Mara ya mwisho kusikitika sana kwa msiba wa mtu maarufu ilikuwa ni msiba wa Seth Bikira wa Kisukuma na leo kwa mara nyingine nina huzuni mno. Lemutuz alikuwa na utu pamoja na ishu zake zingine zilizokuwa kama zinaleta ukakasi. Huyu ni mtu aliyetaka vijana wafanikiwe kimaisha... alikuwa na upendo mkubwa kwa vijana. Mwaka 2014 alituandalia semina ya ujasiriamali ambayo ilikuwa na wazungumzaji wengi heavyweights akiwemo Ruge Mutahaba, Ridhiwani, Davis Mosha, DC Zainab na wengine. Hata machapisho yake mitandaoni zilikuwa zina mafunzo mengi kwa vijana. Alikuwa akisisitiza sana vijana wajasiriamali kuhakikisha tunaaminika na wadau wote hasa taasisi za fedha. Huu ushauri wake nimekuwa nikiuzingatia sana.
MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA. NIMESIKITIKA SANA LEO.