Yuko sahihi, Dola ni mateso makubwa, si kwa Afrika tu, bali dunia nzima. Fikiria nchi yenye matumizi makubwa kama USA iwe inajichapishia pesa halafu zinatumika dunia nzima!! Yaani kiuhalisia ni kuwa wakitaka mafuta au kahawa au dhahabu wanachapisha tu pesa na kuja kununua huku kwetu. Wengine wanahangaika kuzalisha bidhaa wao wanachapa tu pesa.
Nchi za Afrika zinatakiwa kujiongeza.