William Miller: Kama Yesu hakujua Hisabati au kutafsiri mambo bora angalikaa Kimya. Mbona siku ya mwisho wa dunia inakokotoleka kirahisi?

William Miller: Kama Yesu hakujua Hisabati au kutafsiri mambo bora angalikaa Kimya. Mbona siku ya mwisho wa dunia inakokotoleka kirahisi?

1. Tupatie andiko kwamba Mbingu ina vyumba au horizons.
2. Yesu ni Mungu na hivi ana uwezo wa kutuombea akiwa popote pale.je,kulikuwa na ulazima gani kwake kuingia huko Chumbani("patakatifu pa patakatifu") toka mwaka 1844 hadi leo ili kufanya tu hiyo huduma ya maombezi?
3. Ellen White yeye alifundisha kwamba Yesu yuko hapa patakatifu pa patakatifu akiendesha hukumu ya kipelelezi(Investigative Judgement).Je, huduma ya maombezi ni hukumu ya upelelezi?
Fundisho Kuhusu Patakatifu pa Duniani ,Na Jinsi linavyoakisi Huduma ya Yesu Katika Patakatifu pa Mbinguni


Katika Biblia patakatifu pa duniani ni mfano wa patakatifu pa mbinguni. Paulo anapaita patakatifu pa duniani kuwa ni kivuli cha Mambo ya Mbinguni. Biblia yasema hivi;’-watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima. [Waebr8:5]. Hivyo Basi tunaona Ukweli Ufuatao

1. Patakatifu pa duniani ni mfano wa patakatifu pa mbinguni. Patakatifu pa mbinguni ni kitu halisi ambapo patakatifu pa duniani ni kivuli chake, ama mfano wake.

2. Patakatifu pa duniani palikuwa na Hema mbili zilizotenganishwa kwa pazia katikati, Hema ya kwanza iliitwa patakatifu, na Hema ya pili iliitwa Patakatifu Mno. [Tazama Ebr9:2-3].

3. Hema ile ya Kwanza iitwayo Patakatifu palikuwa na vitu vifuatavyo. Palikuwa na kinara cha taa, na meza, na mikate ya Wonyesho, na madhabahu ya dhahabu ya kufukizia uvumba;Tazama Kut40:22-27,Tazama pia Waebr9:2]

4. Hema ile ya Pili iliyiitwa Patakatifu mno ilikuwa na vifuatavyo;”-Chetezo cha dhahabu,Sanduku la Agano lililofunikwa kwa dhahabu pande zote,Kopo la Dhahabu lenye Mana, Fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao viwili vya Agano,[Taz Ebr9:3-5].

5. Katika ile Hema ya kwanza iitwayo Patakatifu, Makuhani waliingia kila siku, Lakini katika Ile Hema ya Pili iitwayo patakatifu Mno Kuhani Mkuu aliingia mara moja kwa Mwaka.[TazamaEbr9:6-7].

6. Huduma za kutoa kafara zilizokuwa zinafanyika kila siku Asubuhi na Jioni daima katika Ile hema ya kwanza iitwayo patakatifu zilikuwa zinafanyika ifuatavyo. Mdhambi alikuwa anakuja na mnyama wake awe kondoo ama ng’ombe mkamilifu, anamleta mbele ya kuhani katika ile Hema ya kukutania. Na kisha anaweka mkono wake juu ya mnyama na kuziungama dhambi zake zote juu ya mnyama yule. Mnyama yule anafungwa na kuwekwa juu ya madhabahu na kisha mdhambi anaagizwa amchinje. Kisha Kuhani aliyetiwa mafuta anaitwaa baadhi ya damu ya yule mnyama na kuingia nayo hadi patakatifu na kisha anainyunyiza juu ya mapazia ya hekalu na juu ya madhabahu ya kufukiza uvumba. Hivyo kwa njia ya damu dhambi zilizotubiwa za mdhambi zinaamishwa hadi patakatifu kwenye mapazia ya hekalu. Na Baada ya hapo yule mnyama alikuwa anateketezwa kwa moto. Tazama[Wal4:1-11].

