Ukiniwekea andiko la Huntington ambalo limezungumzia The Decline of America kabla ya hilo la kutoka Foreign Policy. Tena la miaka ya 50 kama ulivyosema mwanzoni ntakushukuru sana.
Vipimo vikubwa vya uchumi ni PPP, GNP na GDP. Kinachoaminika na taasisi kubwa za kimataifa kama IMF ni PPP.
GNP wamarekani wameacha kukitumia kwasababu kina madhaifu.
Kwani ili tuweze kokotoa PPP na kufanya ulinganifu wa Country's Output tunazingatia vigezo gani ???
Pia, ukiangalia The Big Mac Index 2020 ya PPP, Nigeria na Iraq zimezipita nchi kama Sweden na Norway kweli ???
Turudi kidogo kwa Adam Smith kidogo, taifa ambalo linauza sana bidhaa kuliko mataifa mengine kwenye soko la dunia ndiyo litakuwa na mirija mingi ya kufyonza pesa kutoka mataifa mengi duniani, hivyo ndilo ambalo litakuwa ni tajiri. Marekani amekuwa taifa kubwa kiuchumi duniani kwasababu ndiye aliyekuwa muuzaji mkuba wa bidhaa kwenye soko la dunia. Hili nalo lina ubishi ???
Tuachane na mikisio na tufanye rejea ya takwimu kutoka taasisi kubwa za kiuchumi duniani kama IMF. Wao wamesema kabisa kwamba kipimo bora na kinachoaminika na wao ni PPP kuliko GDP kwasababu GDP inategemea Market Rates which are not stable for a long time and only relevant to internationally traded goods. Non-traded goods are left out of the periphery. Unadhani ni sahihi kusema Marekani ina Uchumi mkubwa kuliko Uchina kwa kuzingatia Market Rates peke yake mkuu ???
Hebu tuache makisio ya wanazuoni na twende kwenye takwimu maana zile huwa hazidanganyi. IMF wanasema PPP ndiyo kikokotoo bora kabisa cha uchumi kuliko GDP kwasababu kinazingatia mambo mengi. Lakini nadhani itakuwa vizuri zaidi kama tusaidie kufahamu kwanza jinsi ambavyo PPP inakokotolewa halafu tufanye rejea ya The Big Max Index 2020 kisha mwisho kabisa turudi kwenye takwimu za IMF na WB.
NB: Maswala ya kisera na kidiplomasia ni muhimu lakini ni Subjective sana katika kuangalia mwenendo wa Uchumi wa nchi. Kuna nchi ambazo hazifanyi vizuri kidiplomasia, haki za binadamu na kisera lakini zinafanya vizuri kwenye soko la dunia. Au hapa ulikuwa unamaanisha nini mkuu ???
Karibu tuendeleze mjadala......
Kwanza kabisa, nimeshangazwa na ombi lako kuhusu andiko la Huntington la miaka ya 50 ambalo limezungumzia "decline of America". Nimeshangazwa kwa sababu sijapata kufahamu sababu juu ya ombi hilo. Je, ni kwa sababu hautaki kukubaliana na hoja yangu kwamba mjadala huu na mingine ya namna hii imekwisha jadiliwa toka miaka ya 50 ama ni kwa sababu nyingine tofauti?
Huntington, kwa maneno yake mwenyewe na katika maandiko na machapisho yake (kama umemfuatilia kwa makini) ameeleza kuhusu chimbuko la huo mjadala wa "decline of America". Kama umemfuatilia kwa makini, amezungumza kwamba alikuwa akiufuatilia huo mjadala tangu miaka ya 50 mwishoni na aliushuhudia huo mjadala ukishamiri katika vipindi tofauti-tofauti ama kwa lugha nyingine "waves". Wave ya kwanza ni kipindi ambacho USSR ilifanikiwa kurusha satellite ya Sputnik 1 mwaka 1957. Mafanikio ya USSR ya Sputnik 1 yaliamsha mjadala kwamba Marekani inaelekea kwenye "decline" na kwamba tayari kuna uwezekano kuwa imekwisha achwa nyuma na USSR katika masuala mbalimbali ambayo yamekuwa yakiiwezesha Marekani kuwa taifa lenye nguvu zaidi duniani. Hiyo ni miaka ya 50 mwishoni.
