Kwenye hoja ya pili, service market ndio ukomavu wa biashara na uzalishaji. Ndio maana kina Apple wanauza devices ila bado wanawekeza kwenye huduma kama Apple Tv na iOS za kuendeshea hizo products. China bado inazalisha tu ila kwa kasi sana inakuja. Marekani ina patents nyingi sana zinazotumika duniani na inaendelea kusajiri nyingine. Uzalishaji wa China hata Vietnam na India wanaweza jaribu kuweka mazingira rafiki wakavuta kiasi kidogo cha uwekezaji, US ana biashara ambazo huzikuti kwingineko kirahisi. Hatujaona China ikija na conglomerates kama CocaCola, Pepsi, Microsoft, McDonald's, Nike, Ford au Boeing.
Hatuoni dunia ikikimbilia kuwekeza kwenye soko la hisa la China, Wachina wenyewe makampuni yao makubwa wanayasajiri kwenye soko la Kimarekani. Hatuoni cream za dunia zikikimbilia China, Wachina wanaenda kusoma na kufanya kazi Marekani na sio kinyume chake.
Hatuoni fedha ya China ikifanya manunuzi, hata China yenyewe haijiamini ina-devaluate Yuan yao ili kuzuia matumizi yake kwenye exchange duniani. USD inazunguka dunia nzima bila kuathiri uchumi wa US.
Hapo namba tatu kwenye jeshi. Marekani ina jeshi kubwa mno na lenye nguvu. Dunia haijalishuhudia jeshi la US likiitetea mipaka yake, huwa tunaona vita za kujitakia ambazo wakishindwa simply wanaondoka. China haina silaha za aina yoyote kutishia Marekani, ukiachana na makombora kama DF-41 vita ya China vs US hakuna Mchina atakanyaga kwenye shores za mainland US. China doctrine zake ni kuizuia US isifike Southern China sea, hata ikitaka kufikisha majeshi yake eneo kama Maryland itaanzaje? Tangu WW2 tunajua madhara ya kupigia vita kwako yalivyo, US kaingia vita zote za karne ya 20 na 21 bila kupigana nyumbani.
Hizi Norinco na Shenyang haziwezi tengeneza silaha za kuzishinda Raytheon, General Dynamics, Boeing, Lockheed Martin, Huntington Ingalls, Northrop Grumman na nyingine nyingi za US.
China hakuna derivative ya DARPA yenye miradi mikubwa ya kimapinduzi kwenye ulinzi. Elimu ya China nayo sio supportive sana kwenye ulinzi kama US. Hata uuzaji wa silaha US anaongoza kuwauzia superpowers ila China bado ananunua silaha muhimu kwa Russia. China anauza silaha kwa kina Nigeria, Pakistan, Sri Lanka ambao wanakwepa masharti na kutafuta bei nafuu ila hawana budget ya kuchukua kwa wingi.
Bila hata allies US vs China lazima China isiishinde US kimapigano. US inaweza shinda au kutoka suruhu ila sio kushindwa. Kwanza experience aliyonayo US ni kubwa mno na yuko kila mahala duniani.
Kwenye ujasusi, cyber warfare na cyber security bado US anamzidi China. Hapa China hajaifikia Israel au Russia.
Tukiachana na ulinzi ambao ni muhimu kuhakikisha usalama wa biashara zote za nchi na ustawi wa sera zake. Maendeleo yajayo tumekubaliana yanatokana na nani anafanya nini na anamiliki nini kwa sasa katika teknolojia.
China ina kina Huawei, ZTE na CSMC ambao hawajazishinda Intel, AMD au Apple.
Kampuni kubwa za magari duniani haziko China. Hata kampuni za EV zinazoibuka US inaongoza ila China iko karibu sana.
5G China anaongoza ila wapo kina Ericsson na Nokia walikuwa wanakuja (hawana fedha). Ikumbukwe Nokia na Ericsson waliitoa 4G, Japan walishatoa 3G kupitia Docomo. Leo hii wako wapi?
Tutakuja kupata 6G wakitokea watu ambitious kama Elon Musk.
Artificial Intelligence na robotics wapo US, Japan na Russia wanakuja vizuri. Tumeona baadhi ya demo za robots kutoka US na Russia ila hatujaona demo za China. AI iko integrated sana kwenye teknolojia za magari kama Tesla na kwenye smartphone. Kwenye AI kompyuta na robots zitafidia watu na uzalishaji utapungua gharama uku kasi ikiwa ileils hakuna likizo wala kuchoka. China sioni kama anaongoza hapa, atategemea idadi yake ya watu na gharama zake ndogo za uzalishaji.
Nilitazama production site ya F-35, wanatumia laser beam kuelekeza mfanyakazi wapi pa kufunga nati, wapi pa kuchomeka hiki. China hana precision hii kwenye uzalishaji na hivo faults kwenye systems muhimu kama kompyuta hazikwepeki wakati huo speed ya kuzalisha hana ila atategemea wingi wa watu.
Teknolojia nyingine za zamani kidogo kwa US bado China hajazifikia. China hana true stealth technology ambayo US anayo tangu 1980s, hana uwezo wa kutengeneza injini za ndege kama P&W pale US, aircraft carrier ndio anayo moja ya kwake ikiwa diesel powered wakati US anazo zaidi ya kumi nuclear powered, nuclear submarines bado sana. Yani nuclear technology bado hajafikia US, mpaka majuzi hapa China ilikuwa inatumia coal wakati wenzake walishahama muda sana uko.
Katika ustaarabu na kutegemeana kwa mifumo na taasisi China haijaongoza. Benki, mashirika ya bima, mifuko ya uwekezaji popote duniani na taasisi zinazojitegemea viko zaidi wazi na endelevu kwa US. Utasikia FDA imezuia Monsanto kuuza dawa flani, FAA imezi-ground Boeing Max mpaka izichunguze, FBI imechunguza Russiagate na kukuta rais Trump hana hatia. Ingekuwa China ungesikia CPP wamefanya hivi, serikali imefanya kile, serikali ime...
Nchi haina hata mgawanyo wa mamlaka itaanzaje kuongoza ulimwengu.
Naamini ili nchi iipite Marekani lazima kwanza iifikie, hata Britain kabla haijapitwa na Marekani kwanza zililingana kisha Marekani akaipita. Sasa China hajaweza kulingana na Marekani, hayuko mzimamzima kuna vitu yuko mbele vingine nyuma kabisa uko