7. Huduma za kutoa makafara zilizokuwa zikifanyika mara moja kwa mwaka katika ile Hema ya pili iitwayo Patakatifu Mno ilikuwa kama ifuatavyo. Mara moja kwa Mwaka ilikuwa inaitwa Siku kuu ya upatanisho. Wana wa Israeli wote walikusanyika mbele ya Hema ya kukutania, wakijichunguza nafsi zao na kuziungama dhambi zao mbele za Mungu. Kuhani Mkuu akiisha kufanya Upatanisho wa nafsi yake Mwenyewe, Walichaguliwa Mbuzi wawili wakamilifu na kupigiwa kura ili apatikane Mbuzi wa Bwana na Mbuzi wa Azazeli. Yule aliyeangukiwa kuwa Mbuzi wa Bwana, anachukuliwa na kufanywa sadaka ya dhambi.Mnyama yule anachinjwa na Kuhani anaichukua Damu ya yule mnyama na kuingia nayo patakatifu mno, na kuinyunyiza juu ya kiti cha Rehema, na mbele ya kiti cha rehema, na kisha atatoka nje na ile damu na kuinyunyiza juu ya madhabahu iliyo mbele za Bwana. Hivyo kwa njia hiyo machafu yote ambayo yalikuwa yakihamishwa kwa njia ya damu hadi mle kwenye Hema ya kwanza iitwayo patakatifu yalitoka yote na kuwa juu ya mikono ya kuhani. Na kisha kuhani alimchukua yule mbuzi wa Azazeli na kisha kuziungama dhambi zile zote za Mkutano wa wana wa Israeli juu ya mbuzi wa Azazeli. Na kisha anachaguliwa Mtu ambaye atamchukua Mbuzi wa Azazeli na kwenda naye mpaka jangwani na kumwacha huko. Hivyo ndivyo Patakatifu palivyotakaswa katika Hekalu la zamani. [Tazama Wal16:1-34]

8. Kama tulivyoona Mwanzoni kuwa patakatifu pa kale pa kidunia palikuwa ni mfano ama kivuli cha patakatifu pa mbinguni, na Musa aliagizwa kutengeneza patakatifu pa kidunia kwa mfano wa patakatifu pa mbinguni kama alivyoonyeshwa. Hivyo kwa maana nyingine ni kwamba patakatifu pa mbinguni ndipo patakatifu halisi, na ambapo pa dunia ni mfano wake. Hivyo mfumo wa patakatifu pa duniani ni taswira na mfanano wa patakatifu pa mbinguni.

9. Swali ka Kujiuliza ni kwamba Je Mbinguni kuna patakatifu[ Santuary]? Na kama lipo linafananaje?

10. Biblia iko wazi kuwa Mbinguni kuna patakatifu, ile hema ya kweli ambayo imefanyika pasipo mikono ya Mwanadamu ambamo Yesu amekwenda kuhudumu kwa ajili yetu. Biblia yasema hivi;’-Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni, mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu. [Ebr8:1-2].

11. Nabii Yohana alionyeshwa Mlango wa Hekalu la Mbinguni ukifunguliwa, Akaonyeshwa ile Hema ya Kwanza iitwayo patakatifu na akamwona Mungu akiwa ameketi kitini pa enzi akizungukwa na Wazee ishirini nan ne, na wale wenye Uhai wanne. Mbele zake zinawaka taa saba za Moto na ndizo Roho saba za Mungu. Taz Ufu4:5]. Tunatambua kuwa hapa ni ile hema ya kwanza iitwayo patakatifu sababu zle taa saba za Moto katika patakatifu pa duniani ziliwakilishwa na kile kinara cha taa chenye taa saba. Katika Kitabu cha Ufunuo 8;3-5, tunaona madhabahu ya dhahabu ya kufukiza Uvumba iliyo mbele za Bwana, chetezo cha kufukiza uvumba, Madhabahu ya dhahabu ya kufukizia Uvumba ilikuwepo katika ile Hema ya kwanza iitwayo Patakatifu.

