nchi isiyo na utulivu haiwezi kuwa superpower.

Usafirishaji.
Magari ya umeme bado US anaongoza ingawa kwa China kama kina Nio wanakuja kasi. Usafirishaji kwa ujumla bado US ana edge, hakuna kampuni ya China inaweza kuipindua Boeing. Pale US kuna kampuni nyingi za kijeshi zinaweza tengeneza ndege za kiraia ila China hakuna hata moja.

Energy.
US anajitosheleza kwenye energy kuliko China. Japan ilipigwa WW2 sababu mojawapo ikiwa ni kuzuiwa kusafirisha mafuta. US ina teknolojia mbadala kama fracking kwenye mafuta na ina washirika wa kuiuzia mafuta kwa uhakika. Kwenye nuclear energy bado US anaongoza tena hapo China hajaifikia Japan.

Mifumo ya fedha.
PayPal, MasterCard, VISA, etc tunajua ni za wapi. Hizo kina Alipay zinatumika ukouko China. $ inaongoza kutumiwa, haitishiwi na yeyote kwa sasa sio crypto, gold wala fedha ya nchi nyingine. Mwaka 2008 uchumi wa dunia uliyumba kwa sababu ya taasisi za Marekani, hii inamaanisha nguvu waliyonayo. China itafanya nini mpaka uchumi wa dunia utetereke? Tukiachana na magonjwa ambayo hata shit country inaweza yatoa dunia ikatetereka.

Kijeshi.
Bado China haijakaribia hata kuifikia Marekani. Bado inajaribu kumfikia Russia ila sidhani kama ni within this 20 years. US ana makumi ya bases dunia nzima, ana allies wengi sana na silaha za kutosha. China ina maadui kama India, Japan, Taiwan, Vietnam, Philippines na hata Australia.

Kimataifa.
China haijawa na ushawishi wa kuikaribia Marekani kwenye EU, Asia-Pacific wala Middle East. Huu ushawishi kwa Africa ni mdogo duniani. Mashirika ya kimataifa kama WB, IMF na UN nzima yamekaa Kimarekani zaidi.

China inaizidi Marekani mbali kwenye population. Ni soko la uhakika na nguvukazi kubwa ya uzalishaji. Pia hii idadi kubwa inatoa mchujo mzuri sana wa vipaji kukiwepo elimu stahiki. Bado hatujaona vyuo vya China vikifanya breakthrough kubwa kama zinazofanyika kwenye vyuo vya Marekani.

Sioni dalili yoyote kubwa ya China kuipiku Marekani. Dalili chache kama PPP zote ni kutokana na population ya China wala sio mbinu, uwezo wala mikakati.
Wamarekani wana tabia ya kuishusha na kuitia hofu nchi yao, sio kama Warusi wenye brags na Wachina wenye historia ya kujipa moyo. Bado US ni strong
Umeeleweka vyema Afande.
 
Bahati nzuri miaka ya juzi kati nimevutiwa kusomasoma kuhusu China hivyo nilipata mawili matatu. Hiki kitabu kimoja kilikuwa kinazungumzia mapinduzi ya AI, AI ndiko dunia inakoelekea. Unapozungumzia mapinduzi ya nne ya viwanda unazungumzia AI. Atakaye tawala AI ataishika dunia. Kwenye hii sekta US ndiyo alikuwa pioneer lakini China amecatch up na kuna uwezekano mkubwa wa kumpita US. Ili AI ifanye kazi inahitaji mabilioni ya data wanasema China kwa idadi yake ya watu na sheria zake kuhusu usiri wa data hiki ni kitu rahisi sana kwake. Kwa hiyo AI ya china ndiyo iko kwenye mazingira bora ya kustawi.

Hiki kitabu kingine (China disruptors)kinazungumzia makampuni ya China. Makampuni binafsi ndiyo huendesha uchumi wa nchi zilizoendelea. Ukiulizwa leo kati ya China na Marekani ni wapi makampuni yanapata ushindani mkubwa wa kibiashara kutoka makampuni mengine ya ndani unaweza sema US. Haiko hivyo, China kwa kila kampuni moja linalosimama kuna makampuni maelfu kadhaa yanakuwa yamekufa. China hakuna copyrights law au tuseme hazisimamiwi kihiivyo, sasa ukigundua kitu leo kesho mwenzako ameiga. Mara kakampuni kameanzishwa kameiga. Makampuni yamebuni mbinu mbalimbali, app kama we chat imebidi iwe app ya kila kitu ili kusurvive. Hizi biashara za mitandaoni, Makampuni ya China yanawekeza mtandaoni na yanajenga store(duka), yanafanya kila mbinu. Ni mazingira magumu sana kusurvive. Hilo linamaanisha nini? Linamaanisha kampuni inayoweza survive China ikitoka huku duniani hakuna wa kusimama nayo. Pia Kampuni zao zina njaa balaa, zinanunua kampuni za Marekani kama zina kichaa vile. Kitu kingine ni quality ya bidhaa, wamejifunza sana kwenye hii sekta.