Kipindi kingine maarufu kilicho shamirisha mjadala huo ni miaka ya 70 mwishoni. Mafanikio ya kiuchumi ya Japan yalipelekea kuamsha mjadala wa namna hiyohiyo nchini Marekani kwamba uchumi wa Marekani inakabiliwa na tishio la ukuaji na Japan inakaribia kuizidi Marekani na huenda imekwisha izidi katika masuala mbalimbali muhimu ya kiuchumi. Pia, ukisoma machapisho ya karne hii ama ya hivi karibuni kuhusiana na hoja hii ya "decline of America", wasomi mbalimbali wanadai kuwa Marekani ipo katika "wave ya 5 ya declinism", na wanafuatisha trend ileile ya kina Huntington ya kuanzia miaka ya 50 mwishoni kuanzia USSR na Sputnik 1, kuelekea Vietnam war, kisha Japan, Ulaya na mpaka hivi sasa, China.
Tuendelee na mjadala!
Umetoa hoja kwamba tuachane na makisio na tuzitumie data zilizopo. Kwanza kabisa, hizo data unazozisema ndizo ambazo zimekuwa zikitumika kufanya makadirio au makisio mbalimbali ya kiuchumi ambayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara. Wataalamu wa masuala ya kiuchumi hutoa makadirio ya ukuaji wa uchumi kwa kuhusisha taarifa mbalimbali zilizopo za kiuchumi kutoka katika mashirika mbalimbali hususani haya tunayoyafahamu sana. Kuna taarifa kuhusu mapato ya nchi na uzalishaji katika kipindi cha muda maalumu, mapato ya raia kutokana na mapato ya nchi zao (per capita income), taarifa za ukuaji wa kiuchumi (GDP growth), na masuala mengineyo.
Hebu sasa tuangazie hizo data za kiuchumi. Nitauzungumzia uchumi wa Marekani kwa data za kiuchumi za hivi sasa ili ku-justify hoja yangu ya awali kuwa China bado haijaizidi Marekani kiuchumi. Fuatana nami!
1) Nominal GDP. Pato la taifa kwa mwaka. Mashirika mbalimbali duniani hasa yale tunayoyafahamu kama vile IMF, World Bank pamoja na UN yanatuambia kwamba, Marekani ni nchi yenye uchumi mkubwa zaidi duniani kwa kipimo cha nominal GDP ikifuatiwa na China. Kuna haja ya kuziweka takwimu hapa?
2) Net wealth ama national net worth. Thamani ya mali zote za nchi ukitoa madeni (assets minus liabilities), ikiwemo thamani ya mali zinazomilikiwa na raia wote kwa ujumla. Marekani ni kinara katika hili pia kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kiuchumi.
3) GDP per capita. Pato la raia kutokana na pato la taifa zima kwa mwaka. Marekani inafanya vizuri zaidi hapa ukiilinganisha na China. Kulingana na data za hivi karibuni za kina IMF, WB na wenzake, Marekani imeorodheshwa katika nafasi kumi za juu ikishindana na nchi za Scandinavia, Luxembourg, Qatar n.k.
4) GDP per capita (PPP). Pato la raia katika kipimo cha Purchasing Power Parity kutokana na thamani ya bidhaa zote na huduma zinazozalishwa kwa mwaka. Pia, Marekani inafanya vizuri zaidi kuliko China kulingana na data zilizopo za hivi karibuni.
Sambamba na masuala hayo, kuna vipimo vingine ambavyo hutumiwa na wataalamu wa masuala ya uchumi kuonesha uwezo wa kiuchumi wa nchi kwa kuzingatia masuala mbalimbali muhimu. Kuna vipimo vya uchumi kama vile: Ease of Doing Business Index, Indices of Economic Freedom, Global Competitiveness Index n.k.
