Wimbi kubwa la vijana wasomi 20's kujitoa uhai, nini maoni yako?

Chanzo kikubwa ambacho nitakiongelea kwa kifupi ni "ni kuwa na ndoto za kufika sehemu fulani bila ya kuwa na plans za how utafika hiyo sehemu fulani.

Pia ukosefu wa elimu sio ile ya kukariri bali elimu ya maarifa na akili vijana wengi hawajitambui.
 
Kuna mmoja alijinyonga ijumaa maziko jumapili jumamosi kaja rafiki yake aliyetumia sanduku lake la posta kuombea ajira ikimtaka jumatatu akaripoti ofisi kubwa yenye mshahara mzuri.
Somo usikate tamaa ukiona Giza limezidi
 
Kitapunguza ndio kwani hujui? Mumeshaambiwa elimu itafumuliwa iwe skills based na upate maarifa ya kushindana kidunia sasa unahitimu phd afu unakuwa Kama huyu wa sasa hata lugha hujui atakuajiri nani huko duniani? Kwa nini usipatwe na msongo wa mawazo? Huku TL katuambia biashara ni 24hrs sio mchana tu,hapo msongo wa mawazo utatoka wapi?
Nilime miti yangu au mazao nk afu nikianza kuvuna niambiwe sijui lipia hiki Mara staksbadhi gharani sijui mipaka imefungwa sasa kwa ghasia hizi za miccm na mikodi lundo Hadi vitambulisho utaacha kupata msongo?
Endeleeni kuchagua ccm na bado ,kuanzia 2025 Hali ndio itaanza kuwa mbaya zaidi maana maelfu kwa maelfu ya vijana watakuwa kitaa na kazi wanazotegemea za bodaboda na bajaj zitakuwa floaded kiasi kwamba haitalipa tena.
 
Safi sana kijana! Maamuzi na hatua uliyochukuwa ndiyo sahihi.
Tanzania bado kuna fursa nyingi ukizitumia vema; maisha yanakwenda.
Mfumo wa elimu yetu siyo rafiki kumpika kijana ajiajiri; unamwandaa kijana kuajiriwa hata kama mazingira ya ajira hiyo hayamhakikishii future yenye tumaini, "white collar".
Hongera sana kijana!
 
Eti Tundu Lissu kawaambia,za kuambiwa changanya na zako...
 
Jitahidi kusomesha watoto wako elimu ya kiafrika ya uwajibikaji hasa shambani na msoto wa hapa na pale,wakikosa watapata siku moja na si kujiua..achana na elimu hii iliyo jaa misingi ya kigeni wasomi wa kisasa wanaotazama tamthilia na kuzani maisha ndo hayo ilihali wakienda makwao wazazi wanalalia vitanda vya kichanja,wanapata stress na kuishia pabaya,mzungu alituweza lakini tumaweza kubadirisha mtazamo
 
Mimi na wewe sote tunajua unachomaanisha. Ugaidi unafanyika kisiri na hata kupambana nao pia kisiri hivyohivyo, kuwa mpole
Ulichomaanisha wewe sicho nilichomaanisha mimi, fisi ni mnyama hatari awapo kwenye makazi ya binadamu, hakuna kosa lolote kujilipua kwenye mkusanyiko wa fisi, upo hapo ?
 
Kujiua kwa kijana si jambo jipya. Ninawafahamu vijana wawili waliofanya hivyo miaka ya 70. Mmoja alikuwa ameanza kazi baada ya kuhitimu Chuo Kikuu cha Dar. Alikuwa akiishi kwa ndugu yake; akampa mimba mfanyakazi wa ndani wa hapo nyumbani. Kwa aibu hiyo, akaenda UDSM akapanda gorofa la Hall 2 akajirusha chini akafa. Miezi michache iliyotangulia mwingine naye alijirusha kutoka jengo la Kitega Uchumi lililopo karibu na Benki Kuu au Mahakama Kuu. Alikuwa ametunukiwa shahada ya chuo kikuu na umri wake ulikuwa 20-na. Kwa hiyo hili jambo si kwamba limeanza leo eti kwa ajili ya ugumu wa maisha ulioletwa na Serikali ya Awamu ya Tano kama anavyoashiria mtoa mada.
 
Kujiua ni kazi ya shetani katika ulimwengu wa roho. Haina uhusiano na kukosa ajira.
 
dah wakuu mimi nimegraduate dec 2019,,nna miez 9 t mtaani ila sielewi kbsa..hii hali ni changamoto kweli acha watu wajinyonge t wakapumzike..matarajio ya wanaokutazama yanakua makubwa kweli kuliko uhalisia.

ushauri kwa graduate wenzngu tafuta kitu angalau kimoja kikupe maana na ham ya kuish maisha yaendele .mie furaha yangu sasaivi ni simba sposi tu,nacheki mbungi la chama langu la simba uku nakunywa pepsi ya jero maisha yanasonga. Eng.ilala yetu.
kama kuna mchongo wowote wa halalai kuingiza miambili mia tatu tustuane wakuu.
 
Cha kwanza nakushauri kama bado uko nyumbani ondoka nenda hata mkoa mwingine kaanze maisha from scratch, weka malengo fanya biashara yoyote utatoboa tu.
 
The Power of positive thinking, kama ningekua sijakisoma hiki kitabu uenda muda huu ningekua na kesi ya kujitoa uhai kwa Mungu tangu 2017. Natamani niandike historia yangu kwa niliyopitia japo bado sipo vzr lkn nimeachana na stress zilizotaka kusababisha nijiue.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…