Wito kwa Bunge la Katiba: Kura iwe ya Siri kwasababu Hakuna aliyetumwa na Watu Kuwawakilisha!

Mara nyingi nimesikia watu wakisema wabunge wa bunge hili ni watu wazima ,na rais kachagua wanasiasa wa zamani
na wasomi kwa misingi ya hekima zao na kama ni wabunge wa majimbo tayari waliishachaguliwa na wananchi wao
na wale wa makundi maalum wametumwa na makundi hayo kwa kuamini kwamba watawawakilisha vema
sasa huu woga wa kusema tunataka kura ya wazi ili tuone wanachokifanya unatoka wapi?
Hii inanipa maswali kama vile,wamewekwa kwa makusudi na hivyo aliyewaweka ana wasiwasi kwamba wanaweza mtosa endapo hawatafanya kwa wazi, hivyo anataka uwazi ili aweze kuwabana au hatuna uhakika na uwezo wao wa kimaamuzi maana wamezoeshwa kuendeshwa kama roboti.Vinginevyo tuamini kwamba watafanya maamuzi kama tulivyowaamini.
Kama hoja ni kuwaona wakituwakilisha,Kura ya wazi itawanufaisha waliomijini ni asilimia ndogo huku asilimia kubwa ya watanzania ipo vijijini ambako hakuna umeme na sehemu zenye umeme ni wachache wenye vingamzi kuona runinga
Hivyo dhana hii ya uwazi naona imewalenga wenye maslahi binafsi wanaoishi mijini ili kufanikisha malengo yao.
 

Nataka kura ya siri ili Tanganyika irejee. Hakuna Tanzania bila Tanganyika na Zanzibar. Kura ya wazi ni kutaka kuzuia Tanganyika isiwepo ukizingatia wajumbe wa bunge la muungano hatukuwa tumewachagua ili kutuwakilisha katika bunge la katiba. Na hawakurudi kutuuliza badala yake wanaingia kwa msimamo wa vyama vyao. kwa maana vyama vyao vimewapa misimamo. Na sisi tusio na vyama au makundi nani anatusemea? Kwa hiyo msimamo ni KURA YA SIRI.
 

hakuna chama kama chama kilichojisimamisha wenyewe msimamo lazima urudi kwa wananchi wanataka nini siyo kufuata chama., ww anzisha chama chako peke yako halafu utaenda kule bungeni utoe msimamo wa chama chako kilichokutuma
 
hakuna chama kama chama kilichojisimamisha wenyewe msimamo lazima urudi kwa wananchi wanataka nini siyo kufuata chama., ww anzisha chama chako peke yako halafu utaenda kule bungeni utoe msimamo wa chama chako kilichokutuma

Bado naona hunielewi,zipo nafasi rasmi za wawakilishi wa vyama vya siasa,hawa lazima wasimamie msimamo wa vyama vyao, na wabunge wasimamie hoja za wananchi wa majimbo yao kwa uwazi ili kila anayewakilishwa aone namna alivyowaskilishwa.
 
Wengi wetu hata huku tulipo hakuna umeme wala luninga. Na hata luninga ikiwepo nasikia TBC ni noma sana! Mnadhani tutawaonaje? Wanaosema tumewatuma kwa msimamo wa kura ya wazi ni waongo wanaotaka kupitisha hoja zao kwa hila. Twajua kuwa kura ya kidemokrasia ni ile ya siri!
 
Kura ya wazi imewatia hofu wajumbe wengi kutokana na msimamo wa CCM kutaka wawakilishi wote ambao wanatokana na Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano pamoja na Wajumbe wanaotokana na Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitia chama hicho ccm wapige kura kwa matakwa ya chama chao wala sio utashi wa wananchi wanaowawakiliaha. Tayari habari zinasema Wabunge 90 wa CCM wamekuwa BLACK LISTED na chama chao na wanaitwa mmoja mmoja kuhojiwa kutokana na msimamo wao wa wazi unaokinzana na matakwa ya chama. hayo ni mabavu ya ccm kujaribu kuwalazimisha wawakilishi wa wananchi. Kwa mtazamo huu, KURA YA SIRI NI MUHIMU.
 
ccm hawataki katiba mpya wanataka kupoteza muda uchaguzi ufike
 
Hivi kuna watu wenye matatizo ya akili humu JF?

Maana naona kuna watu wamekuwa wabobezi wa kuandika pumba tu.

Sasa mtu kama huyu mleta mada si anatia huruma tu?

Hemu tazameni jinsi alivyo andika kwanza, huko kwenye hoja ndio upuuzi mtupu.

Hivi ni nani kasema kura ya wazi itazuia chochote?
 
naunga mkono hoja. kura ya siri ndo mpango mzima. wasituletee za kuleta, ujanja ujanja kwenye mambo ya msingi haufai mbona kura zingine zote huwa ni za siri kwanini hizi za kupitisha ibara za rasimu ndo ziwe za wazi?. nyambafu.
 
Mchakoto huu toka mwanzo ni batili,sina sababu yeyote ya kukubali huu uchafu
 
Wanaoshikilia msimamo kura iwe ya wazi ni wabaya wa Taifa hili La Tanzania na hao wanafaa kupigwa vita ,popote pale penye hofu penye mavutano basi kura ya siri ndio suluhisho.

Kura ya siri huwezi kuonekana mbaya wala mzuri ,baada ya kutoka matokeo utakuwa uwamuzi ulio na busara kubwa wala hakutokuwa na kunyoosheana vidole wala kulipiza kisasi au kufukuzana ,na hata wale waliokuwa au pale panapoashiria watu kutishana ikiwa utapigia huku au kule ,kutakuwa hakupo ,hataweza mtu kumshuku au kumtuhumu mwengine zaidi ya kila mmoja kumtolea mijicho mwenziwe ,lakini hawezi kumwambia kitu kwani hapo ndio pale umdhania ndie kumbe sie.
 
Bado naona hunielewi,zipo nafasi rasmi za wawakilishi wa vyama vya siasa,hawa lazima wasimamie msimamo wa vyama vyao, na wabunge wasimamie hoja za wananchi wa majimbo yao kwa uwazi ili kila anayewakilishwa aone namna alivyowaskilishwa.

hakuna ulazima labda iwe msimamo wa chama ndio msimamo wa wananchi.,
 

naona sindano inakuingia taribuuu
 
Semea nafsi yako sio wananchi wote wanataka kura ya siri mimi binafsi kura ya siri sioni kama ina mantik yoyote ktk kupitisha katiba hao wajumbe walioko bungeni kila mtu ana interest zake sio ccm tu hata cdm hao mnaowasikiliza hakuna anaetafuta katiba ya wananchi pale wote wanafiki tu! lakini kiuhalisia tukiacha na ushabiki wa kisiasa kura ya dhahiri ndio inayofaa kutoa maamuzi kuhusu katiba kwa sababu hii ni serious inshu kwa ajili ya wananchi wote na si kwa ajili ya watu fulani
 
kuna watu vichwa ngumu sana hivi nani hajui kama ccm wana wasi wasi kupiga kura ya siri kwa sababu kuna wana ccm wengi tu ambao hawakubaliani na msimamo wa chama chao? kura ya wazi ni kulazimisha maamzi.
 
Nani amewaroga ccm?ukiwaona kwa macho utazania ni watu.kumbe mioyo yao inakutu ya kutaka kuchonganisha.kama ccm mnatetea kura ya wazi,basi pendekezeni katiba mpya itamke tuwe tunapiga kura ya wazi kwenye uchaguzi mkuu.acheni ulimbukeni.tumewachoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…