Ease of Doing Business Index. Hutumika kuonesha, pia kulinganisha nchi zenye urahisi katika kufanya shughuli za kiuchumi ama kibiashara. Hapa kuna masuala ya masharti rafiki ama rahisi ya kibiashara, ulinzi madhubuti na usalama wa mali, hakimiliki ama property rights hususani intellectual property n.k. Kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni, Marekani inatajwa miongoni mwa nchi zenye urahisi zaidi duniani katika kufanya biashara ikishindana na nchi kama vile Korea Kusini, Denmark, Singapore n.k.
Pia, kuna kipimo kingine kinachofahamika kama Global Competitiveness Index.
Watafiti wa masuala ya kiuchumi huangalia uwezo wa nchi kuweza kuufanya uchumi wake uwe na ustawi kwa jinsi ambavyo nchi hiyo inavyoweza kuzitumia ama inavyozitumia rasilimali ilizonazo.
Hapa kuna masuala kadhaa muhimu sana katika ukuaji na ustawi wa uchumi ambayo huangaliwa ama huzingatiwa:
a) Institutions ama taasisi za umma na zile za binafsi ambazo ni well-functioning.
b) Elimu bora (primary & higher education).
c) Afya bora.
d) Miundombinu mahususi.
e) Market size. Ukubwa wa soko la nje na lile la ndani.
f) Innovation. Uwezo katika uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia.
g) Matumizi ya teknolojia zilizopo na mbinu za kisasa katika uzalishaji. Na kadhalika!
Marekani inafanya vizuri katika hili pia kuliko China. Kwenye ripoti kadhaa za GCI hasa za miaka ya hivi karibuni za World Economic Forum, Marekani imekuwa ikitajwa katika nafasi bora na za juu (ya kwanza ama ya pili) ikishindana na nchi za Scandinavia pia na nchi kama vile Singapore.
Marekani inafanya vizuri kuliko China katika studies nyinginezo muhimu kama vile Global Innovation Index (capacity for, and success in innovation) pia hata katika HDI yaani Human Development Index. Katika HDI kuna masuala kadha wa kadha ambayo huzingatiwa ikiwemo life expectancy ya watu, literacy rate n.k.
Kuna hoja umeiwasilisha kuhusiana na Purchasing Power Parity kwamba ni kipimo "kinachoaminika zaidi kuliko GDP", hapa nafikiri unamaanisha nominal GDP. Nafikiri hoja yako hapa haiko sawa!
Iko hivi,
Kila kipimo cha uchumi kinachotumika na mashirika makubwa kama vile IMF, World Bank na UN kina mipaka yake ya matumizi ama limitations. Wataalamu wa masuala ya uchumi kwa ujumla wanaposema kuwa kipimo fulani ni bora kuliko kingine, ni katika kuzingatia baadhi ya masuala pekee. Kuhusu PPP, ni kipimo kizuri hasa pale unapolinganisha bei ya bidhaa kati ya nchi moja na nyingine kulingana na masoko ya nchi hizo lakini kina mapungufu yake mengi ambayo kwayo hakiwezi kusimama kama kipimo pekee sahihi cha uchumi. Hivi sasa kuna mjadala mkubwa sana kuhusiana na hicho kipimo na baadhi ya vipimo vingine hali ambayo itapelekea wataalamu kuja na vipimio vipya hapo baadaye.
Wataalamu wa masuala ya uchumi wanaeleza kuwa, comparisons kwa kutumia kipimo cha Purchasing Power Parity are more useful than those using nominal GDP. Lakini, Purchasing Power Parity is limited when measuring financial flows kati ya mataifa mbalimbali. Pia huleta shida katika kulinganisha ubora wa bidhaa zinazofanana kati ya mataifa mbalimbali (kuna mfano nimeutoa katika post yangu iliyopita wakati nikijibu hoja ya mchangiaji fulani). Purchasing Power Parity pia inahitaji makisio zaidi ama estimations katika mahesabu yake kuliko nominal GDP. Yote hayo ni kwa mujibu wa IMF. Kwa logic ya kawaida tu, kipimo kinachohitaji makisio zaidi kuliko kipimo kingine sidhani kama kinaweza kusimama pekee kama kipimo bora zaidi ama cha kuaminiwa zaidi kuliko vipimo vingine vyote na katika masuala yote muhimu.
Asante!