Military, kwanza wanasema China hana tabia ya ubeberu(emperialism) hivyo hana haja ya kuweka mabase ya mbali na kushika sehemu za mbali. Changamoto kubwa ya kijeshi kwa China ni South China Sea na Taiwan. Hii south China Sea anagombania na mataifa mengi sana lakini wanasema kwa jinsi nchi hizi na hata Taiwan yenyewe zinavyoitegemea China kwa uchumi wao hakuna atakayethubutu kupigana au kuleta fyokofyoko japo wananunua mandege, manyambizi na kubluff. China anahakikisha wanamtegemea zaidi kiuchumi(Sun tzu anasema kumpiga adui bila kupigana ndiyo hekima kuu)

China imeendelea mpaka hapo kwa sababu ya kubadili sera zake na kuruhusu zaidi sekta binafsi kuingia kwenye uchumi. Lakini mageuzi hayo hayatoshi bado na kila siku yanafanyika ili kufanya shughuli fulani za kiuchumi zifanyike. Waandishi wanasema China bado inahitaji kufanya mapinduzi makubwa zaidi ili izidi kusonga mbele vinginevyo maajabu ya kiuchumi iliyoyapata miaka ya karibuni hayataweza kusogea mbele tena. Isipofanya mabadiliko makubwa kwenye sera zake na namna inavyoendesha mambo isahau kuipita US.

Mi nimeona nizungumzie upande wa China, ila mambo ya kuifanya Marekani ishinde au ishindwe siyaelewi vizuri, imekuwa nchi isiyotabirika, si ajabu ikatumia advantage yake(jeshi).
Asante kwa mchango wako
 
Mkuu, huo msemo unanikumbusha kauli ya msomi mmoja [Profesa] kutoka nchi Urusi aliyewahi kutabiri miaka ya 90 mwishoni kuwa itakapofika mwaka 2010, Marekani itagawanyika vipande sita na kimojawapo (Alaska) kitarejea Urusi.
Ha ha ha ha ha ha warusi hawawapendi kabisa US.
 
Kwenye hoja ya pili, service market ndio ukomavu wa biashara na uzalishaji. Ndio maana kina Apple wanauza devices ila bado wanawekeza kwenye huduma kama Apple Tv na iOS za kuendeshea hizo products. China bado inazalisha tu ila kwa kasi sana inakuja. Marekani ina patents nyingi sana zinazotumika duniani na inaendelea kusajiri nyingine. Uzalishaji wa China hata Vietnam na India wanaweza jaribu kuweka mazingira rafiki wakavuta kiasi kidogo cha uwekezaji, US ana biashara ambazo huzikuti kwingineko kirahisi. Hatujaona China ikija na conglomerates kama CocaCola, Pepsi, Microsoft, McDonald's, Nike, Ford au Boeing.

Hatuoni dunia ikikimbilia kuwekeza kwenye soko la hisa la China, Wachina wenyewe makampuni yao makubwa wanayasajiri kwenye soko la Kimarekani. Hatuoni cream za dunia zikikimbilia China, Wachina wanaenda kusoma na kufanya kazi Marekani na sio kinyume chake.

Hatuoni fedha ya China ikifanya manunuzi, hata China yenyewe haijiamini ina-devaluate Yuan yao ili kuzuia matumizi yake kwenye exchange duniani. USD inazunguka dunia nzima bila kuathiri uchumi wa US.

Hapo namba tatu kwenye jeshi. Marekani ina jeshi kubwa mno na lenye nguvu. Dunia haijalishuhudia jeshi la US likiitetea mipaka yake, huwa tunaona vita za kujitakia ambazo wakishindwa simply wanaondoka. China haina silaha za aina yoyote kutishia Marekani, ukiachana na makombora kama DF-41 vita ya China vs US hakuna Mchina atakanyaga kwenye shores za mainland US. China doctrine zake ni kuizuia US isifike Southern China sea, hata ikitaka kufikisha majeshi yake eneo kama Maryland itaanzaje? Tangu WW2 tunajua madhara ya kupigia vita kwako yalivyo, US kaingia vita zote za karne ya 20 na 21 bila kupigana nyumbani.

