Wanabodi,
Kati ya Taasisi zinazopaswa kufanya kazi kwa weledi mkubwa bila mihemuko ni Jeshi Letu la Polisi.
Kuna baadhi ya issues ambazo jeshi letu la polisi, zinazishughulikia sio issues za kipolisi, ni issues za kijamii na kifamilia.
Kwanza msikilize Kamanda Polisi Huyu
Kisha isome taarifa hii ya Jeshi la polisi
View attachment 2237214
Paskali
- Kazi ya Jeshi la polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zake. Kukitokea kitisho cha usalama au mtu ametoweka hajulikani alipo, ndugu wa mhusika huripoti polisi na polisi kufanya uchunguzi.
- Tukio la kutoweka kwa diwani huyu, halikuripotiwa kituo chochote cha polisi na ndugu yake yoyote, bali Bosi wake, Meya wa Kinondoni alitangaza kwa waandishi wa habari kuwa Diwani hajafika kazini, na nyumbani kwake hayupo.
- Nianze kwa kutoa pongezi kwa Jeshi letu la Polisi, kumbe siku hizi, linazifanyia kazi taarifa za mitandaoni!. Tundu Lissu kabla hajashambuliwa alitoa taarifa kupitia vyombo vya habari, kuwa usalama wake uko mashakani, kuna gari inafuatilia, hadi akaitaja mpaka number!. Jeshi la polisi lilijibu kuwa hawafanyii kazi taarifa za vyombo vya habari, kama ni issues yoyote, Lissu akaripoti polisi ndipo jeshi la polisi lishughulikie!.
- Tukio la kutoweka kwa diwani huyu halikuripotiwa kituo chochote cha polisi zaidi ya vyombo vya habari, kumbe sasa jeshi letu la polisi liko makini kufuatilia taarifa za mitandao ya jamii!. Big up for this.
- Hakuna jinai yoyote ya mtu kutoripoti kazini, mtu asiporipoti kazini taratibu za kiofisi ndizo hutumika. Pia hakuna jinai yoyote mtu kunywa pombe, as long as hujafanya jinai yoyote. Na hakuna jinai yoyote, mtu yoyote kuhama nyumbani kwake na kuhamia mahali popote, hizi ni issues za kijamii za kifamilia.
- Baada ya Diwani kupatikana, kulikuwa na haja gani polisi kusema alikuwa kwa mwanamke, na kumtaja jina!, huku ni kuingilia the right to privacy.
- Hata kama huyu mwanamke ameripoti mtu wake alikuja akiwa amelewa, inawahusu nini polisi kuripoti?, huku ni kumchafua diwani wetu kumuonyeshea ni mlevi!.
- Kwa vile hakuna ndugu yoyote aliyemripoti kupotea, polisi baada ya kumkuta Tabata, walimkama kumpeleka kituoni kwa kosa gani?!. Jukumu la polisi baada ya kumpata, ilikuwa ni kumpa tuu taarifa Meya, kuwa Diwani wake yuko salama, taarifa ya polisi ingeishia kusema amepatikana, hiyo amepatikana wapi, kwa nani, jina la mwanamke hadi kabila lake na uhusiano wao wa miaka 10, ilikuwa inahusu nini?.
- This is pure sensationalism, tusiruhusu sensationalism za aina hii kwenye jeshi letu la polisi.
- Taarifa hii ni an ethical, ni udhalilishaji wa kumdhalilisha diwani wetu, taarifa hii inaingilia the right to privacy ya diwani wetu, tutabadili sheria zetu za uwakili kuruhusu kesi za pro borno, jeshi la polisi hapa linashitakiwa kwa defamation by innuendo, na mtu anashinda kesi mapema asubuhi!.
Leo angalau hujakashifu CDM, kulikoni?