William Miller: Kama Yesu hakujua Hisabati au kutafsiri mambo bora angalikaa Kimya. Mbona siku ya mwisho wa dunia inakokotoleka kirahisi?

Hatimaye, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo na sifa njema, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote ya kupendeza, yoyote yenye staha, ukiwepo uzuri wowote, pakiwepo chochote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo.
Wafilipi 4:8 NEN
 
Yesu alipokuwa ameketi kwenye Mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamjia faraghani, wakamuuliza, “Tuambie, mambo haya yatatukia lini, nayo dalili ya kuja kwako na ya mwisho wa dunia ni gani?”

Yesu akawajibu, “Jihadharini, mtu yeyote asiwadanganye. Kwa maana wengi watakuja kwa Jina langu, wakidai, ‘Mimi ndiye Kristo,’ nao watawadanganya wengi.

VITA: Mtasikia habari za vita na matetesi ya vita. Angalieni msitishike, kwa maana haya hayana budi kutukia. Lakini ule mwisho bado. Taifa litainuka dhidi ya taifa, na ufalme dhidi ya ufalme.

NJAA& MATETEMEKO: Kutakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali. “Ndipo mtasalitiwa, ili mteswe na kuuawa, nanyi mtachukiwa na mataifa yote kwa ajili yangu.

UPENDO KUPOA: Wakati huo, wengi wataacha imani yao, nao watasalitiana kila mmoja na mwenzake na kuchukiana.

ROHO YA UONGO: Watatokea manabii wengi wa uongo, nao watawadanganya watu wengi. Kwa sababu ya kuongezeka kwa uovu upendo wa watu wengi utapoa, lakini yule atakayevumilia hadi mwisho ataokolewa.

Injili ya Ufalme itahubiriwa ulimwenguni kote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo mwisho utakapokuja. “Hivyo mtakapoona lile ‘chukizo la uharibifu’ lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu (asomaye na afahamu), basi wale walioko Uyahudi wakimbilie milimani. Yeyote aliye juu ya dari ya nyumba asishuke ili kuchukua chochote kutoka ndani ya nyumba. Aliye shambani asirudi nyumbani kuchukua vazi lake. Ole wao wenye mimba na wale wanaonyonyesha watoto siku hizo! Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi au siku ya Sabato. Kwa maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo wa dunia mpaka sasa: wala haitakuwako tena kamwe. Kama siku hizo zisingefupishwa, hakuna hata mtu mmoja ambaye angeokoka. Lakini kwa ajili ya wateule, siku hizo zitafupizwa. Wakati huo kama mtu yeyote akiwaambia, ‘Tazama, Kristo huyu hapa!’ Au, ‘Kristo yuko kule,’ msisadiki. Kwa maana watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo, nao watafanya ishara kubwa na maajabu mengi ili kuwapotosha, ikiwezekana, hata wale wateule hasa. Angalieni, nimekwisha kuwaambia mapema. “Kwa hiyo mtu yeyote akiwaambia, ‘Yule kule nyikani,’ msiende huko. Au akisema, ‘Yuko kwenye chumba,’ msisadiki. Kwa maana kama vile umeme utokeavyo mashariki na kuonekana hata magharibi, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa maana popote ulipo mzoga, huko ndiko wakusanyikapo tai. “Mara baada ya dhiki ya siku zile, “ ‘jua litatiwa giza, nao mwezi hautatoa nuru yake; nazo nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za anga zitatikisika.’


UJIO WA PILI WA KRISTO: “Ndipo itakapotokea ishara ya Mwana wa Adamu angani, na makabila yote ya dunia yataomboleza. Nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya angani, katika uwezo na utukufu mkuu. Naye atawatuma malaika zake kwa sauti kuu ya tarumbeta, nao watawakusanya wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho mmoja wa mbingu hadi mwisho mwingine.
Mathayo 24:3‭-‬7‭, ‬9‭-‬31 NEN
 
Mnajadili "fix" tupu!
Kwa maana Lutheran haikutokea Anglican bali Roman Catholic.
Sasa kama hili lililo wazi kabisa machoni petu linadanganywa itakuwaje hayo ya miaka maelfu kadhaa iliyopita?
 
Huu mjadala mtamu sana ngoja nikitafute kitabu cha Daniel nikipitie alafu nirudi.

Ni kweli mjadala ni mzuri sana kwa sababu yawezekana tumepuuza jambo ambalo linaweza kutusaidia binadamu kujiandaa dakika za mwisho mwisho kabla Yesu hajaanza kutoka katika chumba cha "patakatifu pa patakatifu" na hivi nasi watenda dhambi kuingia pamoja na wasabato wateule.
 

Hayo maombezi,Yesu anawaombea akina nani hapo "chumbani patakatifu pa patakatifu'?
 
Ilishaandikwa "Hakuna ajuaye siku wala saa ya kurudi kwa mwana wa Adam" ikimaanisha kurudi kwa Yesu Kristo ni siri ya Mungu mwenyewe, kwahiyo huyo Miller na wapuuzi wenzie waondolee huko upuuzi wao
Na ndivyo wazee wa kanisa walinifundisha, mpaka watakapobadilisha mafunzo hayo sibadili msimamo huo, wazee wa kanisa wakisema jambo sibadili msimamo wao hadi waseme tena vingjnevyo, halafu period!
 
Kanisa la anglikana ndio Lutherani ya leo???

Kuna tofauti kubwa mkuu.Kanisa la Anglikana ni lile ambalo muanzilishi wake ni Mfalme Henrio wa VII wa Uingereza.Huyu alijiondoa kutoka Kanisa Katoliki baada ya kukataliwa na Papa kumtaliki mke wake wa ndoa ili aweze kuvuta kimada.

Na Kanisa la Lutheran ni lile linaloitwa KKKT au wana matengenezo.Hili lilichomoka kutoka Kanisa Katoliki baada ya Padri anayeitwa Martin Luther kutengwa na kanisa katoliki kwa kudai alikuwa na mambo yake yaliyokuwa yanahitaji kufanyiwa kazi.
 
Na lilianza Lutheran ,kisha wakafuata Anglican si ndio Mkuu ?
 
Nimekuelewa, rekebisha kwenye mada umeandika Lutherani ya leo asili yake ni anglikana.
 
Mkuu kwenye maada ukaedit kule ili kutowachanganya watu kwani kuna sehemu umeandika lutherani ilitokana na kanisa la Anglican
 
Soma yale maswali yake ndo utaona alikuwa analenga nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…