TANZIA William Malecela (Le Mutuz) afariki Dunia

TANZIA William Malecela (Le Mutuz) afariki Dunia

Ivi kwani alikuwa anaumwa ama? Mbona ghafla Sana ivo🤔🤔
Alikuwa na shida ya moyo kizuti chake kila kitu alikuwa akikiweka wazi nenda kwenye page yake insta hakuna kitu kinachohusu maisha yake/ familiya na afya kila kitu alikuwa akikiweka wazi. Aliweka tangu alivyoanza kuumwa matibabu na kila step aliweka wazi. Picha zipo kwa page yake.
 
watoto wa Mzee Malecela waliotangulia “mbele za haki” ni:
1). Senyagwa Malecela
2). Dkt. Irene Malecela
3). Mkwavi Ipyana Malecela
4). Dkt. Mwele Malecela, na
5). William Malecela (Le Mutuz) duniani kuna watu wanapitia magumu sana.
Wamebaki wangapi sahivi, yaan walio wazima??
 
75% ya JamiiForums Members walikuwa wakisema GENTAMYCINE ndiyo Marehemu hivyo pengine kuanzia leo Watabadilika au waendelee Kuamini kuwa Mimi ni Yeye hivyo hata hii Post naiandika nikiwa Frijini Mortuary ya Muhimbili National Hospital ( Wadi #26 ) nilikohifadhiwa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Le Mutuz huwezi fahamu kuwa ni mtoto wa mkubwa yaani mzee marehemu John Malecela alikuwa ni mmoja wa viongozi ambao wana vijana walo "humble" sana si wa kujikweza.

Sheikh lini tena Mzee John Samuel Malecela ametutoka ?

Tuwe makini tusilete taharuki kwa kuandika taarifa nzito zisizo sahihi kisa unahisi fulani atakuwa marehemu au amekumbana na kadhia fulani
 
Kama umesoma ile Historia ya maisha
yake utagundua hata hao ndugu zake nao hawafai hata kidogo alikuwa ktk vita nao.
ndugu aliokuwa katika vita nao ni watoto wa ndoa wa malecela. hao hadi kesho wana vita naye akiwa kaburini. kama alikuwa na vita hadi na watoto wa mama yake kule mbeya/tunduma, basi ana shida, though ukweli ni kwamba le mutuz naye kuna wakati nati kichwani zilikuwa kama zimelegea na kujifanya baharia na uzungu uzungu wake ule. ila alikuwa mtu poa sana.
 
Mara ya mwisho kusikitika sana kwa msiba wa mtu maarufu ilikuwa ni msiba wa Seth Bikira wa Kisukuma na leo kwa mara nyingine nina huzuni mno. Lemutuz alikuwa na utu pamoja na ishu zake zingine zilizokuwa kama zinaleta ukakasi. Huyu ni mtu aliyetaka vijana wafanikiwe kimaisha... alikuwa na upendo mkubwa kwa vijana. Mwaka 2014 alituandalia semina ya ujasiriamali ambayo ilikuwa na wazungumzaji wengi heavyweights akiwemo Ruge Mutahaba, Ridhiwani, Davis Mosha, DC Zainab na wengine. Hata machapisho yake mitandaoni zilikuwa zina mafunzo mengi kwa vijana. Alikuwa akisisitiza sana vijana wajasiriamali kuhakikisha tunaaminika na wadau wote hasa taasisi za fedha. Huu ushauri wake nimekuwa nikiuzingatia sana.

MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA. NIMESIKITIKA SANA LEO.
Nami nilikuwepo hiyo siku, hivi ilikuwaga ukumbi gani vile?
 
Sisi kwetu Tanga twasema "Mtumba Tikubada" yaani mjomba kaenda.

Ilikuwa ni mwaka 2005 nikiwa States kwenye jitihada zangu za kusaka vyeti, nikakutana na Field Marshal aka Le Mutuz real name William Malecela.

Nilikuwa namuita uncle kwani alikuwa ni mkubwa kidogo kwangu ila ukija kwenye kukaa na kujadili politics na mikakati ya maisha, kwa kweli Le Mutuz alikuwa nguli.

Katika watoto wa wakubwa ambao nimekutana nao iwe ndani au nje ya nchi Le Mutuz huwezi fahamu kuwa ni mtoto wa mkubwa yaani mzee John Malecela alikuwa ni mmoja wa viongozi ambao wana vijana walo "humble" sana si wa kujikweza.

Wapo watoto wengi wa wakubwa wa siku hizi ambao hujidai na kutukana watu na kufanya ujinga mwingi lakini huyu Le Mutuz aliheshimu watu na ukiwa na hoja basi mtabishana kwa hoja.

Ndie alienieleza kuhusu JF enzi hizo imetoka kuanzishwa ikiitwa Jambo Forums na baadae nilipokuwa Zurich kikazi mwaka 2006 nikajiunga rasmi hadi leo.

Tukiwa JF, tuwe na staha na kuheshimu michango ya wengine na kuheshimu watu khasa wale usowafahamu maana hatufahamu ya kesho.

Binadamu tuhangaike kwa namna yoyote ile hapa duniani bado yabaki kuwa Dunia ni mapito na sote tutailamba vumbi iwe kwa hiari au kwa mshinikizo lakini Mungu hutupokea.

RIP Le Mutuz aka Field Marshal, baharia, real Name William Malecela mzee wa "You Know I know".
Niliposoma hapo umesema ulikuwa zurich akili yangu inaenda mbali natamani sana, you are living the life i dream of
 
Back
Top Bottom