12. Nabii Yohana alionyeshwa pia Hekalu lililoko mbinguni likifunguliwa tena na kisha akaona Sanduku lile la Agano lenye kubeba Amri kumi. Hapa Nabii alionyeshwa ile Hema ya pili iitwayo Patakatifu mno. Sanduku la Agano katika Hekalu la Kidunia lilikaa patakatifu Mno.Biblia yasema hivi;’-Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi sana. [Ufu11:19]

13. Hivyo basi tunaona kuwa kama patakatifu pa kidunia palivyo na sehemu mbili ambazo zinatanganishwa na pazia yaani patakatifu na patakatifu Mno, hali kadhalika na patakatifu pa mbinguni pana sehemu mbili ambazo ni Patakatifu na Patakatifu mno.

14. Hebu sasa tuangalie Mfanano wa huduma kama zilivyokuwa zikifanyika katika patakatifu pa duniani na patakatifu pa mbinguni.

15. Katika patakatifu pa kidunia makuhani ama kuhani Mkuu aliingia patakatifu kwa damu ya wanyama ili kuwafanyia wana wa Israeli upatanisho. Katika patakatifu pa mbinguni Yesu anaingia kwa damu yake mwenyewe ili kuwafanya watu wake upatanisho. Biblia yasema hivi;’- wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. [Ebr9:12]

16. Katika Patakatifu pa duniani, Kiti cha rehema na Sanduku la Agano lilikaa katika Ile hema ya pili iitwayo Patakatifu mno, Lakini Utukufu wa Mungu ulipopashukia Patakatifu mno na kukaa juu ya kiti cha rehema, Utukufu wa Mungu ulipajaza mahala pote patakatifu na patakatifu mno, kama ishara kuwa Uwepo wa Mungu unapatikana kote kote iwe ni Patakatifu ama iwe ni patakatifu mno. Hali kadhalika na katika patakatifu pa mbinguni Mungu anaonekana katika Hema zote mbili iwe ni patakatifu ama patakatifu mno.[Tazama Kut40:34]

17. Kila Siku daima, Makuhani waliingia Patakatifu wakiwa na damu ya mnyama ili kufanya upatanisho, Hali kadhalika na Kristo baada ya kupaa na kwenda mbinguni, alikwenda kukaa mkono wa kuume wa Mungu na kuanza kazi yake ya kuwafanyia watu wake upatanisho na kuwaombea. Biblia yasema hivi;’-Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni, mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu. [Ebr8:1-2].

18. Mara moja kwa Mwaka Kuhani Mkuu aliingia patakatifu mno ili kupatakasa patakatifu. Hali kadhalika na Kristo Aliingia patakatifu mno Mwaka 1844 AD, ili kupatakasa Patakatifu kulingana na unabii wa Daniel wa siku 2300 ambao ni sawa na Miaka 2300.Unabii unasema kuwa Mwishoni mwa siku 2300 ndipo patakatifu pataakaswa. [Tazama Dan8:14.]

19. Katika Patakatufu pa kidunia, Baada ya Mdhambi kumchinja mnyama, Kuhani aliichukua ile damu na kisha kuinyunyiza katika mapazia ya Hekalu, na hivyo kwa njia ya damu Dhambi za mdhambi aliyetubu kuhamishwa katika mapazia ya hekalu kama kumbukumbu ya dhambi zake, zikisubiri kusafishwa mara moja kila Mwaka. Katika patakatifu pa mbinguni, dhambi zote za watakatifu zilizosamehewa na kutubiwa, zinarekodiwa katika vitabu vya mbinguni, pamoja na ushahidi wa toba yake ya dhati, vikisubiri kuja kuondolewa kwa umilele wakati wa kazi ya Yesu katika ile hema ya pili iitwayo patakatifu mno. Musa alipowaombea wana wa Israel aliomba hivi;’- ;’-Walakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi yao - na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichoandika.[Kut32:32]. Lakini Jibu la Mungu likawa hivi;’-Bwana akamwambia Musa, Mtu ye yote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu. [Kut32:33].Pia soma Ufu20:12.

