TANZIA William Malecela (Le Mutuz) afariki Dunia

TANZIA William Malecela (Le Mutuz) afariki Dunia

Sisi kwetu Tanga twasema "Mtumba Tikubada" yaani mjomba kaenda.

Ilikuwa ni mwaka 2005 nikiwa States kwenye jitihada zangu za kusaka vyeti, nikakutana na Field Marshal aka Le Mutuz real name William Malecela.

Nilikuwa namuita uncle kwani alikuwa ni mkubwa kidogo kwangu ila ukija kwenye kukaa na kujadili politics na mikakati ya maisha, kwa kweli Le Mutuz alikuwa nguli.

Katika watoto wa wakubwa ambao nimekutana nao iwe ndani au nje ya nchi Le Mutuz huwezi fahamu kuwa ni mtoto wa mkubwa yaani mzee John Malecela alikuwa ni mmoja wa viongozi ambao wana vijana walo "humble" sana si wa kujikweza.

Wapo watoto wengi wa wakubwa wa siku hizi ambao hujidai na kutukana watu na kufanya ujinga mwingi lakini huyu Le Mutuz aliheshimu watu na ukiwa na hoja basi mtabishana kwa hoja.

Ndie alienieleza kuhusu JF enzi hizo imetoka kuanzishwa ikiitwa Jambo Forums na baadae nilipokuwa Zurich kikazi mwaka 2006 nikajiunga rasmi hadi leo.

Tukiwa JF, tuwe na staha na kuheshimu michango ya wengine na kuheshimu watu khasa wale usowafahamu maana hatufahamu ya kesho.

Binadamu tuhangaike kwa namna yoyote ile hapa duniani bado yabaki kuwa Dunia ni mapito na sote tutailamba vumbi iwe kwa hiari au kwa mshinikizo lakini Mungu hutupokea.

RIP Le Mutuz aka Field Marshal, baharia, real Name William Malecela mzee wa "You Know I know".
Uzi huu nimeusoma kwa umakini nimefurahi kuona comments za watu waliojiunga jf wakati inaanza wakati huo sisi tuko secondly hatujui yanayoendelea duniani. Shikamoo.
 
Duh,Apumnzike kwa amani. Huyu alikuwa anakula good time na Wabebez. Ila maisha yanazidi kunifundisha kuwa Humble.
HEEEeeeHeeEEeeh!

Dakika chache tu zilizopita baada ya kuandika hayo ukawa umesahau kila kitu!

Hayo ndiyo maisha.

Watu wangetembea na zigo la huzuni kila siku, sijui dunia ingekuwaje?

Ishi maisha yako tu, kama ulivyopangiwa kuyaishi, usitafute kurekebisha kwa matukio yanayopita haraka haraka.
 
Death Is the Destination we all share

Death is Certain

Kifo ni hakika, sote tutakipitia endapo Bwana atachelewa Rudi
Kwa Hakika, na umesema vizuri ikiwa Bwana Yesu Kristo atakuwa bado hajarudi (Lazima atarudi kama alivyoahidi)

Akirudi mapema parapanda itakapolia na kukuta watakatifu walio Hai, basi hawatapitia mauti.
 
Uzi huu nimeusoma kwa umakini nimefurahi kuona comments za watu waliojiunga jf wakati inaanza wakati huo sisi tuko secondly hatujui yanayoendelea duniani. Shikamoo.
Taasisi huanzishwa na waasisi.

Tumetoka mbali sana, msituone hivi ujue?

Kulikuwa na chama la uhakika hapa likijadili issues, Field Marshal, Kibunango, Steve D, Mwanakijiji, Balantanda, Kana ka Nsungu na wengine wengi sana.

Ila mimi umri nao waanza kuingia utu uzima sema mazoezi ya hapa na pale, kunyanyua vitu vizito, kukimbia na napapenda sana Arusha nikiwa kwa kazi.

Arusha ndo kituo changu cha kwanza cha zile kazi zetu zile za kuonyesha watalii wapi pa kwenda kazi na mihangaiko baada ya shule.

You know what I mean?

😉
 
Duuuh Aiseee Jana tu alipost ofisi yake ya TANCOT House Down town Posta!

Poleni Ndugu ,Jamaa na Marafiki.
Mi nimemuona pale Ben tower ijumaa yaan juzi[emoji26]

Kama kawaida yake na wabebez akaniita nikamsonya akacheka sana, ...masikini ningeenda hata kumsikiliza utani wake then nicheke nisepe! Imeniuma sana
 
Back
Top Bottom