William Miller: Kama Yesu hakujua Hisabati au kutafsiri mambo bora angalikaa Kimya. Mbona siku ya mwisho wa dunia inakokotoleka kirahisi?

William Miller: Kama Yesu hakujua Hisabati au kutafsiri mambo bora angalikaa Kimya. Mbona siku ya mwisho wa dunia inakokotoleka kirahisi?

Hayo maombezi,Yesu anawaombea akina nani hapo "chumbani patakatifu pa patakatifu'?
Ungekuwa unajua dhana ya huduma ya hekaluni toka kipindi cha agano la kale na nini kuhani alikuwa akifanya alipokuwa anaingia katika chumba cha patakatifu pa patakatifu mara moja kwa mwaka...ungejua Yesu akiwa kuhani wetu mkuu anafanya nini hapo patakatifu pa patakatifu pa Mungumi.
 
Mkuu tulia...usome mada uelewe.....

Hebu tuanbie labda itawezekanaje huyo Papa kuwalazimisha watu kusali Jumapili angali dunia hii kuna uhuru wa kuabudu....mbona ni kichekesho cha karne hiki...

Haya labda utuambie haya umeyapatia wapi....?
Ndugu yangu haya mambo ni makubwa sana...kama husomi biblia huwezi kujua...nakushauri soma vizuri kitabu cha Daniel chote na Ufunuo...humo ndiyo mambo yote utayapata. Ila inatakiwa umuombe sana Mungu akupe roho wake uelewe vinginevyo utatoka kapa.

Kuhusu watu kulazimishwa kusali siku ya Jumapili ipo inakuja...Soma Ufunuo 13, utaipata, na kama ni mfutiliaji wa mambo, kuna kitu kinaitwa One World Religion, ambacho kimeshaanza kufanyiwa kazi.

Mwaka 1999, viongozi wa makanisa yote ya Kiprotestant na Roman Catholic walisaini makubaliano ya kuondoa tofauti zao, ili kuwa kitu kimoja. Na Octoba mwaka jana, katika kuazimisha miaka 500 ya uprotestant, ulioanzishwa na Martin Luther alipoandika mambo 93 ambayo alikuwa anapingana na kanisa la Roman Catholic, kanisa la Lutheran lilisaini declaration ya kumalizika kwa uprotestant. Kama unafuatialia mambo utakuwa unajua hili. Hii ni mwanzo wa One World Religion.
 
Mwanzoni ulimkana Miller na sasa kwa ujanja unakubali.... Hiki ni kituko kingine...ehhhh
,

Hapa ndio pa tamu sasa.....Kama ulikuea hunui Bwana Joseph Bates ndiye aliyanza kumsafisha William Miller baada ya Great Disappointment....kisha baadae ndio akaja Bi Ellen G White.....





Sasa mkuu wewe unsonekana una uelewa kidogo wa mambo ya Kisabato...utatusaidia kujibu maswali yetu ...

japo umeanza kwa kukanusha kuwa humjui miller na wala hakuna msabato na hana mahusiano na usabato, hali kijanja ukaja kumkubali.....
Ni wapi nimemkana Miller?
 
Hayo maombezi,Yesu anawaombea akina nani hapo "chumbani patakatifu pa patakatifu'?
Anawaombea wakosaji wote. Hujui kwamba Yesu ni mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu. Kila unapotenda dhambi na unapotubu Yesu anapeleka maombi yako mbele za Baba yake ili usamehewe?
 
Ungekuwa unajua dhana ya huduma ya hekaluni toka kipindi cha agano la kale na nini kuhani alikuwa akifanya alipokuwa anaingia katika chumba cha patakatifu pa patakatifu mara moja kwa mwaka...ungejua Yesu akiwa kuhani wetu mkuu anafanya nini hapo patakatifu pa patakatifu pa Mungumi.

1. Tupatie andiko kwamba Mbingu ina vyumba au horizons.
2. Yesu ni Mungu na hivi ana uwezo wa kutuombea akiwa popote pale.je,kulikuwa na ulazima gani kwake kuingia huko Chumbani("patakatifu pa patakatifu") toka mwaka 1844 hadi leo ili kufanya tu hiyo huduma ya maombezi?
3. Ellen White yeye alifundisha kwamba Yesu yuko hapa patakatifu pa patakatifu akiendesha hukumu ya kipelelezi(Investigative Judgement).Je, huduma ya maombezi ni hukumu ya upelelezi?
 
Najua vizuri sana...uliza swali nitakujibu!

Miller, ndiye muanzilishi wa doctrine ya "Unabii",akianzia na unabii wa Kurudi upesi kwa Yesu(imminent advent).Hiyo ndio mada ya leo.Sasa hebu tuambie fomula ya Miller ilikuwa sawa na kama haikuwa sawa, tueleze wale wafuasi wake waliokaza juu ya fundisho la unabii tuwaamini vipi? Ni kwa vipi kama nao waliweza kukubaliana na Miller, nao leo hii wasihesabike wapotoshaji tu maana wamejenga juu ya msingi wa Miller?
 
Wewe....hivi kweli na wewe unajiita binadamu kama mambo madogo haya huyajui..

Kalenda hii yaani mf..leo ni tarehe 31/10/2018 ni Gregorian Calender ....

Ni Kalenda ya Kanisa Katoliki ..kwa kirefu inaitwa Pope Gregory Calender...(Gregorian)
Mkuu usi panic na kuanza kutawanya matusi kwa nadharia hewani.
Ungejibu "NDIO" ungeingia kwenye kundi la waungwana!
 
Ndugu yangu haya mambo ni makubwa sana...kama husomi biblia huwezi kujua...nakushauri soma vizuri kitabu cha Daniel chote na Ufunuo
Aliyekuambia mimi kuwa hivyo vitabu sijasoma mpaka mmoja anipe ushauri wa kuvielewa na nani...?

Kwanini unataka nivielewe kwa jinsi yako wewe(Ellen G White kind of Thinking)


Wewe ndiye unayepaswa kukaa chini na tukufundishe maana y vitabu vyenye maandishi ya Kiapokaliptiki
 
Mwaka 1999, viongozi wa makanisa yote ya Kiprotestant na Roman Catholic walisaini makubaliano ya kuondoa tofauti zao, ili kuwa kitu kimoja. Na Octoba mwaka jana, katika kuazimisha miaka 500 ya uprotestant, ulioanzishwa na Martin Luther alipoandika mambo 93 ambayo alikuwa anapingana na kanisa la Roman Catholic, kanisa la Lutheran lilisaini declaration ya kumalizika kwa uprotestant. Kama unafuatialia mambo utakuwa unajua hili. Hii ni mwanzo wa One World Religion
Hebu tutolee hekaya zako za abunuasi hapa...
 
Back
Top Bottom