Wito kwa Serikali: Gharama za Vivuko vya Azam Kigamboni-Magogoni iangaliwe Upya

Mkuu you can not have your cake and eat it too... Kwahio kama ni mtu binafsi amewekeza na usimpangie bei.., muache yeye afanye anavyojua huenda yeye target yake ni premium customers...

Dawa ya hili jambo Serikali iwe na Vivuko vyake vya UMMA vya kutoa huduma (yaani hapa kigezo iwe affordability) ?

Lakini kutokana na Upeo wetu mfupi hata vya UMMA vyote na kila kilicho cha UMMA nacho tunataka kubinafisha...

 
Wameua kile kivuko kimoja ili vibaki vivuko vya azam na matokeo ndio kama hayo, bei kuongezeka.

Watengeneze kivuko walichokiharibu ilhali wananchi wanalipa nauli, serikali ilete vivuko vingi. Suala la kuvuka sio la kibiashara ni la lazima, ni jukumu la serikali kupitia kodi za wananchi.
 
Izingatiwe kuwa suala la vivuko sio biashara huria. Ni serikali tu ndio yenye mamlaka ya kuwa na vivuko. Kwa hiyo hata Azam kuwa na kivuko ilikuwa ni kwa ruhusa na makubaliano maalum, kwa hiyo makubaliano hayo yasitumike kama mwanya wa viongozi kujipigia hela kwa mgongo wa Azam
 
Sawa sawa, kingine serikali uchek kama kuna uwezekano wa kusubsize au kutoa unafuu wa kikodi kwa azam, tusilazimishe bei iwe nafuu tu
 
Serikali ijenge daraja, iache kukimbia kivuli chake
 
Serikali imeamua kufanya kuwa biashara
 
Iwe Soko Huria ila Serikali iwe na mali yake na Vivuko vyake na wala isiwe UBIA wala PPPs Serikali ihusike hundred percent kwenye hizi huduma ila mtu asikatazwe kutoa Huduma hizo kwa faida hata kama akitaka acharge kwa milioni kila mteja all the best..., unless kama anatumia limited facility ambayo Serikali haiwezi kufanya hivyo sehemu nyingine au mtu mwingine sehemu nyingine sioni tatizo la kumkata mtu kuwekeza as they see fit... hio itakuwa ni chochote kati ya hizi hapa chini

Binafsi nachopenda kila mtu afanye anachofanya kwa faida yake wala asikatazwe ila sababu UMMA tunatoa KODI basi sio Hisani inabidi na ni lazima watupe hizo HUDUMA as long as wanakusanya KODI (Market Socialism)

 
Serikali inavyowaona wananchi wake kama maadui namba moja wa nchi. Hiyo gharama haitoshuka

Vivukovya distance ya kigamboni ni bure duniani kote kasoro Tanzania tu
 
itabidi wajifunze kuogelea aisee!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…