Hizi Norinco na Shenyang haziwezi tengeneza silaha za kuzishinda Raytheon, General Dynamics, Boeing, Lockheed Martin, Huntington Ingalls, Northrop Grumman na nyingine nyingi za US.

China hakuna derivative ya DARPA yenye miradi mikubwa ya kimapinduzi kwenye ulinzi. Elimu ya China nayo sio supportive sana kwenye ulinzi kama US. Hata uuzaji wa silaha US anaongoza kuwauzia superpowers ila China bado ananunua silaha muhimu kwa Russia. China anauza silaha kwa kina Nigeria, Pakistan, Sri Lanka ambao wanakwepa masharti na kutafuta bei nafuu ila hawana budget ya kuchukua kwa wingi.

Bila hata allies US vs China lazima China isiishinde US kimapigano. US inaweza shinda au kutoka suruhu ila sio kushindwa. Kwanza experience aliyonayo US ni kubwa mno na yuko kila mahala duniani.

Kwenye ujasusi, cyber warfare na cyber security bado US anamzidi China. Hapa China hajaifikia Israel au Russia.

Tukiachana na ulinzi ambao ni muhimu kuhakikisha usalama wa biashara zote za nchi na ustawi wa sera zake. Maendeleo yajayo tumekubaliana yanatokana na nani anafanya nini na anamiliki nini kwa sasa katika teknolojia.

China ina kina Huawei, ZTE na CSMC ambao hawajazishinda Intel, AMD au Apple.

Kampuni kubwa za magari duniani haziko China. Hata kampuni za EV zinazoibuka US inaongoza ila China iko karibu sana.
5G China anaongoza ila wapo kina Ericsson na Nokia walikuwa wanakuja (hawana fedha). Ikumbukwe Nokia na Ericsson waliitoa 4G, Japan walishatoa 3G kupitia Docomo. Leo hii wako wapi?
Tutakuja kupata 6G wakitokea watu ambitious kama Elon Musk.

Artificial Intelligence na robotics wapo US, Japan na Russia wanakuja vizuri. Tumeona baadhi ya demo za robots kutoka US na Russia ila hatujaona demo za China. AI iko integrated sana kwenye teknolojia za magari kama Tesla na kwenye smartphone. Kwenye AI kompyuta na robots zitafidia watu na uzalishaji utapungua gharama uku kasi ikiwa ileils hakuna likizo wala kuchoka. China sioni kama anaongoza hapa, atategemea idadi yake ya watu na gharama zake ndogo za uzalishaji.

Nilitazama production site ya F-35, wanatumia laser beam kuelekeza mfanyakazi wapi pa kufunga nati, wapi pa kuchomeka hiki. China hana precision hii kwenye uzalishaji na hivo faults kwenye systems muhimu kama kompyuta hazikwepeki wakati huo speed ya kuzalisha hana ila atategemea wingi wa watu.

Teknolojia nyingine za zamani kidogo kwa US bado China hajazifikia. China hana true stealth technology ambayo US anayo tangu 1980s, hana uwezo wa kutengeneza injini za ndege kama P&W pale US, aircraft carrier ndio anayo moja ya kwake ikiwa diesel powered wakati US anazo zaidi ya kumi nuclear powered, nuclear submarines bado sana. Yani nuclear technology bado hajafikia US, mpaka majuzi hapa China ilikuwa inatumia coal wakati wenzake walishahama muda sana uko.

Katika ustaarabu na kutegemeana kwa mifumo na taasisi China haijaongoza. Benki, mashirika ya bima, mifuko ya uwekezaji popote duniani na taasisi zinazojitegemea viko zaidi wazi na endelevu kwa US. Utasikia FDA imezuia Monsanto kuuza dawa flani, FAA imezi-ground Boeing Max mpaka izichunguze, FBI imechunguza Russiagate na kukuta rais Trump hana hatia. Ingekuwa China ungesikia CPP wamefanya hivi, serikali imefanya kile, serikali ime...
Nchi haina hata mgawanyo wa mamlaka itaanzaje kuongoza ulimwengu.