20. Mara moja kwa Mwaka katika patakatifu pa kidunia Kuhani mkuu aliingia Patakatifu Mno na damu ya Mbuzi ili kupatakasa patakatifu. Mbuzi wawili walipigiwa Kura mmoja awe wa Bwana na Mwingine awe wa Azazeli. Mbuzi wa Bwana alichinjwa na kuhani aliichukua damu ya mnyama na kuinyunyiza juu ya kiti cha Rehema, na mbele ya kiti cha rehema, na hivyo dhambi zote zilizokuwa zikihamishwa ndani ya ile hema ya patakatifu kwenye mapazia ya Hekalu zilikuwa zinaondolewa zote na patakatifu panatakaswa na dhambi zote zinakuwa juu ya mikono ya kuhani. Na kisha anachukuliwa yume Mbuzi wa Azazeli na Kisha kuhani anaweka Mikono yake juu ya Mbuzi wa Azazeli. Hivyo machafu yote ya wana wa Izraeli yalitoka kwenye Mikono ya kuhani hadi kwa Mbuzi wa Azazeli, na kisha Mtu aliyewekwa tayari aliagizwa amchukue Mbuzi huyo na kwenda naye jangwani na kumuacha huko. Hali kadhalika na Patakatifu pa mbinguni, Nabii Danieli alionyeshwa kuwa Mwishoni mwa siku 2300 ambayo ni sawasawa na Miaka 2300, ambazo kulingana na Unabii ziliishia mwaka 1844 AD, Yesu aliingia Patakatifu Mno pa Mbinguni ili kupatakasa patakatifu. Tokea Mwaka huo vitabu vya mbinguni vimekuwa vikikaguliwa na kuchunguzwa, na wale watakatifu waliotubu katika Damu ya Yesu dhambi zao zinafutwa milele, na majina yao yanadumishwa katika kitabu cha Uzima. Lakini wale watakatifu ambao wataonekana kuwa kuna dhambi ambayo haikutubiwa, basi dhambi zao hazitafutwa hata milele na majina yao yatafutwa yatoke katika kitabu cha Uzima. Dhambi ambazo watakatifu walizitenda zitafutwa na zitawekwa mikononi mwa Yesu, na kazi yake katika patakatifu pa mbinguni ikiisha, ndipo ataziweka dhambi zote ambazo watakatifu walisababishiwa kuzitenda juu ya Shetani, na Shetani atafungwa hapa duniani na malaika zake mda wa Miaka Elfu, akisubiri Uangamivu wake wa Mwisho. Kazi ya Yesu katika patakatifu mno mbinguni ikiisha, Anapewa Ufalme, na idadi ya waliokombolewa inakamilika. Yesu atarudi kuwachukua watakatifu.

21. Nabii Danieli alionyeshwa Baba akihama toka patakatifu na kwenda patakatifu mno kwa kiti chake cha Enzi cha Moto na chenye Magurudumu ya moto. Alionyeshwa malaika Maelfuelfu wakisimama mbele zake na kumtumikia. Alionyeshwa vitabu vya mbinguni vikifunguliwa na kuchunguzwa, na Upinga Kristo uliovaa vazi la Udini ukihukumiwa. Biblia yasema hivi;’- Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao. Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa. [Dan7:9-10].

22. Nabii Daniel alionyeshwa Yesu akija na Mawingu ya Mbinguni, sii kuja hapa duniani, bali akimkaribia mzee wa siku huko Patakatifu mno mbinguni, ili kumalizia kazi yake ya Mwisho ya Upatanisho katika patakatifu pa mbinguni, na kusimama kama mtetezi wa watakatifu wakati rekodi zao zinapokaguliwa mbele za Baba. Kazi yake ikiisha anapewa ufalme, na kisha anakuja kuwachukua watakatifu. Biblia yasema hivi;’- Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa. [Dan7:13-14]
 
Aliyekuambia mimi kuwa hivyo vitabu sijasoma mpaka mmoja anipe ushauri wa kuvielewa na nani...?

Kwanini unataka nivielewe kwa jinsi yako wewe(Ellen G White kind of Thinking)


Wewe ndiye unayepaswa kukaa chini na tukufundishe maana y vitabu vyenye maandishi ya Kiapokaliptiki
Unasoma lakini huelewi...kama unaelewa tupe tafasri ya unabii wa Daniel 8:14 wa siku 2300.
 
Sasa kama unawafahamu kwanini umeandika kituko kama kile....???

Nimeshangaa kwanini unakataa William Miller hakuwa muanzilishi wa Usabato....
Miller hakuanzisha usabato. Walioanzisha SDA ni wakina Joseph Bates, James White na Ellen White na wengine.

