TANZIA William Malecela (Le Mutuz) afariki Dunia

TANZIA William Malecela (Le Mutuz) afariki Dunia

Lemutuz alikwa na miaka 60 +.Sema post zake Instagram zilikuwa zinamfanya aonekane mdogo kuliko umri wake halisi.
Nilikua namuona kwenye 40 hivi, kumbe ni mtu mzima hivyo? mitandao hii inatuvua nguo mno!
 
Ndo mkuu, nimekaa pale kama mwaka hivi nazunguka hapo na Geneva.

Mimi nimefanya kazi kwenye mashirika ya kimataifa na mojawapo ni UNHCR hivyo nimezunguka kidogo hii dunia yetu tambarare.
Mkuu, naomba nije PM kwa sababu huko ulipopita ndipo na mimi natamani kupita,mimi ni kijana nina degree na leseni ya udereva, naamini nikiwa nawasiliana na watu wa aina yako kuna mawili, huenda na mimi nikatimiza ndoto yangu ya kufanya kazi hizo NGO au nikapata chochote kizuri katika maisha
 
Sidhani kama watawaza,,,,,,
Mimi kiukweli Sina excuse yoyote na baba anaekimbia watoto.sina.
Kulea watoto mwenyewe kunaleta simanzi moyo unaweza ukafa ganzi ukatamani huyo jamaa afe
Yeye alisemaga aligombanaga na mama Yao,,,ila watoto wanasema aliwaaga anaenda kusalimia bongo na hakukua na ugomvi na haluwai kurudi na wala hakuwahi kiwatafuta..
My dear baba ambaye hakuwajal tangu watoto Leo hii unafikiri watakua na uchungu?
Na SI ajabu wamekua Kwa taaabu...
Kama wewe ni mwanaume hata kama unampitia taabu vip na uliyezaa nae hakikisha upotezi mawasiliano/ukaribu na wanao hata kama huna pesa ...usije baadae ukapopup tu....kulea watoto mwenyewe ni taaabu sana
Wanawake ndo chanzo, mnapenda kubaki na watoto mkiwafundisha sisi ni wabaya
 
Mkuu, naomba nije PM kwa sababu huko ulipopita ndipo na mimi natamani kupita,mimi ni kijana nina degree na leseni ya udereva, naamini nikiwa nawasiliana na watu wa aina yako kuna mawili, huenda na mimi nikatimiza ndoto yangu ya kufanya kazi hizo NGO au nikapata chochote kizuri katika maisha
Sikuzuii kuja JF lakini mimi ni mtu ambe nipo "busy" mno na mihangaiko yangu hivyo nikipata nafasi ntakupa za hapa na pale.

Kazi ya UN huwa wazitangaza kwenye website yao na watakiwa kuwa wazifuatilia.

Kwa sasa sifanyi kazi huko ila ntakupa dondoo za hapa na pale.

Lakini mimi nilianza kufanya kazi UNHCR baada ya masomo nikapangwa Kigoma enzi hizo.

Hivyo kama wapiga kazi mwajiri wako aweza kuanza kukuhamisha na mara nyingi kituo kinofuata ni Nairobi.

Baada ya hapo weye wenyewe huanza kuangalia kazi zitokazo ambazo twaziita "internal" kwa wale waajiriwa na baadae huzitoa kwa public.

Hivyo anza na UNHCR ya Tanzania, Arusha kuna ile mahakama ya kimataifa na Nairobi pia pana ofisi za mashir

Pia pale barabara ya Sokoine karibu na stesheni ya reli pana ofisi za UN karibu na ofisi za mazee.

Hivyo ukiwa JF pia pitia hizo website zao.

Na si lazima upate kazi ya juu waweza kuanza kama dereva ambae hulipwa "foreign currency" khasa dola.
 
Sisi kwetu Tanga twasema "Mtumba Tikubada" yaani mjomba kaenda.

Ilikuwa ni mwaka 2005 nikiwa States kwenye jitihada zangu za kusaka vyeti, nikakutana na Field Marshal aka Le Mutuz real name William Malecela.

Nilikuwa namuita uncle kwani alikuwa ni mkubwa kidogo kwangu ila ukija kwenye kukaa na kujadili politics na mikakati ya maisha, kwa kweli Le Mutuz alikuwa nguli.

Katika watoto wa wakubwa ambao nimekutana nao iwe ndani au nje ya nchi Le Mutuz huwezi fahamu kuwa ni mtoto wa mkubwa yaani mzee John Malecela alikuwa ni mmoja wa viongozi ambao wana vijana walo "humble" sana si wa kujikweza.

Wapo watoto wengi wa wakubwa wa siku hizi ambao hujidai na kutukana watu na kufanya ujinga mwingi lakini huyu Le Mutuz aliheshimu watu na ukiwa na hoja basi mtabishana kwa hoja.

Ndie alienieleza kuhusu JF enzi hizo imetoka kuanzishwa ikiitwa Jambo Forums na baadae nilipokuwa Zurich kikazi mwaka 2006 nikajiunga rasmi hadi leo.

Tukiwa JF, tuwe na staha na kuheshimu michango ya wengine na kuheshimu watu khasa wale usowafahamu maana hatufahamu ya kesho.

Binadamu tuhangaike kwa namna yoyote ile hapa duniani bado yabaki kuwa Dunia ni mapito na sote tutailamba vumbi iwe kwa hiari au kwa mshinikizo lakini Mungu hutupokea.

RIP Le Mutuz aka Field Marshal, baharia, real Name William Malecela mzee wa "You Know I know".
Kumbe mabeberu ndo wanakupa ugali afu unawakandia na kumpenda Mrusi
 
Back
Top Bottom