Naamini ili nchi iipite Marekani lazima kwanza iifikie, hata Britain kabla haijapitwa na Marekani kwanza zililingana kisha Marekani akaipita. Sasa China hajaweza kulingana na Marekani, hayuko mzimamzima kuna vitu yuko mbele vingine nyuma kabisa uko
Nakusoma mkuu
 
Uko sahihi kabisa lakini kitu kimoja ambacho nadhani unasahau kukisema kwa hayo mataifa yote ambayo yaliwahi kulinganishwa na Marekani: Ujerumani Magharibi, Umoja wa Kisovieti na Japan hazijawahi kuwa na uchumi mkubwa kuliko Marekani wala kumshinda nguvu ya soko. Umoja wa kisovieti katika ubora wake miaka ya 60's ilikuwa ni asilimia 30 hadi 40 ya GDP ya Marekani. Marekani alikuwa bora katika GDP, PPP na muuzaji mkubwa wa bidhaa na huduma.

Sasa tukichambua uchumi na historia, Marekani alikuwa taifa lenye nguvu duniani kiuchumi mwaka 1872 baada ya kuwa na PPP kubwa kuliko mataifa yote duniani. Hadi kufika mwaka 1900 PPP ikamuwezesha Marekani kuwa taifa lenye uchumi imara kuliko yote. Mwaka 2009 Uchina ndiyo likawa taifa lenye PPP kubwa kuliko Marekani, sasa nadhani tukizungumza Uchumi, PPP huleta faida kibao kwa taifa lolote duniani lile linalofuata mfumo wa soko huru.

Kingine ni kwamba Japan, USSR na Ujerumani Magharibi hayajawahi kuwa The Biggest Exporters of Merchandise hadi kuweza kumtishia Marekani. Mataifa ambayo yamewahi kushika hii nafasi ni Imperial Germany mwaka 1900 na Dola la Muingereza kabla ya 1900. Taifa linalokuwa tajiri kuliko yote duniani ni lile ambalo linauza bidhaa nyingi pamoja na huduma kuliko taifa jingine lolote lile duniani, Marekani imeshika nafasi hii tokea mwaka 1945. Mwaka 2014 IMF ikatangaza kwamba Uchina ndiyo The Greatest Exporter of Merchandise. Marekani amefika hapo alipo kwasababu ya soko lililojengwa kuanzia kipindi cha The Gilded Age na World Wars.

Nafurahi sana kwamba umewalete wakina Huntington na Hoffman: Sasa kama umesoma vizuri, matatizo haya yalianza na Charles De Gaulle baada ya Marekani kuachana na The Gold Standard na kuanza kutumia Fiat Money. Watu kama Charles De Gaulle wakasema kwamba Marekani imefilisika na utajiri wake wote umeisha: Wakina Huntington walifanya chambuzi wakizingatia hili.

Ukweli mchungu ni kwamba Marekani imefika miaka ya 80 ikiwa na hali mbaya sana kiuchumi na Ronald Raegan alikopa sana pesa kutoka taasisi za ndani na nchi za nje. Swali lao hawa wasomi wote ni hili: Siku mataifa makubwa yanaacha kutumia dollar (The Fiat Money) unadhani Marekani itapona ??? Swali hili halijatolewa majibu mpaka leo.

Hoja kubwa ya Graham T Allison, Kishore Mahbubani na Joseph Nye siyo The Decline of America kama wakina Huntington wanavyosema kwenye The Clash of Civilization, but rather The Relative Decline of America. Marekani anaweza kuwa na uchumi huu-huu ambao anao sasa lakini Uchina akiendelea kukua kwa kasi hii basi atakuwa na uchumi mkubwa mara mbili ya Marekani hadi kufika 2070. Suala zima la Relative Decline halikuguswa kabisa na Huntington wala Hoffman, kama kuna sehemu wamelizungumzia tuoneshane.

Ahsante sana.
We jamaa upo kimya mno.

Backbencha tunakusikilizia uteme madin tufanye yetu
 
Kwangu naona US kaimarika zaidi kwenye systems zake za kidunia na kwa vile ndio muaisi wa Globalization bado anagusa kila sekta muhimu duniani na anahusika na kila kitu hata ambacho hakimuhusu. Sina rejea za wasomi ila nina sababu kama hizi:

Teknolojia zote.
US anaongoza kuwekeza kwenye tech mpya itakayoongoza dunia. Space inashindaniwa zaidi na makampuni ya Kimarekani kama SpaceX na Blue Origin. Nano technology na Artificial Intelligence bado US yuko mbele. Nchi zote zilizotawala au kuongoza dunia ziliongoza kiteknolojia, China bado.