Miller alikuwa mbabtist....na hata Ellen white na wenzake alikuwa wababtist, baada ya hiyo Great Disappointment, walianza kusoma biblia upya na kujifunza unabii upya, na ndipo EGW akaonyeshwa maana halisi ya unabii wa Daniel 8:14 na akaonyeshwa patakatifu pa mbinguni na akaonyeshwa lile sanduku la agano lililo na Amri Kumi za Mungu, na amri ya nne ya ya sabato ilikuwa inang'aa kuliko amri zingine.

Na ndiyo alipoendelea kujifunza biblia akaendelea kufunuliwa zaidi kuhusiana na sabato. Na ndipo yeye na wenzake wakaondoka katika kanisa la Baptist na kuanza kusali siku ya saba ya Juma, na ndipo SDA kama dhehebu likaanzishwa.
 
"Kanisa la Kibaptisti, ni mumeguko karne ya 17 BK kutoka Kanisa la England,yaani Kanisa la Serikali ya Uingereza (Anglikani) ambalo leo linaitwa Lutheran Church."

Mtoa mada HAJUI ALICHOKIANDIKA.
Baada ya para hiyo hapo juu nimekataa kuendelea kusoma.
 
Nimekkuuliza unanilazimisha kufafanulia kwa jinsi ya Kisabato....???? Yani jinsi ambavyo kitabu cha "Pambano Kuu" (Great Controversy) kinavyoeleza...??


Nani aliwaloga Wasabato...?
Sasa si utoe hiyo tafasiri yako...mbona unaruka ruka tu?
 
Umeandika kiushabiki sana. Lengo lako ni kuwaattack wasabato na wala si vinginevyo.

Mambo mengi uliyoeleza hapa si ya kweli, kama ifuatavyo.

1. Miller haukuwa msabato na hata kipindi akiwa anahubiri kurudi kwa Yesu, hapakuwa na dhehebu la kisabato.

2. Mama White pia hakuwa msabato kipindi hicho maana hapakuwa na hilo dhehebu, na wala hakuwa mwanzilishi wa hiyo kanuni ya kurudi Yesu unayoisema, isipokuwa alikuwa mfuasi wa Miller.

3. Papa hatawafumusha wasabato kusali jumamosi kama ulivyodai, badala yake atawalazimisha watu wote kusali siku ya kwanza ya juma (yaani Jumapili) badala ya siku ya saba ya juma (yaani Jumamosi).

4. Yesu yuko katika chumba cha patakatifu pa patakatifu mbinguni akifanya huduma ya uombezi, na si kwamba ameshaanza kushuka kuja duniani kama unavyodai. Maana patakatifu pa patakatifu ni mbinguni.

5. Wasabato hawaja set siku yoyote ya kuja kwa Yesu kama unavyotaka kuwaaminisha watu, badala yake wamaamini kwamba Yesu amekaribia sana maana dalili karibia zote zimeshatimia.

6. Pamoja na kukosoa mahesabu ya Miller kuhusiana na unabii wa Daniel wa siku 2,300, hujatoa tafsiri mbadala wa unabii huo kana k
kwamba unabii huo hauna maana yoyote kwa wanadamu wa leo.

7. Ukweli ni kwamba, mahesabu ya Miller yalikuwa sahihi, kwamba mwaka 1844 kulikuwa na tukio kubwa lilikuwa linaenda kutokea. Kosa la Miller ni kwamba, alitafasri vibaya kuwa hekalu ni dunia na kutakaswa kwa Hekalu ni dunia kusafishwa kwa moto (kama ulivyoelezea vizuri kabisa).

Ukitaka kujua tafasri ya huo unabii wa siku 2,300 unakaribishwa kuuliza.
Namba 4 imenistua , unasema yes anafanya huduma ya uombezi anaomba kwa Nani sasa ikiwa nyinyi mnadai yeye ni mungu sasa anamuomba Nani msaada ,fafanua plz
 
Namba 4 imenistua , unasema yes anafanya huduma ya uombezi anaomba kwa Nani sasa ikiwa nyinyi mnadai yeye ni mungu sasa anamuomba Nani msaada ,fafanua plz
Anawaombea watenda dhambi kwa Baba yake. Mtu anapoomba msamaha wa dhambi, Yesu anayapeleka maombi hayo kwa Baba yake kwa ajili ya msamaha.
 
Hilo ndo jibu....???

Yani hizo aya zote 18 za kitabu cha Ufunuo ndio kuna Tarehe...???


Una akili timamu kweli wewe...?
Wewe huwezi kuelewa...maana unataka direct quote ya tarehe...Soma na uelewe, na bila roho mtakatifu huwezi kuelewa, unabii hauji direct kama unavyotaka wewe...
 
Wanazuoni:

Kichwa cha habari hapo juu sio kwamba ni cha uchochezi au kwamba kimelenga kupasukia watu kwa kashifa au kwamba ni kufuru kwa Mungu.La hasha, bali ni tafsiri ya kile alichomaanisha Mwanajeshi mmoja huko Marekani pale alipoibuka na Formula ya kukokotoa tarehe ya kurudi kwake Yesu duniani. Jamaa huyo anaitwa WILLIAM MILLER.

William Miller alizaliwa tarehe 15 Februari1782, huko Jimboni Massachusetts, Marekani na kisha kulelewa katika familia ya Kikristu iliyokuwa na makazi yake Jimbo la New York ya Kaskazini.Familia ya William Miller ilikuwa ya Kibaptisti. Babu yake na wajomba zake wawili walikuwa ni wachungaji katika kanisa la Wabaptisti. Kanisa la Kibaptisti, ni mumeguko karne ya 17 BK kutoka Kanisa la England,yaani Kanisa la Serikali ya Uingereza (Anglikani) ambalo leo linaitwa Lutheran Church.

Miller, katika ujana wake alipata kujiunga na jeshi laMarekani na kufikiaCheo cha Kapteini, wakati wa vita kati ya Marekani na Uingereza (Great Britain) mnamo mwaka 1812.Na inasemekana alikuwa na akili sana na kwamba alikuwa na kipaji cha kufafanua mambo.Bwana Miller baada ya kumaliza utumishi wake Jeshini na kurudi toka vitani (kati ya Marekani na Uingereza mwaka 1812), alianzisha makazi katika Shamba lake huko Low Hampton, New York, ambamo alikuwa amejenga nyumba na akawa akiishi hapo na wakati fulani akawa akienda kusali kwenye kanisa la Baptist la karibu yake.

Bwana Miller kwa kujishughulisha na mambo ya kiimani alipata kuwa mwana-DEIST,yaani alipata kuamini katika Falsafa ya Deism.

Deism ni Falsafa inayokazia kwamba Mungu hajihusishi moja kwa moja na mambo ya ulimwengu huu; kwamba yeye ndiye muumba wa vyote na kwamba ni mkamilifu lakini mungu huyo, hajiingizi katika mambo ya ulimwengu unaonekana kwa njia ya miujiza na kuwa ufunuo sio chimbuko pekee la maarifa juu ya imani na kwamba kufikiri tu kwa mwanadamu na kufanya utafiti juu ya maumbile kunatosha kufahamu na kubainisha kwamba kuna Mungu mmoja.

Kwa hiyo, tafsiri ya imani hii ya Deism ni kwamba Mungu baada ya kuumba ulimwengu alijiondokea zake na kuacha vitu vyote tuvirithi na tokea wakati huo hana mpango navyo tena na wala hajali yanayoendelea huku duniani.

SASA katika mkururu huo wa kutaka kuchimbua mambo magumu ndio William Miller alijikuta akivamia suala ambalo ndio kiini cha mjadala huu wa leo.Ni suala la tarehe ya kurudi kwa YESU KRISTU.