Kwenye electronics.
Tukiachana na uzalishaji ambao umegusia hasa tuje kwenye nani anamiliki hizo teknolojia za uzalishaji. Mwaka jana US alipoiwekea Huawei vikwazo nikashangaa kuona TSMC ya Taiwan inayoongoza kwenye foundry duniani nayo imelazimika kuendana na vikwazo kwa kigezo cha kutumia core American technology. Kampuni za processors, mifumo ya kompyuta, etc nyingi zaidi ziko US au ziko modeled kwenye mfumo wa US. Huawei na Samsung ziko vile kwa sababu ya kutumia American technology, wao ndio wanaruhusu competition wakiamua wanazuia.

Utulivu wa ndani.
CCP ndio inaongoza China tangu 1940s, hawa hawajakomaa lolote kisiasa bali wanatumia intimidation na nguvu nyingi. US wamekomaa sana hata hizi issue za BLM ni utoto mbele ya utengamano wao. China ina matatizo na Taiwan na Hong Kong, haina demokrasia wala mifumo imara na inategemea uwezo wa aliyepo madarakani. Nchi isiyo na utulivu haiwezi kuwa superpower.

Usafirishaji.
Magari ya umeme bado US anaongoza ingawa kwa China kama kina Nio wanakuja kasi. Usafirishaji kwa ujumla bado US ana edge, hakuna kampuni ya China inaweza kuipindua Boeing. Pale US kuna kampuni nyingi za kijeshi zinaweza tengeneza ndege za kiraia ila China hakuna hata moja.

Energy.
US anajitosheleza kwenye energy kuliko China. Japan ilipigwa WW2 sababu mojawapo ikiwa ni kuzuiwa kusafirisha mafuta. US ina teknolojia mbadala kama fracking kwenye mafuta na ina washirika wa kuiuzia mafuta kwa uhakika. Kwenye nuclear energy bado US anaongoza tena hapo China hajaifikia Japan.

Mifumo ya fedha.
PayPal, MasterCard, VISA, etc tunajua ni za wapi. Hizo kina Alipay zinatumika ukouko China. $ inaongoza kutumiwa, haitishiwi na yeyote kwa sasa sio crypto, gold wala fedha ya nchi nyingine. Mwaka 2008 uchumi wa dunia uliyumba kwa sababu ya taasisi za Marekani, hii inamaanisha nguvu waliyonayo. China itafanya nini mpaka uchumi wa dunia utetereke? Tukiachana na magonjwa ambayo hata shit country inaweza yatoa dunia ikatetereka.

Kijeshi.
Bado China haijakaribia hata kuifikia Marekani. Bado inajaribu kumfikia Russia ila sidhani kama ni within this 20 years. US ana makumi ya bases dunia nzima, ana allies wengi sana na silaha za kutosha. China ina maadui kama India, Japan, Taiwan, Vietnam, Philippines na hata Australia.

Kimataifa.
China haijawa na ushawishi wa kuikaribia Marekani kwenye EU, Asia-Pacific wala Middle East. Huu ushawishi kwa Africa ni mdogo duniani. Mashirika ya kimataifa kama WB, IMF na UN nzima yamekaa Kimarekani zaidi.

China inaizidi Marekani mbali kwenye population. Ni soko la uhakika na nguvukazi kubwa ya uzalishaji. Pia hii idadi kubwa inatoa mchujo mzuri sana wa vipaji kukiwepo elimu stahiki. Bado hatujaona vyuo vya China vikifanya breakthrough kubwa kama zinazofanyika kwenye vyuo vya Marekani.

Sioni dalili yoyote kubwa ya China kuipiku Marekani. Dalili chache kama PPP zote ni kutokana na population ya China wala sio mbinu, uwezo wala mikakati.
Wamarekani wana tabia ya kuishusha na kuitia hofu nchi yao, sio kama Warusi wenye brags na Wachina wenye historia ya kujipa moyo. Bado US ni strong
Ni zaidi ya mwaka na miezi mitano sasa, assessment yangu hii inabaki vilevile. Russia wana bragging ila uwezo wa kawaida, tunawaona pale Ukraine. China wana mikwara na kujipa moyo, tumewaona jana na leo pale Taiwan.