Ni hivi, kwa muda miaka miwili William Miller alipata kujichimbia ndani kwake “akibundi” au akibukua Biblia na ndipo katika kukisoma Kitabu cha Nabii Daniel, sura 8:13-19 ambacho kiliandikwa kabla hata Yesu hajazaliwa akagundua fomula ya kukotoa tarehe ya kurudi kwa Yesu duniani ambako inasomeka hivi:

“13.Ndipo nikamsikia mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari ya sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lini, kukanyagisha patakatifu na jeshi? 14 Akamwambia, Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa. 15 Ikawa mimi, naam, mimi Danieli, nilipoyaona maono hayo, nalitafuta kuyafahamu, na tazama, alisimama mbele yangu mmoja mfano wa mwanadamu.16 Nikasikia sauti ya mwanadamu katikati ya mto Ulai, iliyoita na kusema, Gabrieli, mfahamishe mtu huyu maono haya.17 Basi alipakaribia mahali niliposimama; nami naliogopa alipokaribia, nikaanguka kifudifudi; lakini aliniambia, Fahamu, Ee mwanadamu, kwa maana maono haya ni ya wakati wa mwisho.18 Basi alipokuwa akisema nami, nalishikwa na usingizi mzito na uso wangu uliielekea nchi; lakini alinigusa, akanisimamisha wima.19 Akaniambia, Tazama, nitakujulisha yatakayokuwa wakati wa mwisho wa ghadhabu; maana, ni ya wakati wa mwisho ulioamriwa.”

Kanuni ya Miller inadai kwamba kinabii siku moja kwa Mungu ni sawa na mwaka mmoja wa Kalenda ya wakati huo na hata sasa. Kwa msingi hiyo, siku alizoziongelea Daniel kwa jicho la Miller ni sawa na miaka 2,300 kwa kutumia Kalenda ya wakati huo ambayo ilikuwa ni ya Gregori na ambayo inatumika hadi sasa. Kalenda ya Gregori ilianza kutumika nchini Marekani mwaka 1752. (Kalenda ya Gregori ilizinduliwa rasmimwaka 1582 na kuanza kutumiwa na nchi kama Ufaransa, Italia, Polandi, Ureno na Uhispania).

Katika Sadikifu(thesis) hiyo ya Miller, alikaza kudai kwamba wapo wasomi wengine kama yeye ambao tafiti zao zimeonyesha kuwa tarehe ya kurudi kwa Yesu INAKOKOTOLEKA KIRAHISI SANA. Miongoni mwa wanazuoni waliotajwa alikuwa ni Mwanasayansi Sir Issac Newton.Huyu kwa mjibu wa Miller anadai naye alipata kufanya hesabu kama zake (alipokuwa akitafiti juu ya Kanuni za asili zinazotawala mvutano kati ya Dunia na Jua, Laws of Gravity) na kupata majibu sawa na ya Miller juu ya unabii huo wa Biblia wa kurudi kwa Yesu, na kwamba Newton aliacha maandishi mengi sana juu ya jambo hilo!

Kwa maelezo ya Miller na kwa kadri ya “ufunuo wake” na kwa kanuni yake (ya Kitabu cha Daniel) na kwa kusoma historia, aliweza kwa hakika kwa madai yake kuona kuwa mwaka wa kuanza kuhesabika hizo siku 2,300 ambazo ni sawa na miaka 2,300 ilikuwa mwaka 457K.K. Kwa hiyo, kwa kutumia alichofanya ni kuchukua huo mwaka 457BK ns kutoa miaka 2,300 na hivi kupata jibu la 1843 kwamba ndiyo ingalikuwa ni muda wa kutakaswa “patakatifu pa patakatifu.” Hata hivyo baadaye tarehe ilisogezwa mbele hadi tarehe 22 Oktoba 1844.

Mathematically,Kanuni ya Miller ilikuwa ni hii:

2,300-457=1843 (siku ya kuingia Yesu duniani).

Vigezo alivyotumia Miller katika kuthibitisha Sadikifu yake

Kuna mambo mawili Miller aliyatumia katika kuthibitisha kwamba fomula yake ilikuwa sawa:

  • Miller alidai kuwa uelewa wa watu wa wakati wake ilikuwa kwamba patakatifu pa patakatifu kulimaanisha ulimwengu wetu tunamokaa.
  • Kutakaswaa kwa Ulimwengu tena kwa moto kulikuwa na maana ya kufikia mwisho na kufikia mwisho kwa dunia maana yake ni Yesu Kurudi?
Nini kilitokea baada ya Fomula ya kurudi Yesu kugunduliwa?

Baada ya Miller kuwa amechoropoka na fomula yake alianza kupita huko na huko akiwahubiria watu ili wachukue tahadhari kwa kujiandaa kumpokea Yesu.Miongoni mwao alikuwa mwanamama anayedaiwa kuwa “Nabii mahiri” sana kuwahi kutokea hapa duniani(kwa sababu aliwahi kupewa maono zaidi ya 2000) kusimika usabato duniani na ambaye anatajwa kuwa ndiye amepewa “maono” juu ya jinsi ambavyo Papa atawafumusha wasabato waanze kusali Jumamosi siku zijazo.

Msimamo wa yesu juu ya mwisho wa dunia

Utakumbuka kuwa Kitabu cha Daniel kiliandikwa miaka mingi sana kabla Yesu hajazaliwa.Na utaona kwamba hata Kanuni ya Miller juu ya kurudi kwake ilianza kuhesabiwa mwaka 457BK. Kwa hiyo, wakati Yesu anazaliwa kitabu cha Daniel kilikuwepo tayari na hizo habari za kutakaswa Patakatifu pa Patakatifu Yesu alikuwa amezisoma.

Pamoja na ukweli huo wote kwamba Yesu alikuwa amekisoma kitabu hicho bado alipoulizwa juu ya mwisho wa dunia alisema hivi kwa kadri ya Injili ya Matayo 24:35-38:

“35 Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.36 Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.37 Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.38 Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina.”

Analysis ya Sadikifu ya “Mwanahisabati” Miller

Kwa kuisoma Sadikifu (thesis) ya Miller na msimamo wa Yesu juu ya mwisho wa dunia,yafuatayo yanajitokeza:

1. Miller na wenzie walikosea wapi katika fomula yao kiasi kwamba Yesu hajawahi kuonekana toka mwaka 1843?

2. Je, wanahisabati wanaweza kuendeleza pale Miller na wenzie walipoishia katika kukokotoa mwisho wa dunia kwa kuihakiki hiyo fomula ya Kisabato juu ya kurudi kwa Yesu?

3. Je, Miller na wenzie hawakuwa wamefanikiwa kulisoma Agano Jipya ambamo msimamo wa Yesu juu ya tarehe ya mwisho wa dunia unawekwa wazi wazi kuwa tarehe husika haijulikani?

4. Je, ikiwa Miller na wafuasi wake akiwemo Mama wa “maono”,Ellen White, walikuwa wamelisoma Agano Jipya ni kwa nini wao waliamua kuasisi Fomula ya jambo ambalo Yesu alikwisha kusema hana uwezo nalo?

5. Je, kwa Yesu kusema haijui tarehe halafu Miller na Ellen White wakaja wakasema wanaifahamu tarehe ina maana Wasabato hao na wa leo mbingu ni yao kiasi kwamba wanaingia na kutoka hata wameweza kushirikishwa yanayoendelea huko Mbinguni?

6. Je, kwa Miller na Ellen kukubaliana kwamba wao walikuwa wameipata fomula ya kurudi kwa Yesu walimaanisha kwamba wao walikuwa ni wasomi sana na kwamba Yesu kusema haijui tarehe kulimaanisha Yesu alikisoma Kitabu cha Daniel na kutokikielewa au kwamba Yesu alikuwa anasoma mambo kwa kurukaruka?

7. Je, hadi sasa tumsikilize nani kati ya Yesu na wasabato juu ya mwisho wa dunia kwa sababu Ellen White ameshapewa maono yanayoonyesha kwamba Yesu ameshaanza kushuka na kwamba kwa sasa yuko katika chumba cha patakatifu pa patakatifu sana ambako anapitia majina ya wasabato na akitoka hapo moja kwa moja anatia timu hapa duniani?


Kwa yote hayo,sasa KARIBUNI kwa mjadala.
Kuna neno maarufu linaitwa MPINGA KRISTO.
ambalo kwa bahati mbaya walishabatizwa wakatoliki,lkn tujiuli kitu hapa,
Yesu alisema hakuna ajiaye siku wala SAA ila baba
Miller na Eg wakasema wanaijia na wakaitabiri,
Maana yake nini,
Waliipinga kauli ya Yesu,
Walimfanya Yesu kuwa muongo,
Huo ndo upinga Kristo
 
Back
Top Bottom