Ninachobadilisha hapa ni makadirio yangu yasiyo sahihi kwamba China ingetumia miaka kama 20 kuizidi Russia kijeshi. Huo muda ni mwingi sana, Russia ilikuwa overestimated mno na China imepiga hatua kadhaa kijeshi mfano uzinduzi wa Type 003 aircraft carrier mwezi jana ambayo ilijengwa kwa kasi. Pia nimeiona Type 005 destroyer. Kwa sasa naamini kwa speed hii ya China hatuhitaji miaka zaidi ya 10 ili China iizidi Russia kijeshi. Hapo nimekwishazingatia vitu vingi sana baina ya Russia yenyewe, mfano quality of production na sanctions kwenye technology
 
Una yafahamu masuala ya kijeshi na ulinzi ya mataifa mbalimbali kwa upana zaidi ?
 
Utulivu wa ndani.
CCP ndio inaongoza China tangu 1940s, hawa hawajakomaa lolote kisiasa bali wanatumia intimidation na nguvu nyingi.
Ki vipi CPC hawaja komaa kisiasa ? Na ni nguvu zipi CPC wana tumia ?
 
Huawei na Samsung ziko vile kwa sababu ya kutumia American technology,
Huawei ipo vile ilivyo kutokana na kuwa backed by China government na hii ni kwa makampuni yote ya wazawa ya China.
 
China ina matatizo na Taiwan na Hong Kong, haina demokrasia wala mifumo imara na inategemea uwezo wa aliyepo madarakani. Nchi isiyo na utulivu haiwezi kuwa superpower.
Una ufahamu mfumo wa utawala wa China na siasa zake ?
Demokrasia ni nini ?
Ni utulivu upi China ilio kosa ?

Taiwan, Hongkong zote ni China moja.
 
Usafirishaji.
Magari ya umeme bado US anaongoza ingawa kwa China kama kina Nio wanakuja kasi. Usafirishaji kwa ujumla bado US ana edge, hakuna kampuni ya China inaweza kuipindua Boeing. Pale US kuna kampuni nyingi za kijeshi zinaweza tengeneza ndege za kiraia ila China hakuna hata moja.
Mambo yame badilika pakubwa sana, fuatilia.
 
Energy.
US anajitosheleza kwenye energy kuliko China. Japan ilipigwa WW2 sababu mojawapo ikiwa ni kuzuiwa kusafirisha mafuta. US ina teknolojia mbadala kama fracking kwenye mafuta na ina washirika wa kuiuzia mafuta kwa uhakika. Kwenye nuclear energy bado US anaongoza tena hapo China hajaifikia Japan.
Fuatilia, mambo yame badilika sana.
 
Mwaka 2008 uchumi wa dunia uliyumba kwa sababu ya taasisi za Marekani, hii inamaanisha nguvu waliyonayo. China itafanya nini mpaka uchumi wa dunia utetereke? Tukiachana na magonjwa ambayo hata shit country inaweza yatoa dunia ikatetereka.
Ume fuatilia ripoti ya mkurugenzi wa IMF kuhusu madhara ya kiuchumi kwa dunia kutokana na nchi ya China kuwa katika lockdown ya uviko19 kwa miaka mitatu mfululizo kabla haija ondolewa mwisho wa mwaka jana na makadirio ya ukuaji wa uchumi wa dunia baada ya kuondolewa kwa lockdown hiyo ?.
 
Kijeshi.
Bado China haijakaribia hata kuifikia Marekani. Bado inajaribu kumfikia Russia ila sidhani kama ni within this 20 years. US ana makumi ya bases dunia nzima, ana allies wengi sana na silaha za kutosha. China ina maadui kama India, Japan, Taiwan, Vietnam, Philippines na hata Australia.
Ukubwa wa nchi kijeshi unapimwa katika nini ?
 
Kimataifa.
China haijawa na ushawishi wa kuikaribia Marekani kwenye EU, Asia-Pacific wala Middle East. Huu ushawishi kwa Africa ni mdogo duniani. Mashirika ya kimataifa kama WB, IMF na UN nzima yamekaa Kimarekani zaidi.
Sio kweli
 
Sioni dalili yoyote kubwa ya China kuipiku Marekani. Dalili chache kama PPP zote ni kutokana na population ya China wala sio mbinu, uwezo wala mikakati.
Mbinu gani ?, Uwezo gani ? Mikakati ipi ?
 
Wamarekani wana tabia ya kuishusha na kuitia hofu nchi yao, sio kama Warusi wenye brags na Wachina wenye historia ya kujipa moyo. Bado US ni strong
Kwani ni masimango ya wa marekani kwa nchi yao au ni ripoti mbalimbali za kitaalamu ndizo zina ongea ?
 
Back
Top Bottom